Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, March 31, 2010

Rais Kikwete na Balozi wa China waweka jiwe la msingi ujenzi wa Taasisi ya Moyo Muhimbili.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wanne kushoto) na Balozi wa China nchini Bwana Liu Xinsheng(watatu kushoto) wakiweka udongo katika jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Taasisi ya tiba ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH leo asubuhi.Wengine katika picha ni Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa(watano kushoto) na kuli ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Adolar Mapunda, wapili kushoto ni kiongozi wa ujumbe wa Jamhuri ya watu wa China Bwana Sun Liang (picha na Freddy Maro)

Read more...

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VITABU

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiangalia vitabu mbalimbali vya sayansi vilivyotolewa kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia elimu ya Sayansi nchini.Kulia ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.

Wakuu wa vyuo na shule mbalimbali za Sayansi nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya sayansi za maabara kutoka kwa watu wa marekani jana jijini Dar es salaam.Vitabu 1920 vyenye thamani ya shilingi milioni 91 vimetolewa na kukabishiwa kwa wakuu wa vyuo hivyo.
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa chuo cha maabara Litembo kilichoko wilayani Mbinga mkoani Ruvuma sista Angelina Marry Kihwili vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi na Afya nchini.Katikati ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.


Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa shule za maabara za Sayansi, Muhimbili Mr. Colman Msuya vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi nchini.

Read more...

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali akabidhi Ripoti za ukaguzi wa Matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake Kwa Rais Kikwete Ikulu


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti za ukaguzi wa matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Msaidizi wa mkaguzi mkuu Bwana Atanas Tarimo(Picha na Freddy Maro)

Read more...

HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA DIAMOND APRILI 9-10.


Mratibu wa Mradi wa Harusi Trade Fair Sati Gadhvi akizungumza leo jijini Dar es salaam kuelezea maonyesho ya bidhaa za Harusi yanayotarajiwa kufanyika Aprili 9-10/ 2010 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo washiriki zaidi ya 40 wanaojishughulisha na mambo ya kuandaa harusi wanatarajiwa kushiriki, amesema kiingilio katika maonyesho hayo kitakuwa shilingi 2000 kwa mtu mmoja aliyeko kulia katika picha ni meneja masoko na Mauzo wa Harusi Trade Fair Khamis Omar.

Read more...

Tigo sasa yaja na Sumni kupiga simu.

Kulia ni Meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja matangazo na promosheni Redemtus Masaja akizindua Rasmi viwango nafuu vipya vya mawasiliano kwa wateja wa Tigo kuanzia kesho. Ukiwa Tigo Thumni inathamani kama zamani!Ongea utakavyo, sasa ni nusu shilingi kila sekunde baada ya dakika ya kwanza,saa20 kwa siku, kasoro saa12jioni-4usiku.Tigo

Tigo introduce another affordable tariff Tigo Thumni Dar es salaam April 2010 Tanzania telecommunication company Tigo announces the launches of another most affordable tariff for Tigo pre paid subscribers which will be available for every Tigo subscribers from now onwards every single day. Mbando akiwa na Masanja wakishikilia mabango yao ya Nusu shilingi.
Speaking in the press conference Tigo PR Executive Jackson Mmbando said “This new tariffs wants to encourage TIGO subscribers to make calls for lower prices at Tshs 1/2 after the 1st minute, 20 hours a day except between 6pm to 10 pm at night

Our new tariff services will be known as Tigo Thumni /Ongea kama Zamani! Which means With Tigo, Thumni it’s like in the old days when currency had much value. Talk as much as you want for only 1/2 Tsh per second after the 1st minute, 20 hours a day except from 6pm to 10 pm.! Jackson insists that!

for this we want to grant our customers with enough freedom to access today’s world in a simple manner by giving them thumni as a special tariff they can afford and manage to strive against the social life.

We are sure that this will give enough opportunity to every one using Tigo to interact and share their professional experiences in a truly different way.”

Now lets every one talk and enjoy Kama Zamani with only ½ Tsh per second after the first 60 seconds of each call to other Tigo subscribers

Just to remind you with this tariff there is no registration requirement of any kind. The user just needs to have a Tigo pre-paid sim card, and good enough thumni tarrifs will not affect home zone tariffs of ROBO shillings per second after the first minutes while in Zanzibar.

We real encourage our subscribers to continue enjoy our best price ever now!

Tigo with our introduction of Longer longa, XTREME services, Usipimes , Xtreme SMS and today Tigo Thumni I believe it explain Tigo Brand as most affordable, thus means consider our subscribers situation and we own the spirit of simplicity, uncomplicated, open, assessable and always there when needed.

Read more...

Wawili wapiga hodi kwa Ndesamburo


Bwana Batista Mwendivita ambaye ni Mjumbe wa halmashari kuu ya Wilaya ya Moshi Mjini CCM na Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu mkoani Kilimanjaro kushoto na MwanaCCM mwingine Gibson Nderangusho wakitangaza mbele ya wanahabari kwa pamoja nia yao ya kugombea ubunge katika jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, wote kwa pamoja wamesema wana nia hiyo na katiba zote mbili ya Chama Cha Mapinduzi na ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania zinawaruhusu kufanya hivyo na ni haki yao ya kimsingi , marafiki hao wawili walitangaza nia yao leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.

Read more...

TANZANIA KUPATA BILIONI 322 KUTOKA BANKI YA AFRIKA (ADB)

Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana mjini Dares salaam wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.


Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana hati jana jijini Dar es salaam ya makubaliano ya msaada wa kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt Sipho Moyo.

Read more...

Promosheni ya Shangwe za Tigo Kombe la Dunia


Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando akikabidhi zawadi ya LCD TV kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Shangwe za Tigo Kombe la Dunia, Mark Elias Makundi jijini Dar es Salaam . Katikati ni Ofisa Viwango wa Tigo, David Zakaria.

Read more...

Tuesday, March 30, 2010

Zain yaanza Maadhimisho ya Upandaji Miti kitaifa


Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi (kushoto) akipanda mti kuazimisha siku ya utunzaji wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeendeshwa na Shirika la linalojishugulisha na shuguli za utunzaji wa mazingira na mimea la WWF kwa kushirikiana na Zain Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta.

Read more...

Maige aanza upandaji miti Shinyanga


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige mwenye suti nyeusi, akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Town iliyoko mjini Shinyanga,wakati wa sherehe za kuelekea Siku ya Taifa ya kupanda Miti nchini ambayo kitaifa inafanyika Aprili Mosi mkoani Shinyanga, aliyeshika. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Felician Kilahama na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Fabian Stanslaus.

Read more...

Wanafunzi wa dunia wautembelea ubalozi wa Tanzania


wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ambao waliichagua Tanzania kama nchi wanayoiwakilisha katika Baraza hilo. Na ili waifanye kazi hiyo vema, wanafunzi hao waliutembelea Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ili kujifunza na kupata uelewa zaidi kuhusu historia ya Tanzania, matatizo, mafanikio , changamoto, na namna gani Tanzania inavyoutumia Umoja Mataifa kusukuma ajenda zake mbalimbali. Aliyevaa suti nyekundu ni Afisa Ubalozi Bi Joyce Kafanabo ambaye alitoa maelezo na kujibu maswali mbalimbali ya wanafunzi hao, kwa niaba ya Balozi.

Read more...

Jina la Hotel lamchanganya RC


KATIKA hali ya ambayo haikuwa ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brigedia
Mstaafu Dk. Yohane Balele mwishoni mwa wiki aligoma kwa muda kuifungua Hoteli ya kisasa ya Piracy kutokana na jina lake kumaanisha kitu ambacho kinakera.
Jina hilo kwa kiswahili maana yake uharamia. Utata huo ulichukua muda wa zaidi ya saa mbili na kumfanya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Meja Mstaafu Bahati Matala kupata kazi kidogo kuwasiliana na mwenye hoteli ili jina libadilishwe.

Read more...

Mpendanzoe ahamia CCJ

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) leo.


Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akitangaza kwa waandishi wa habari jana jijini Dar leo ju ya nia yake ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) . Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise na kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCJ Dickson Nghilily. Picha na Tinganya Vicent - MAELEZO

Read more...

Mtoto wa Mkulima ndani ya Vietnam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride la heshima

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea maua kutoka kwa mtoto wa Vietnam wakati alipopokelewa rasmi kwenye viwanja vya Ikulu ya Hanoi , Machi 29, 2010 kuanza ziara yake ya kikazi nchini Vietnam. Kulia ni mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung.

Read more...

Mama Salma Kikwete akiwa ziarani mkoani Mara

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha Nyamuswa, wilayani Bunda mkoani Mara, wakati akielekea mjini Bunda kukagua shughuli mbalimbali za akinamama wajasiriamali wilayani humo.


Mkurugenzi Mkuu wa Singita Grumeti Reserves Bwana Graham Ledger,kulia, akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kazi za taasisi ya WAMA. Makabidhiano hayo yalifanyika katika hoteli ya Grumeti iliyoko katika hifadhi ya Serengeti .

Read more...

TAARIFA KWA UMMA

Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili. Muswada huo ulipitishwa tarehe 11 Machi 2010 katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au “kinyemela”. Kifungu kidogo cha 7(3) kinaweka masharti yanayohitaji uthibitisho wa wajumbe wanaounda Timu za Kampeni za Wagombea wa Kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani. Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

Kwa kuzingatia madai ya Mheshimiwa Dk. Slaa, Vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa maelezo mbalimbali kuhusu suala hili. Katika mazingira haya, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na Wadau na Wabunge, Bunge liliagiza Muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.

Marekebisho hayo ni:

(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.

(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni”. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.

Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya “Timu ya Kampeni” ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika “Timu ya Kampeni”. Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.

Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

Kwa kuzingatia maelezo haya kuhusu hoja za Wabunge ninaridhika kuwa kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Uchaguzi kimezingatia matakwa na maagizo ya Bunge sawa sawa. Kifungu hicho hakikuingizwa kwenye Sheria “kinyemela” au kwa hila. Aidha, mtiririko wa mamlaka za kuthibitisha Timu ya kampeni una mantiki sahihi yenye lengo zuri la kufanikisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.


Imetolewa na
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
29 Machi, 2010

Read more...

Monday, March 29, 2010

Wachina Ikulu

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mara baada ya kuwasili Ikulu leo jijini Dar es salaam kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51.
Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.

Read more...

JK apokea misaada toka China

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mahojiano na mwakilishi wa shirika la habari la Xinhua nchini Tanzania Bi. Guo Chunju mara baada ya nchi ya China kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini leo jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Kikwete akikagua pikipiki ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na nchi ya China kupitia kwa Balozi wa nchi hiyo Liu Xinsheng (mwenye suti kushoto) kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Makabidhiano hayo ya vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51 yamefanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais Jakaya Kikwete akiagalia msaada wa baiskeli zilizotolewa na nchi ya China ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 vilivyotolewa na nchi hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Balozi wa China Liu Xinsheng aliyekabidhi msaada huo.

Read more...

Serikali yaonya juu ya biashara ya madini feki nchini


Kamishna wa Madini Dalaly Kafumu akitoa tamko la tahadhari leo jijini Dar kwa waandishi wa habari juu ya kuibuka kwa utapeli wa biashara madini ambao umeanza kushamiri hapa nchini na hivyo kuanza kutishia uwekezaji katika Sekta hiyo. Alisema kuwa baadhi ya matapeli wanashirikiana raia wa nchi za kigeni kuwauzia watu madini bandia. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Read more...

Vodacom yamwaga kompyuta mashuleni Singida

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack akiangalia jinsi kompyuta inavyofanya kazi baada ya kukabidhiwa rasmi kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za sekondari ya Shului na Isuna zote za Iramba anaeangalia kushoto Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mshamu Manyinja na Alice Mlumba.
Afisa wa Vodacom Foundation Grace Lyoni akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14

Read more...

Simba na mikakati mbadala

Mwenyekiti wa Mabingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania 2010/2011 Simba Sports Club Mzee Hassan Dalali akifungua tawi la Simba linalojulikana kama "Simba Ng'ata" huko Kurasini Mivinjeni Wilayani Temeke jijini Dar es salaam jana jioni huku wanachama wa tawi hilo wakiangalia, wanachama na mashabiki wa Simba wameliita tawi hilo la simba jina la Simba Ng'ata kutokana na timu ya Simba kufanya mambo makubwa katika msimu huu wa ligi hasa baada ya kutofungwa mchezo hata mmoja mpaka wanatangaza ubingwa.

Wageni mbalimbali wakiwa wamekaa wakati wa uzinduzi wa tawi la SIMBA NG'ATA. Tawi hilo lilifunguliwa rasmi naMwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali aliyefuatana na Mweka hazina msaidizi wa SSC bwana Chano. , aliyekaa katikati ya Chano na Dalali ni Mwenyekiti wa muda wa tawi hilo anayejulikana kwa jina la Moloto, na kushoto kwa Dalali ni Hamisi Jabu baba yake mzazi na mchezaji wa SSC Juma Jabu.

Read more...

Mwakilishi wa Unicef aaga Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wakazi Nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK Amani Abeid Karume,akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Heimo Laakkomen,aliyekuja kumuaga Rais,Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya kumaliza muda wake wakazi Nchini.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.Zanzibar

Read more...

Friday, March 26, 2010

Waziri Membe afungua Diaspora II London


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mwanaidi Majaar wakipata maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba za kuuza kutoka Miranda Lutege,Meneja uhusiano wa Benki ya Biahara ya Afrika( CBA)muda mfupi kabla Waziri Membe hajafungua mkutano wa pili wa Diaspora hapa London leo.

Read more...

Usiku wa Precision Air wang'ara

Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air, Bw. Alfonse Kioko akitoa risala yake mbale ya wafanyakazi na wageni waalikwa.


Mwakilishi wa kampuni ya Highlight Travel- BCD Travel ya nchini Kenya, akipokea cheti kutoka kwa Bw. Shafi Kaka ambaye ni Rubani Mkandawire wa Precision Air. Pembeni ni mwakilishi wa kampuni ya Carlson Wagonlit Travel ya nchini Kenya, Bi. Julie Scott pamoja na Station Meneja wa Precision Air Kenya na Uganda Bi. Sarah Wachira.


Meneja Mkuu wa Precision Air Ground Handling Company Bw. Elias Moshi akimpa tuzo mwakilishi was Winglink Travel Ltd ambao walikuwa washindi wa tatu-Dar.
Picha zaidi tembelea http://michuzijr.blogspot.com/

Read more...

Pinda ndani ya Japan

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Japan, Mhe. Lumumba Lumbumba baada ya mkutano wake na mabalozi wan chi za Afrika mchini Japan uliofanyika kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo, Machi 26, 2010. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga picha na Gavana na Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu ya Japan, Bw. Shosaku Yasui kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Japan Machi 26, 2010.

Read more...

Mama Salma Kikwete alipotembelea Monduli

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi zahanati ya kijiji cha Oltukai kilichoko katika wilaya ya Monduli Machi 24, 2010.



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Monduli Mhe.Edward Lowasa mara baada ya Mama Salma kuwasiri mjini Monduli kwa ziara ya siku moja wilayani humo Machi 24, 2010.

Read more...

MULTCHOICE YALETA DECODER ZENYE UBORA WA HALI YA JUU


Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Salamu akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam leo wakati kampuni hiyo ilipozindua uuzaji wa Vinga'amuzi vipya vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo ni M-Net HD, SuperSport HD, Discovery HD Showcase and iConcerts HD, Furaha amesema ving'amuzi hivyo vyenye uwezo wa kurekodi matukio au vipindi vinapatikana katika maduka mbalimbali ya mawakala wa kampuni hiyo kote nchini, wengine katika picha ni Barbara Kambogi katikati Meneja uhusiano na mwisho nia Ronald Shelukindo Meneja Huduma.

Read more...

NMB yaikumbuka Namtumbo

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Shy-Rose Bhanji akipeana mkono na Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Namtumbo Paulo Gailanga baada ya kukabidhi msaada wa madawati wa madarasa mawili katika shule ya Msingi Nambehe iliyopo kijiji cha Msindo. NMB pia ilitoa misaada mbalimbali wilayani Namtumbo yenye thamani ya shillingi Millioni 10.


Maafisa wa benki ya NMB wakimpa pole mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Namtumbo, wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma. Maafisa wa NMB walikabidhi magodoro na drandarua kwenye kituo hicho ikiwa ni msaada wa benki hiyo juzi. NMB pia ilitoa misaada mbalimbali kwa ujenzi wa mashule wilayani humo yote ikiwa na thamani ya shillingi millioni 10m/-. Makabidhiano hayo yalifanyikia wilayani namtumbo juzi.

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP