Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, April 16, 2010

WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO YAWAPIGA MSASA WAFANYAKAZI WAPYA


Baadhi ya washiriki wa mafunzo elekezi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda(hayupo pichani) wakati wa ufunguaji mafunzo elekezi leo mjini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda akifungua mafunzo elekezi ya waajiriwa wapya wa Wizara hiyo leo mjini Dar es salaam. Mafunzo hayo ni sehemu ya utaratibu wa Serikali wa kuwaelimisha watumishi wake wapya kwa ajili ya kuongeza ufanisi mahali pa kazi.Picha na tiganya vincent-maelezo

Read more...

Bungeni Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Aprili 19, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Spika wa Bunge Samuel Sitta (kulia) wakati alipoongoza kikao cha wabunge hao kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 18, 2010. Kushoto ni Kaimu Katibu wa wabunge wa CCM na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama. .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Ziara ya Wanasheria wa Tume Mbinga, Songea


Ofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) Flaviana Charles akionesha msisitizo wakati akiwasilisha mada ya Sheria ya Mirathi mbele ya Makatibu Tarafa na Wazee wa Mbinga mkoani Ruvuma.

Baadhi ya Makatibu Tarafa na Wazee wa Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakifuatialia mada zilizokuwa zikitolewa na timu ya wanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.


Baadhi ya Watumishi wa Serikali kutoka idara mbalimbali za Serikali Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakifuatialia mada zilizokuwa zikitolewa na timu ya wanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.


Ofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) Flora Tenga aliyesimama akizungumza mbele ya Watumishi wa Serikali kutoka idara mbalimbali wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati timu ya wanasheria wa Tume ilipofanya ziara ya kutoa elimu ya sheria kwa umma wilayani humo, wengine ni Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Tume Caritas Mushi katikati na Ofisa Sheria Flaviana Charles.

Read more...

Wanachama wapya wa UWT kutoka vyuo vya Dodoma wapewa kadi.

Naibu Kaibu Mkuu wa UWT Taifa Asha Bakari akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bi Situmai Makae wakati akiwaapisha wanachama wapya Wa UWT zaidi ya 800 jana mkoani Dodoma kutoka Vyuo vinne , CBE, Mipango, St Johns na UDOM.Mpiga zeze maarufu nchini Dr. Masalia akipiga zeze katika sherehe hiyo juzi
Wanachama wapya wa UWT kutoka vyuo mbalimbali Mkoani Dodoma wakiapa kuwa watiifu kwa chama chao.Picha zote na Mwanakombo Jumaa.

Read more...

Mkulo na Mkukuta yake.


Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(katikati) akibadilishana mawazo jana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma na Mbunge wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Mkoani Mwanza, Dk. Raphael Masunga Chegeni(kushoto) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Lucy Owenya ( kulia) mara baada ya kumalizika kwa kukusanya maoni ya wabunge juu mchakato wa majadiliano ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania(MKUKUTA) ambazo zoezi hilo limeanza jana jioni na linaendelea nchini kote.


Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(kulia) akibadilishana mawazo jana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (katikati) pamoja na Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Clifford Tandari( kushoto) mara baada ya uzinduzi wa mchakato wa majadiliano ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania(MKUKUTA) ambazo zoezi hilo limeanza jana jioni na linaendelea nchini kote.

Read more...

President Jakaya Kikwete meets the UN Secreary General Ban Ki Moon at the UN Headquarters in New York

The UN Secretary General Ban-ki Moon welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete at his UN Headquarters office in New York today for official talksPresident Jakaya Mrisho Kikwete and the UN Secretary General Ban ki Moon withe their teams get down to business at the UN Heaquarters in New York today.Photos by Freddy Maro

Read more...

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA KUSINI NA MALAWI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere , Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 16, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya (katikati)na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere , Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Peter Msolwa wakitoka kwene ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, leo Aprili 16, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Serengeti yaibuka na promosheni mpya kwa wateja wake

Meneja Matukio na promosheni wa kampuni ya bia ya Serengeti(SBL) Bwana Bahati Singh, akionyesha kipeperesushi kinachoonesha zawadi mbalimbali kwa waandishi wa habari leo Dar es salaam. Kesho zawadi hizi zitatolewa kwenye viwanja vya Kinondoni Boafra and Mwembe yanga Temeke. Kulia ni na Afisa Habari Mwandamizi wa SBL Bwana Imani LwingaMeneja Matukio na promosheni wa kampuni ya bia ya Serengeti(SBL) Bwana Bahati Singh, akiongea na waandishi wa habari leo Dar es salaam akielezea kuhusu promosheni ya vuna pesa na Mizawadi Kede-kede itakayotolewa na SBL ambayo itaanza kesho katika viwanja mbalimbali jijini. Kesho zawadi hizi zitatolewa kwenye viwanja vya Kinondoni Biafra and Mwembe yanga Temeke. Kulia ni na Afisa Habari Mwandamizi wa SBL Bwana Imani Lwinga.

Read more...

MISS UNIVERSE WAINGIA KAMBINI KUJIWINDA NA KINYANG'ANYIRO APRILI 23.

Miss Universe wa mwaka 2009 Illuminata James, akimkagua mmoja wa waremmbo, Warembo wanaoshiriki mashindano ya Miss Universe 2010 , Nezia Anthony wakati wa kuanza rasmi kwa kambi yao katika Hoteli ya Giraffe Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni yaCompas Communicatins Maria Sarungi ambaye pia ndiye mwandaaji wa Miss Universe Tanzania akiongea mbele ya wageni mbalimbali na warembo wakati warembo wapatao 20 walipoingia rasmi kambini kwa muda wa wiki moja katika hoteli ya Girrafe Ocean View Mbezi kujiandaa na shindano hilo linalotarajiwa kufanyika aprili 23 kwenye ukumbi wa Mlimani City baadae mwaka huu jijini Dar es salaam.
(picha na Mohamed Mambo)


Warembo wanaoshiriki mashindano ya Miss Universe wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuanza rasmi kwa kambi yao katika Hoteli ya Giraffe Dar es salaam leo.

Read more...

Thursday, April 15, 2010

AICC YASAINI MKATABA WA KUUNDA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (kulia) akibadilishana na Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mkataba huo ulisainiwa katika ofisi za AICC mjini Arusha. Kushoto ni Katibu wa TUICO tawi la AICC, Rashid H. Rashid.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (katikati) akibadilishana na Mwenyekiti wa TUICO tawi la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Ezekiel Kiologwe mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la AICC. Mkataba huo ulisainiwa wiki hii katika ofisi za AICC, mjini Arusha. Kushoto ni Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (katikati) akitia saini mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la AICC. Mkataba huo ulisainiwa wiki hii katika ofisi za AICC. Kushoto ni Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo na kulia ni Mwenyekiti wa TUICO tawi la AICC, Ezekiel Kiologwe na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa AICC, Savo Mung’ong’o. (Picha kwa hisani ya AICC) .

Read more...

Waziri Mkulo azindua mchakato wa maoni ya MKUKUTA awamu ya 2 mjini Dodoma


Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kuanza kwa mchakato wa kujadili kuhusu Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) awamu ya pili. Mchakato wa kutoa maoni umeanza jana mjini Dodoma ambapo wabunge walipata fursa ya kutoa maoni yao jinsi ya kuboresha awamu ya pili ya MKUKUTA. wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wizara ya fedha na Uchumi John Haule (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Kuondoa Umaskini na Uwezeshaji Anna Mwasha(kulia)

Read more...

Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge yatembelea VOA


Matembezi ya kamati ya mambo ya nje ya bunge ikiwa katika ofisi za VOA, Kutoka kushoto Khadija Riyami,Wilson Masilingi,Juma Nkamia 'Kocha Mtangazaji' , Afisa Ubalozi Suleiman Saleh,Mh.Juma Killimba,Mkamiti Kibayasi na Mariam Kurtz.

Read more...

Bungeni Dodoma

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 15, 2010


Baadhi ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikili Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma leo.


Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo akifungua mkutano wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wanawake kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma

Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo (waliokaa watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa baada ya kufungua mkutano wao wa mwaka kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma,

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya wabunge, bungeni mjini Dodoma, Aprili 15,2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Ta, Dr. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akifurahia jambo katika Mazungumzo na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama kwenye viwanja vya Bunge Aprili 15, 2010.
Read more...

President Kikwete attends a special UN Meeting on improving maternal Health, meets UNFPA Executiv Director in New York


The UN Secretary General Ban Ki Moon welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete for joint Press Conference shorlt after the conclusion of a special UN closed door meeting on improving Maternal Health Held at the UN Headqarters in New York this morning.

President Jakaya Mrisho Kikwete welcomes the Executive Director for the United Nations Population Fund(UNFPA) Dr.Thoraya Obaid in New York for official talks this morning the President later participated in a specil meeting on Improving Maternal Health convened by the UN Secretary General Ban -ki Moon at the UN Headquarters.


President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the UNFPA Executive Director Dr.Thoraya Obaid in New York this morning. Photos by Freddy Maro of Ikulu

Read more...

ZAWADI ZA ZANTEL

MENEJA MAUZO WA ZANTEL MKOA WA MWANZA Bw.KENNEDY NDONONDO AKIMKABIDHI MSHIDI WA PROMOSHENI YA CHOMOKA NA PIKPIKI Bw.FRED KISSAKA TOKA MWANZA ALIYEJISHINDIA PIPIKI. ZANTEL INAENDESHA PROMOSHENI KABAMBE KWA WAKAZI WA MWANZA NA MARA TU, ILI KUSHIRIKI TUMA NENO PIKIPIKI KWENDA 15583 NA UJISHINDIE ZAWADI KIBAO.


MENEJA MAUZO WA ZANTEL MKOA WA ARUSHA Bw.HAIDAR CHAMSHAMA AKIMKABIDHI MSHIDI WA PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MKWANJA Bw. ELIGAH LAIZER TOKA ARUSHA ALIYEJISHINDIA FEDHA TASLIMU SHILINGI MILIONI MOJA. ZANTEL INAENDESHA PROMOSHENI KABAMBE KWA WAKAZI WA KILIMANJARO NA ARUSHA TU ILI KUSHIRIKI TUMA NENO MKWANJA KWENDA 15583 NA UJISHINDIE ZAWADI KIBAO.

Read more...

Miaka 10 ya Hospitali ya taifa Muhimbili

Kinamama wakipata maelezo ya huduma za Muhimbili


Wananchi wakipata vipeperushi kwenye maonyesho


wafanyakazi wa Muhimbili katika sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo


Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Deo Mtasiwa akifungua rasmi Maonesho ya kutimiza mkiaka 10 ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.William Lukuvi (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonyesho haya kesho tarehe 16 Aprili 2010.Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Leonard Lema akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua maonyesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kuadhimisha miaka 10 toka ilipoanzishwa Aprili 2000.


Read more...

BAYPORT YALIPATIA JESHI LA POLISI VIFAA VYA MICHEZO.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport Financial Services Bw. Ngula Cheyo Kushoto akimkabidhi kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Dashhood Mndeme vifaa mbalimbali vya michezo vitakavyotumiwa na Jeshi la Polisi katika michezo yao itakayofanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi)ambayo huadhimishwa Tarehe 1 Mei kila mwaka duniani kote, hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani leo asubuhi.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza maelezo ya ofisa wa kampuni ya Bayport Financial Services

Read more...

Wednesday, April 14, 2010

Bungeni Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Usalama Barabarani upande wa watu wenye ulemavu , Jutoram Kabatelle kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Aprili 14, 2010.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa , Kingunge Ngombale -Mwiru kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma,


Waziri mkuu, Imzengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa Viti Maalum, Gaudentia Kabaka (katikati) na Mbunge wa Busanda , Lolesia Bukwimba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Aprili 14, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

TBL YAENDESHA SEMINA YA SIKU MOJA KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO LEO

Wanahabari za michezo wa wakifuatilia kwa makini semina ya siku moja ya namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam,inayoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mjimwema uliopo katika hoteli ya South Beach resort,Kigamboni


Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari za michezo waliofika katika semina ya siku moja ya namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam,inayoendelea kufanyika katika hotel ya South Beach resort,Kigamboni leo

Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja akizungumza na waandishi wa habari za michezo waliofika katika semina ya siku moja ya namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam,inayoendelea kufanyika katika hotel ya South Beach resort,Kigamboni leo

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP