Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, November 19, 2009

Vodacom Tanzania yamwaga 25m/- Zenji kwa Mapinduzi Cup

Mkurugenzi masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 25 kwa naibu waziri kiongozi na waziri wa habari utamaduni na michezo wa Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna kwa ajili ya udhamini wao wa kombe la Mapinduzi kwenye sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya zanzibar ocean view leo.


Naibu waziri kiongozi na waziri wa habari utamaduni na michezo zanzibar, Mh. Ali Juma Shamhuna akiongea kwenye hafla ya kupokea hundi ya sh.milioni 25 udhamini wa Vodacom Tanzania kwa kombe la mapinduzi 2010. hafla ilifanyika kwenye hoteli ya zanzibar ocean view.

Read more...

UNFPA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Batilda Burian akizinduwa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani Kulia Mwakilishi wa (UNFPA) Nchini Tanzania Dk Juliha Onabanjo katika ofisi za UN Kinondoni Dar es Salaam.

Read more...

Same

Businesspeople sell maize at a weekly open market at Ndungu in Same District, Kilimanjaro Region. Several villages in the district face an acute food shortage. (Photo by Mroki Mroki)

Read more...

Lugha Gongana

Nimeletewa picha hii na da mau akisema kwanini watu tunalalamikia kiinglish wakati ni lugha ya kuvunjwa kila mahali. hapa alikuwa shanghai China na umombo wenyewe si unauona yaani ndio tafsiri ya hicho kilichoandikwa kikwao. Picha Toka kwa Lukwangule

Read more...

Wednesday, November 18, 2009

Busara 2010

Mtanange wa saba wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 11 hadi 16 Februari 2010; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya saa kumi na moja.Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.

Read more...

Hatimaye Kombe la Dunia kutinga Tanzania

Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa juu ya maandalizi ya ujio wa kombe la Dunia linalotarajiwa kuwasili kesho na kuzinduliwa kesho hiyohiyo na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete saa kumi jioni, ambapo pia mashabiki mbalimbali watapata fursa ya kupiga nalo picha kwa kumbukumbu kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika nchi nyingine.

Read more...

Serengeti yamwaga mamilioni kwa Kisura wa Tanzania


Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akikabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi Milioni 35 kwa meneja mradi wa Kisura wa Tanzania Grace Kilembe huku kisura wa Tanzania 2008 Emmy Nelau na Meneja mkuu wa Serengeti Winston Kagusa waliosimama katikati wakishuhudia tukio hilo lililofanyika kiwandani hapo, aliyesimama kushoto ni Brand Manager wa Kampuni hiyo Nandi Mwiyombela, shindano la kisura wa Tanzania linatarajiwa kufanyika Disemba mosi mwaka huu kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar se salaam.

Read more...

Mchuma wa Fiesta

Meneja Matukio na Promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh naye alipata nafasi ya kuweka saini katika gari hilo.


Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akiweka saini kwenye gari aina ya Mitsubishi pajero linalotarajiwa kutolewa kwa mshindi wa bahati nasibu mashabiki wa Fiesta One Love itakayofanyika sambamba na tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya posta Kijitonyama, mashabiki watapata nafasi ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo kutokana na tiketi zao walizokata ili kuingia kwenye tamasha hilo ambapo wasanii mbalimbali watatoa burudani kutoka hapa nchini na nje ya nchi akiwemo mkali wa Hiphop kutoka nchini Marekani
Busta Rymes, kweli hii ni Fiesta one Love

Read more...

Mh. Burian na ujumbe wa EU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Batilda Burian akizungumza na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya{EU} kulia kwa Waziri ni Balozi wa Sweden Bw Staffan Herrstrom na Balozi wa Jumui ya Ulaya Bw Tim Clarke uliomtembelea na Kumweleza msimamo wao Kuhusu Mabadiliko wa Tabianchi kuelekea Mkutano wa Denmmark. Picha na Ali Meja

Read more...

Mh. Sitta amtembelea Dk. Migiro New York

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe.Samuel Sitta akisalimiana na Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha - Rose Migiro alipomtembelea ofisini kwake, makao makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani leo. Spika yupo Jijini New York kuhudhuria Mkutano wa pili wa kamati ya maandali ya mkutano wa Maspika wa Mabunge Duniani utakaofanyika Julai 2010 huko Geneva. Chini wakiwa na Afisa habari wa Bunge Owen Mwandumbya wa Bunge.



