Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein,akifunua pazia kuweka jiwe la msingi majengo ya Shule ya Sekondari Wami katika kijiji cha Dakawa Wilayani Mvomero Morogoro jana,Dk.Shein amechangia shilingi milioni tatu katika ujenzi huo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Issa Machibya.Picha na Amour Nassor
Wednesday, September 30, 2009
Discussing...
MWANAMITINDO FATMA AMOUR KUZINDUA "MAGIC OF TANZANIA" NCHINI MAREKANI
Karen amesema wasanii hao kutoka mikoa ya Tanga, Zanzibar Bagamoyo Dar es salaam Arusha na Dodoma watashiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
Ameongeza kuwa mafunzo yataanza tarehe 6 oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, ameongeza kuwa wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs ambaye ataongoza wenzake 12 katika safari hiyo anatarajiwa kuzindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi utakaofanyika jimbo la Ohio tarehe 12 oktoba, pia atatambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine nchini Marekani.
Fatma Amour akitoa shukurani zake kwa Ubalozi wa Marekani kwa kumchagua kwenda katika mafunzo hayo yatakayochukua mwezi mmoja nchini Marekani.
kutoka kushoto ni Fatma amour,Zena Abdallah,Amoke Kyando aliyerejea kutoka katika mafunzo hayoSalma Masenga, Harieth Kagangule, Mwandale mwanyekwa (Big Mama) na Scolastca Malecela wakiwa katika picha ya pamoja
Mama Kikwete Twiga sekondari.
Tuesday, September 29, 2009
Ajinyakulia Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu
Mratibu wa Gofu wa kampuni ya Illovo Ltd, Pieter Van Eeeden (kulia) akimkabidhi mcheza gofu, thian Myburgh (kulia) Simu mpya aina ya Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu yaliyofanyika wiki iliopita katika uwanja wa gofu wa Illovo, Kilombero Mkoani Morogoro. Mashindanon hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Zain na kukutanisha wacheza golf mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.
Mambo ya uzinduzi wa michuano ya Netiboli
Katibu mkuu msaidizi wa CHANETA Rose Mkisi kushoto na Mweka hazina wa chama hicho Flora Kasambara wakiingia katika viwanja vya mashindano kabla ya kufunguliwa rasmi na mke wa rais Mama Salma Kikwete jana
Mke wa Rais Mama Salama Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya netball kwenye uwanja mkuu wa Taifa jana akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho ambapo Tanzania ilishinda magoli 33-19 mashindano hayo ya kimataifa ya Netball yanasimamiwa shirikisho la vyama vya Netball vya kimatifa International Federation of Netball Association (IFNA)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati alipofungua mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yanayofanyika nchini yakiandaliwa na chama cha Netball CHANETA yaliyoanza jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa. kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na anayefuata ni Anna Bayi Mwenyekiti wa Chama cha hicho.
JK afungua jengo la ubalozi wetu Washington DC
Jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani ambalo JK alilifungua jana asubuhi. Jengo hili limenunuliwa na serikali ya Tanzania kwa jumla ya dola za kimarekani $10,415,000.
JK akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani jana asubuhi
JK akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijinji Washington Marekani jana asubuhi.
JK akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Balozi iliyopo katika jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani jana asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na wapili kushoto ni Balozi wa Tanzania Washington Ombeni Sefue
Picha na Freddy Maro wa Ikulu
Barack Obama and First Lady Michelle Obama With World Leaders at the Metropolitan Museum in New York
Vyoo vya kikohozi.
Maria Nyerere azungumza na waandishi
Mjane wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere (Mama wa Taifa) akizungumza na waandishi nyumbani kwake Msasani Dar es Salaam jana, kuhusiana na tuzo aliyoipokea Mapema mwezi huu kutoka kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa inayotambua Mchango wa baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika.
Monday, September 28, 2009
Wanafunzi Kibasila Sekondari wafunga Barabara





WANAFUNZI wa shule ya sekondari kibasila na shule ya msingi kibasila leo walikua na mgomo kutokana na eneo hilo kuwa na ajali za mara kwa mara kusababisha vifo kwa wanafunzi wa shule hizo.
Tukio hilo lililotokea leo asubuhi ambapo wanafunzi wawili wa shule ya msingi kibasila waligongwa na mwananchi mmoja ambaye alikua akiwavusha barabara kugongwa na hali yake sio nzuri na yuko hospitali ya temeke kwa matibabu zaidi.Kwamujibu wa mashuuda wa tukio hilo walisema kuwa wanafunzi waliogongwa ni Consolatha Kilasa ,Wiliston Sango wote wa darasa la 5 waliokuwa wakitoka nyumbani kuelekea shuleni ata hivyo jina la msamaria mwema halikupatikana.
Akiongea na gazeti hili mmoja wa walimu alisema kuwa mwanafunzi mmoja aliyejulikana kwa jina Wiliston Sango yupo hospitali ya mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi kutokana na kujeruhiwa vibaya.
Pia katika tukio hilo wanafunzi waliweza kuzuia baadhi ya magari yasipite katika eneo hilo likiwamo gari la jeshi lenye namba za usajili 2813 JW97 Defender na gari la polisi PT-0176.
Makamu mkuu wa shule ya kibasila mwalimu Catherine Urio alito wito na kuomba wakala wa barabara kuweka matuta,taa,alama za pundamilia na askari wa kuongozea magari kwani kutokuwepo kwa vitu hivyo kunasababisha ajali nyingi na watu upoteza maisha kwa wingi.
Hatahivyo wanafunzi walisema kuwa hawataki kusikia siasa zinatendeka wanachotaka wao matuta yawekwe na taa pia trafiki awepo katika barabara hiyo ya changombe.
Wakati huo huo mwenyekiti wa serikali za mitaa Sophia Kinega alisema ni halali kwa wanafunzi kufanya mgomo huo kwani ajali nyingi zinatokea na kuua wanafunzi mara kwa mara kwani wanafunzi hao wanaona uchungu kuona wenzao wakipoteza maisha.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jordan Lugimbano aliwataka wanafunzi aongee nao ila wanafunzi hao walionekana wakimzomea,baada ya muda wanafunzi walikubali na kwenda kuongea nae iliwaweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Rais Kikwete akutana na Ban-ki-Moon New York
Afunga Ndoa na Wanawake Wanne Kwa Mpigo
Saturday, September 26, 2009
JK Na Kamaresh New York
JK na Ray chambers wa mumbe maalum wa malaria
Ajali zaingine jamani!!!
TBL yaipiga jeki kamati ya usalama barabarani
Friday, September 25, 2009
BASKETBALL CHARITY DAY
JAPAN YATOA BILIONI 2.4 KUSAIDIA MPANGO WA KUDHIBITI UKIMWI
Miss Tanzania ndani ya Vodashop
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania leo mchana huu wametembelea duka la Vodashop lililopo mtaa wa Samora karibu na Idara ya Habari Maelezo na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika duka hilo, kama unavyoona mmoja wa wafanyakazi wa vodacom katika duka hilo Jannet Massanja aliyesimama katikati akitoa maelezo kwa warembo hao na kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na warmbo hao shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika wiki ijayo oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es salaam.
Dar es salaam.
USAID YAMWAGA VIFAA VYA KUPIMIA KIFUA KIKUU
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni akiangalia kifaa cha kupimia ugonjwa ya kifua kikuu (Microscope) iliyokabidhiwa kwake na Elise Jensen (wa kwanza kulia) mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani (USAID) huku maofisa wa Wizara na shirika la USAID wakishuhudia, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Wizara ya Afya. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Microscope 40, Jokofu moja na microscopy slide boxes 1600 vyote vikiwa na thamani ya dola za Kimarekani 109,715 na vitagawanywa katika mikoa yote nchini.











