Monday, August 31, 2009
JK NDANI YA LIBYA
Shein ndani ya Geneva

Rais Jakaya Kikwete akiagana na mmoja wa watawa wa Kanisa Katoliki mara baada ya kumalizika kwa futari ambayo aliwaandalia viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, Ikulu, Dar es Salaam juzi.
Jangili anaswa na nyara
BODI YA UKAGUZI WA FILAMU YAZINDULIWA, UONESHAJI HOLELA WA SINEMA SASA MARUFUKU
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Pof.Hermas Mwansoko,akifuatiwa na Beneventus Lopa Afisa Mipango na Utawala wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Clement Mshana
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu mara baada ya uzinduzi.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rose Sayore. Picha na habari na Aron Msigwa- MAELEZO.
Ajira ya CloudsTV, watu kibao
mtangazaji wa Clouds 88.4 Zamaradi akiwa hoi bin taaban kwa kazi za kufanyia intavyuu mamia ya vijana waliojitokeza kuwania nafasi moja ya atakayekuwa mtangazaji nambari moja wa kituo kipya ya CloudsTV kinachotarajia kuanza kazi karibuni.
zamaradi akiongea na vijana kwenye foleni ya mwisho ya intavyuu. foleni zilikuwa tatu. ya kwanza kupatiwa namba. ya pili kusajili jina na wasifu, ya tatu ni hii
Saturday, August 29, 2009
NGOMA AFRICA Wanapofunga Mtaa Hamburg Ujerumani

Ras makunja na kikosi chake The Ngoma Africa band,juzi 21-08-2009waliufunga mtaa mrefu katikati ya jiji kubwa la Hamburg,Ujerumani.katika maonyesho ya Alafia -Afrika Festival,na kusababisha ulinzi mkali kuwepo katika onyesho hilo , mbele ya jukwaa kulijaa mashabiki ambao walikuwa wakidai kuwa ngoma africa ni bendi yao ya damu.
Nyuma ya jukwaa kulikuwa kumejaa Polisi ambao nao walisema kuwa baada ya kumalizika onysho hilo lazima Makunja na kikosi chake wasindikizwe na Ulinzi na hakuna mshabiki wa kuwasogelea! hiyo ilikuwa ikimaanisha FFU wa Ngoma Africa chini ya ulinzi wa washabiki na polisi walikuwa salama kabisa.
Poromota wa onyesho hilo aliwatangazia washabiki kabla ya muziki kuanza kuwa "Washabiki wanaombwa kucheza muziki mbele ya jukwaa" tafadhali nyuma ya jukwaa ni sehemu ya ulinzi tuu! jukwaa lipo kati! upande wa mbele washabiki na upande wa nyuma polisi,Ras Makunja na Ngoma Africa yake wamewekwa mtu kati!!

Ras Makunja akiwa na bendi yake Ngoma Africa
Waraka wa waislam
Friday, August 28, 2009
Sasatel yatinga kwa Kova
The Government of Tanzania will soon start construction of a monument and a podium
Mr Isdori Shirima the Arusha Regional Commissioner (Right), The Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism Dr Ladislaus Komba (second right) and some officials from the Ministry of Tourism listening to the site explanation given by an officer (not in the picture).
Washindi mbalimbali wa TIGO
Kulia ni Meneja promosheni na matangazo wa Tigo Redemtus Masanja akimkabidhi zawadi Rowland Mwakibete mshindi wa kitita cha milioni moja katika promosheni kabambe ya Tigo Kila Mmoja Anashinda wakati wa hafla fupi ya makabidhianao iliyofanyika makao makuu ya Tigo leo mchana.Katika anaeshuhudia ni Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando.
Serengeti Boys na dozi zake Sudan
Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Vijana U 17, Salleh Ali akidaka mpira langoni kwake huku mshambuliaji wa Ethiopia, Abdelkarim Hassen akiusubiri umtoke. Nyuma ni Hassan Hamisi akimlinda.Timu hizo zilichuana juzi katika mchezo wa kuwania Kombe la Chalenji la Afrika Mashariki na Kati, Tanzania ilishinda 1-0
Taarifa zilizotufikia hivi punde zina pasha timu ya Zanzibar imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kufungwa goli 2-1 na Elitrea katika mchezo wao wa Robo fainali
Thursday, August 27, 2009
sherehe za jeshi la wananchi kutimiza miaka 45
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).
JK amzika Askofu Mayala
mama kikwete azindua kampeni ya vodacom foundation ya mwezi mtukufu wa ramadhani
Mama Salma kikwete akiwasili kwenye eneo la tukio jana mjini Bagamoyo tayari kuzindua kampeni ya Vodacom Foundation ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo pamoja na kufuturisha sehemu mbalimbali nchini misaada kibao hutolewa

Mama Salma Kikwete akiwakabidhi vyakula watoto yatima ambao wanaishi katika mazingira magumu msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,Wilayani Bagamoyo jana
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Kweigr akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare na Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba huko Bagamoyo jana

baadhi ya wanafunzi wa madras katika hafla hiyo

Mama Salma Kikwete akimkabidhi vifaa vya charahani Mwenyekiti wa kikundi cha kina mama wanaolea watoto yatima Bi.Muridhia Bakari msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba,Wilayani Bagamoyo jana.
Mama Salma Kikwete akiwakabidhi vyakula watoto yatima ambao wanaishi katika mazingira magumu msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,Wilayani Bagamoyo jana
baadhi ya wanafunzi wa madras katika hafla hiyo
Mama Salma Kikwete akimkabidhi vifaa vya charahani Mwenyekiti wa kikundi cha kina mama wanaolea watoto yatima Bi.Muridhia Bakari msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba,Wilayani Bagamoyo jana.