Read more...

Rukwa na Matukio.

MAFUNDI wakijenga daraja lililopo maeneo ya Majengo katika Manuspaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa hivi leo. Daraja hili limeharibiwa vibaya kutoka na mvua kubwa za msimu uliopita na zinazoendelea kunyesha msimu huu katika maeneo mengi mkoani humo.

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Msakila High School katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wakishiriki katika ujenzi wa uzio wa shule yao kwa njia ya kujitolea leo
Picha na Rukwa Peti Siyame

Read more...

Mama Kikwete katika ziara ya Manyoni.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amebeba kibuyu mara baada ya kukabidhiwa na wanawake wa kabila la wataturu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika mkoa wa Singida. Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.(


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari Itigi msaada wa magodoro 20 kwa ajili ya hosteli ya wanafunzi wasichana wa shule hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelekezo kutoka kwa Mikasi Mpembee kuhusu jinsi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ya uyanjo VICOBA inavyofanya kazi. Taasisi ya WAMA iliichangia Uyanjo VICOBA Tshs.1,000,000/= fedha ambazo zitatumika kuinua mtaji wa biashara.
(Picha na Juma Kengele - Ikulu)


Read more...

Monday, November 16, 2009

TBC SPORTS CLUB WAPEWA JEZI

TAJI LIUNDI(KULIA)-meneja wa timu ya shirika la utangazaji Tanzania (tbc sports club)akipokea jezi kutoka kwa TEDY MAPUNDA-meneja wa uhusiano,habari na mawasilino wa SERENGETI BREWERIES(SBL).msaaa wa jezi juu na chini 20 na mipira mitano.vyote vinathamani ya shilingi laki 8.TBC SPORTS CLUB kwa sasa ipo TANGA ikishiriki michuano ya mashirika ya umma na makampuni binafsi SHIMMUTA.

Read more...

Youssou Nd'our atembelea Clouds Fm

Mwanamuziki nyota wa kimataifa toka nchini Senegal, Youssou Nd'our akizawadiwa fulanazzz na Mkurugenzi wa Clouds Media Group/Prime Time Promotions Bw.Joseph Kusaga mchana huu.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group/Prime Time Promotions Bw.Joseph Kusaga akizungumza mchana huu ofisini kwake Mikocheni jijini Dar na Mwanamuziki nyota wa kimataifa toka nchini Senegal, Youssou Nd'our

Read more...

Washindi wa chemsha bongo wazawadiwa

Kulia ni Deputy HR Manager (Afisa Rasilimali Watu) wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Laptop kwa mshindi wa PILI wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO Hassan Mohamed wa MBAGALA, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita.


Kushoto ni Deputy HR Manager (Afisa Rasilimali Watu) wa Tigo Bennett Kakorozya akikabidhi zawadi ya Plasma TV Inch 26 kwa mshindi wa kwanza wa promosheni ya TIGO CHEMSHA BONGO Jamal Jumbe wa KINONDONI, katikati ni Tawonga Mpore Ofisa huduma za ziada Tigo na Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando wakishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo ofisi za Tigo makao makuu. kushiriki Mteja alitakiwa kutuma neno SWALI kwenda 15550 na kisha alianza kupokea maswali mbalimbali kutoka Tigo kwa mwezi mmoja uliopita

Read more...

Mama Kikwete katika ziara ya Bahi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpima uzito mtoto Jonathani Deogratus mwenye umri wa miezi kumi ambaye alipatikana na uzito wa kilo 11.5 huku mama wa mtoto huo Rosemary Deogratus akimsaidia kuweka kwenye mzani wakati alipotembelea kituo cha afya Kigwe kilichopo wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Dodoma mjini kuhusu kujitokeza kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa kijiji cha Kigwe juu ya kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa maralia wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo katika wilaya ya Bhi mkoani Dodoma kwa ajili ya kuwapatia msaada wa vifaa mbalimbali vya afya.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amevaa vazi la asili la kabila la wagogo mara baada ya kuvalishwa na wakazi wa kijiji cha Mdemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.



Mke wa Rais Mwalimu Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisahihisha daftari la Lea Wimbe ambaye ni mlemavu wa kusikia mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya viziwi Kigwe. Mama Kikwete alitembelea shuleni hapo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma

Picha na Juma Kengele - Ikulu

Read more...

