
afande wa FFU akiwa kashikilia bomu la kurusha kwa mkono ambalo halikuwahi kulipuka na kukutwa ndani ya kibegi nje ya jengo la benki ya NMB tawi la Temeke

damu ya wafanyakazi wa katika kaunta ya benki ya NMB tawi la Temeke ambapo majambazi yapatayo saba hivi yalivamia kwa mabomu ya mkono ambapo baada ya kurusha moja nje na kuua mlinzi wa kampuni binafsi aliyekuwa getini, yakarusha mabomu mawili ndani yaliyojeruhi watu 13, ikiwa ni pamoja na askari polisi wawili na kukomba takriban shilingi milioni 150 kabla ya kutoroka. Hii ni mara ya kwanza kutokea uporaji wa aina hii na umekuja siku moja tu baada ya Kamanda wa kanda maalumu ya Dar Afande Selemani Kova kutoa tahadhari kwamba taarifa za kiintelegensia zao zinaonesha kuna kundi la majambazi yenye silaha kali linataka kufanya uhalifu jijini

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Afande Manumba akionge na wanahabari sehemu ya tukio. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Lawrence Masha, Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema na Mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi pia walikuja eneo la tukio baadaye na kutembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Temeke iliyo jirani na Benki hiyo.
No comments:
Post a Comment