Meneja Masoko wa Precision Air, Emilian Rwejuna (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wao katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2010 katika hafla ya uzinduzi wa mshindano ya mwaka huu kwenye Hoteli ya Moevenpick Royal Palm jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa PSI, John Wanyancha na Meneja Mauzo na Masoko wa Moevenpick, Zena Sapi ambao wote ni wadhamini wa mashindano hayo.
Miss Universe Tanzania 2009, Iluminata James akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ua uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta Miss Universe Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa Serengeti Breweries, Imani Lwiga na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Serengeti Breweriers Ltd Imani Lwinga kushoto akikabidhi Mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication Co. Ltd Maria Sarungi ambao ni wandaaji wa Miss Universe Tanzania kulia na katikati ni Miss Universe Tanzania 2009 Illuminata Jemsi, ikiwa ni udhamini wa shindano la Miss Universe 2010.
No comments:
Post a Comment