Makamanda wa CCM

Mwanasiasa Mkongwe nchini , Kingunge Mgombale – Mwiru ambaye pia ni Naibu Kamanda Mkuu wa UVCCM na Mbunge wa Kuteuliwa ( wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM , Mhandisi Petro Kingu , ambaye alikuwa Kamanda wa UVCCM wa Morogoro mjini baada ya kukabidhi cheti cha utumishi kwa nafasi hiyo ambayo imechukuliwa na Pascal Kihanga ( hayupo pichani) wikiendi hii mjini Morogoro

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, (kulia) akimsikiliza Mwanasiasa Mkongwe nchini Kingunge Ngombale –Mwiru ambaye pia ni Naibu Kamanda Mkuu wa UVCCM na Mbunge wa kuteuliwa ( hayupo pichani) baada ya kusimikwa juzi kuwa Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ulanga ambapo Kamanda wa Wilaya ni Rajab Mkwesi ( hayupo pichani). Picha na John Nditi.

Read more...

Wednesday, November 4, 2009

Jose Mara azaliwa Novemba 2

Burudani ilitolewa na FM Academia na mtoto mwenyewe kwa kucheza sebene

zawadi za mtoto zilitolewa

Picha ya pamoja kwaajili ya kumbukumbu kwa waalikwa wote nayo ikapigwa, hii ilikuwa ndani ya ukumbi wa New Africa Hotel katikati ya jiji la Dar es Salaam Novemba 2 2009




Mwanamuziki wa bendi ya FM Academia Jose Mara na mkewe Monica a.k.a Mama Junior wakiwa wamejishika kiuno wakitafakari namna ya kukata keki ya hiyo ya kuadhimisha tarehe ya kuzaliwa Jose mMara.

Read more...

MBIO MAALUM ZA KUKIMBIZA BENDERA YA TAIFA ZAENDELEA.

Wanariaadha wa mkoa wa Arusha wakianza siku ya pili ya mbio maalumu za kukimbiza bendera ya Taifa kwa kupokezana baada ya kupokea bendera hiyo kutoka kwa wenzao wa Dar es Salaam, jana. Wanariadha hao watamaliza mbio hizo siku ya ijumaa kwa kuipandisha bendera ya taifa katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro.



Mwanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Pius Sulle akikimbia mbio maalumu za kukimbiza bendera ya taifa kwa kupokezana kutoka Chalinze hadi Segera baada ya kupokea bendera hiyo kutoka kwa wenzao wa Dar es Salaam, juzi. kabla ya kuhitimisha mbio hizo siku ya ijumaa kwa kuipandisha katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro. Mbio hizo za kampeni ya ‘Fikisha Tanzania katika hatua za juu’ zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro

Read more...

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwa amesimama mbele ya gari lake aina ya Suzuki Vitara Grand mara baada ya kukabidhiwa jana mchana kwenye duka la Vodashop mtaa wa Ohio.

Miriam Gerald akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC1 Evance Mhando mara baada ya kukabidhiwa gari lake jana mchana

Meneja mkuu wa Makampuni ya Shivacom Parthiban C. wa pili kutoka kulia na Meneja wa udhamini na mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za Gari aina ya Suzuki Grand Vitara Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald katika duka la kampuni hiyo lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam, Gari hilo jipya lina thamani ya shilingi milioni 53 na litamsaidia mrembo huyo katika kazi zake mbalimbali za kijamii Miriam Gerald alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar es salaam na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.


Read more...

JK na mratibu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Bwana Alberic Kacou muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

Read more...

Rais Kikwete aifariji Familia ya Marehemu Ng'itu Mbezi Beach

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Prisca Ng'itu mke wa Marehemu Sigfrid Ng'itu aliyekuwa Mbunge wa CCM Ruangwa wakati Rais Kikwete alipokwenda kuifariji familia ya Marehem huko mbezi beach,jijini Dar es Salaam jana jioni.(picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa Ruangwa CCM marehemu Sigfrid Ng'itu wakati Rais Kikwete alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mbezi beach Dar es Salaam kuifariji familia yake.Marehemu Ng'itu alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu Septemba 15 mwaka huu akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP