Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Dodoma mjini kuhusu kujitokeza kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amevaa vazi la asili la kabila la wagogo mara baada ya kuvalishwa na wakazi wa kijiji cha Mdemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.
Mke wa Rais Mwalimu Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisahihisha daftari la Lea Wimbe ambaye ni mlemavu wa kusikia mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya viziwi Kigwe. Mama Kikwete alitembelea shuleni hapo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma
Picha na Juma Kengele - Ikulu
No comments:
Post a Comment