Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, February 26, 2010

Dr. Salim Ahmed Salim amlilia Balozi Mwakawago.

Dk.Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa AU, akizungumza na waandishi habari kufuatia kifo cha aliyekuwa balozi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Hayati Daudi Mwakawago (71).Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) sasa AU, Dk.Salim Ahmed Salim, akitia saini kitabu cha maombolezo, kufuatia kifo cha balozi wa zamani wa kudumu wa Umoja wa Mataifa, Alhaj Daudi Mwakawago nyumbani kwa marehemu Msasani Maduka Mawili jijini Dar es Salaam Alhamisi Februari 25, 2010.
Marehemu balozi Mwakawago amefariki mapema Alfajiri ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 71.
Kwa mujibu wa mdogo wa Marehemu Yasini Mwakawago, marehemu alifia hospitali ya Aga Khan alikokimbizwa kwa kusumbuliwa na Malaria lakini baadae aligundulika kuwa na matatizo ya Figo lililopelekea apumuwe kwa taabu.
Mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumamosi Februari 27. (Picha na Khalfan Said)

Read more...

Hussein Machozi aibuka na za mwizi 40
Mambo vipi? Napenda kukufahamisha kuwa Hussein Machozi ametoa tena singo yake nyingine inayoitwa ZA MWIZI 40, ambao umeachiwa rasmi hivi karibuni katika radio stations.
wimbo huu unapatikana katika album yake ya KWA AJILI YAKO.

Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na KWA AJILI YAKO na UTAIPENDA.
Kwa sasa tuko katika hatua za mwisho za kushot video ya wimbo huo, na tunategemea kuifanyia Dar es Salaam na Adam Juma wa Visual Lab wiki ya kwanza ya March, na video itatoka mara tu tukikabidhiwa na Adam.

SONG'S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
song arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS

Read more...

INFINITY ENT'S pres, SWAGGA NIGHT


INFINITY ENT'S pres, SWAGGA NIGHT. Sat 13th, MAR 2010 at SPICE LOUNGE, 3 Savoy Crecent, Theatre District, MILTON KEYNES. mk9 3pu,DJ DOUBLE T & Dj BILLY will make it happen.BONGO FLAVAS, R&B, RAGGA, OLD SKOOL. Dress Smart to impress. 10Pm till Late, Admission: £5 B4 12.VIP TICKETS AVAILABLE AT THE DOOR. Mishemishe sio mchezoo.

Read more...

Traffic light party in London march 5, 2010


Read more...

Kumekucha mjini


RSVP Club
(formerly much more club
@ Club Bilicanas complex)
NOW OPEN
Monday-Fridays From 5pm-5am!
ENTRANCE:FREE before 10pmwith 10,000 tsh coupon redeemable on drinks on weekdays!!
15,000 TSH ENTRY ON FRIDAYS AND SATURDAYS!LIVE JAZZ, BLUES and ROCK 'N' ROLL BAND

ON SUNDAYS-Entrance 5,000 with 5,000redeemable in drink coupons!!
Happy Hours from 5pm-10pm
ALL DRINKS 30% off!!Also available:
-SEXY DANCERS PERFORMANCES (Kandi Gurlz)&SPECIAL SONG REQUESTS from our DJ?sFor more info Visit:

Or Call

+255 764 853 396

Read more...

Kanumba kutikisa tena anga ya filamu na "THIS IS IT".


"Mashabiki wangu na wadau mbalimbali hii ni Filamu yangu mpya itakayotoka hivi karibuni, imetengenezwa chini ya kampuni yangu ya Kanumba The Great Film, hivyo kaeni mkao wa kula mengi nitawajurisha hivi karibuni, hii si ya kukosa. Akhsanteni sana",hayo si maneno ya JIACHIE bali ni kutoka kwa The Great mwenyewe ukitaka kufahamu kuhusu ujio wa filamu yake na mambo mengine yahusuyo tasnia ya filamu

Read more...

Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba ziarani nchini Misri.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba akiwa katika picha ya pamoja na Sheikhul-Azhar (GRAND SHEIKH OF AL-AZHAR) Pr. Dr. Muhammad Sayyed Tantawyi katika Ofisi zake za Masheikhatul-Azhar zilizopo Darassa


Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa S Simba akiwa pamoja na katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Kitaanzania wasomao Nchini Misri (T.S.U) na Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Al-azhar Cairo Nd,Ghalib Nassor Monero katikati Sheikhul-Azahar Baada ya Mazungumzo katika ofisi za Sheikhul-Azhar Daraasa Cairo.Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba katika Mazungumzo na Sheikhul-Azhar Pr. Dr. Muhammad Sayyed Tantawy Katika ofisi yake Masheikhatul-Azhar iliopo Daraasa.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba yupo nchini Misri Akihudhuria Mkutano Mkuu wa 22 (The 22nd General Conference: Under the Title The Objectives of Shariah(Islamic Law)And Issues of the Contemporary Age. Mkutano huo ambao ulianza siku ya 22-25 February 2010 sawa na 8-11 Rabi Al-awwal 1431H. Mkutano huo ulifanyika Katika Hoteli ya Conrad, Cairo, na ulijumuusha Masheikh na Viongozi wa Wakuu wa Nchi mbalimbali.

Read more...

Rais Kikwete aliporejea Dar

JK akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. William Lukuvi mara baada ya kuwasili jioni hii katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nje ya nchi kwenye ziara ya kikazi nchini Uturuki na Jordan. Kabla ya kutua Dar asubuhi alipitia Mwanza kufungua mkutano mkuu wa TAKUKURURais Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa katika ziara ya kikazi Mashariki ya Kati. Mwingine katika Picha ni Kingunge Ngombale Mwiru.

Read more...

Thursday, February 25, 2010

Dr. Kimei awaaga waliomaliza Kidato cha sita Tambaza


Wahitimu wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Tambaza wakimsikiliza mgeni rasmi Dk Charles Kimei wa CRDB

Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akihutubia wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika Sekondari ya Tambaza Dar es Salaam leo,Kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Terence Bunyogera na kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Jorum Lukwalo.Wahitimu wa kiume wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi Dk.Charles Kimei Mkurugenzi wa Benki ya CRDB.

Read more...

MWANAFUNZI BORA TANZANIA 2009 APOKEA ZAWADI ZAKE

Baba Mzazi wa Imaculata Prof. Restori Mosha akizungumza na waandishi wa habari kuelezea kipaji cha mtoto wake Imaculata Mosha wakati alipopokea zawadi yake kutokana na kufanya vyema katika mtihani wa kidato cha nne mwak 2009, kulia ni Immaculata Mosha


Mshindi wa jumla kwa masomo yote nchini na kuwa mshindi wa kwanza pia katika masomo ya sayansi kwa kupata "A" katika masomo yote ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2009 Immaculata Mosha, akipokea zawadi yake ya Kompyuta aliyopewa na Chuo cha Clever Tourisim & Hotel Management Hotel kutoka kwa Afisa Elimu Mkuu Wizara ya Elimu Bi. Doroth Mwaluko katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo , Imaculata pia alikabidhiwa shiligi 100.000 kutoka kwa chuo hicho.

Read more...

KITABU CHA MOSSY MAGERE

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akizindua kitabu cha Mwandishi Mossy Magere (kulia) kinachohusu uchaguzi mkuu 2010 kilichobeba jina "Mshike Mshike wa kisiasa 2010",


Nakala ya kitabu MSHIKE MSHIKE WA KISIASA 2010.uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam leo.


Mwandishi wa Habari Mossy Magere akiwa ameshikilia nakala ya kitabu alichotunga baada ya waziri Chikawe kukizindua Dar es Salaam leo.

Read more...

Rais Kikwete afungua mkutano wa mwaka wa TAKUKURUMkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo unaofanyika mjini Mwanza leo asubuhi.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wakipigamakofi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo mjini Mwanza leo.Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea na kushoto ni Waziriri wan chi Ofisi ya rais Utawala Bora, Sofia Simba.


Read more...

Miriam Gerald apandishwa tena kizimbani

Miss Vodacom Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’, leo wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 na watuhumiwa hao wanaendelea kuwa nje kwa dhamana.

Read more...

Anna Makinda apata mpinzani Jimboni kwake.

Mwanasheria wa kujitegemea Bw. Deiniol J. Msemwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Njombe Kusini Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi Oktoba mwaka huu endapo atapitishwa na chama chake.

Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo na yeye mwenyewe akapata wasaa wa kuongea na wanahabari na kuwatangazia nia yake hiyo.
Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na Mwanasiasa Mkongwe toka enzi za Uhuru mwanamama shupavu Anna Makinda ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dainiol Msemwa amesema ametuhubutu kutangaza nia yake hiyo kwa kuwa uwezo anao na katiba ya chama cha mapinduzi inamruhusu kufanya hivyo, lakini pia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki hiyo ya kuchagua ama kuchagulia kama raia wa Tanzania.

Katika Picha wengine wanaofuatia ni Enock Ngombale Mwiru Mshauri wa siasa wa mgombea na mwisho ni Jerome Joseph Msemwa wakili

Read more...

Hii ndiyo adha ya kuota manyoya, usiombe yakukute.

Huyu nae uso wote unamnyoya. Iwapo kama tendo lililovuma siku kadhaa na kuwa gumzo jijini Dar es Salaam juu ya omba omba aliyemuotesha mtu manyoya ni lakweli basi mfano wake ndo huu je inakutokea utafanya nini?

Mmoja wa jamaa ambaye alitoa msaada na kugeuzwa anamanyoya mwili mzima akiwa hana la kufanya

Read more...

Thursday, February 25, 2010MABALOZI WATEULE WAMUAGA RAIS KARUME


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akizungumza na mabalozi wateule wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za nje,(katikati)Prof Abillah Omar,Balozi nchini Saudi Arabia na(kushoto)Dr James Mwasi nchini Bujumbura-Burundi,waliokuja kumuaga Rais jana,Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar

Read more...

Executive Solutions Wamuombea Alan TurnerWafanyakazi wa Executive Solutions waliohudhuria misa hiyo maalum ya Turner.

Watumishi wa ES ambapo Alan alikuwa akifanya nao kazi wakifuatilia misa hiyo kwa makiniVijana wa The Voice kutoka magomeni Dar es Salaam wakiimba katika Misa hiyo takatifu
Mkurugenzi Mtendaji wa Executive Solutions Aggrey Mareale akiwa katikati ya waliohudhuria misa hiyo maalum.


Wapowapo ya watu walioguswa sana na msiba huo ambao walishindwa kujizuia kwa kilio.
Waombolezaji wengine wakifuatilia misa hiyo Dar es salaam


Read more...

Wastaafu wa iliyokuwa EAC walonga juu ya mafao yao.


Katibu wa Kamati ya Madai ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Kitengo cha Bandari Said Mikohi (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya uongozi wa Bandari kukwamisha kulipwa kwa mafao yao mpaka sasa kama walivyofanyiwa wenzao. Wengine ni Katibu Msaidizi wa Kamati hiyo Kassim Omary (kushoto) na kulia ni mmoja wa wajumbe Emmanuel Mpoto .Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Read more...

Nakaaya na Hussein Machozi kuvamia Babati


Read more...

Mambo ya Kichina hayo!!Read more...

WARSHA YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KUELEKEA UCHAGUZI

Washiriki na waandishi wa habari walioshiriki mjadala wa majukumu ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Majadala huo uliandaliwa na Sauti ya Ujerumani.


Mwenyekiti wa MISA –TAN Ayub Rioba akisisitiza jambo jana mjini Dar es salaam kwenye mjadala wa majukumu ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Wengine katikakti ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dunstan Tido Mhando na Mkuu wa Sauti ya Ujerumani kanda Afrika na Mahariki ya Kati Ute Schaeffer (kushoto) .Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dunstan Tido Mhando (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Sauti ya Ujerumani kanda Afrika na Mashariki ya Kati Ute Schaeffer (kulia) wakati wa majadiliano juu ya wajibu wa vyombo vya habari kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Majadiliano hayo yameandaliwa na Sauiti ya Ujerumani

Read more...

Picha zaidi za ziara ya JK Jordan


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jordan Samir Rifai.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Seif Ali Iddi na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jordan, Ameir Al Hadidi wakitia saini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Uchumi na Sayansi kati ya Tanzania na Jordan huko Amman, mji mkuu wa Jordan wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humoNaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ali Iddi na Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Jordan, Mohammad Ali wakibadilishana mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Jordan.

Read more...

BALOZI DAUDI MWAKAWAGO AFARIKI DUNIA!

HABARI ZILIZOPATIKANA MUDA SI MREFU ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.

MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.

BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU.

ALIWAHI PIA KUCHAGULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, KOFFI ANNAN KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.

Read more...

Wednesday, February 24, 2010

Simba 1-1 African Lyon

Matokeo ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika ya Simba na African Lyon umemalizika kwa sare ya 1-1, goli la A. Lyon limefungwa dakika ya 5 na Sentongo, wakati la Simba limefungwa dakika ya 81 na Musa Hasan Mgosi.

Read more...

ZATI HONOURS ZANZIBAR HISTORIAN

MEMBERS OF ZATI, COMMISSION FOR TOURISM AND REPRESENTATIVES OF VODACOM AND KCB ON A GROUP PICTURE..CELEBRATING THE SUCCESS OF THE EVENINGPROFFESSOR ABDUL SHERIFF FAMOUS ZANZIBAR HISTORIAN RECEIVING THE ZATI SPECIAL AWARD FROM THE BRITISH HIGH COMMISSIONER4 TO TANZANIA BALOZI DIANE CORNER FOR HIS OUTSTANDING WORK IN PRESERVING HISTORY AND PROMOTING THE RICH SWAHILI CULTURE WHICH HAD A DIRECT POSITIVE IMAGE ON THE CULTURAL TOURISM OF ZANZIBAR

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP