Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Showing posts with label Wizara. Show all posts
Showing posts with label Wizara. Show all posts

Friday, April 16, 2010

Mkulo na Mkukuta yake.


Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(katikati) akibadilishana mawazo jana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma na Mbunge wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Mkoani Mwanza, Dk. Raphael Masunga Chegeni(kushoto) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Lucy Owenya ( kulia) mara baada ya kumalizika kwa kukusanya maoni ya wabunge juu mchakato wa majadiliano ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania(MKUKUTA) ambazo zoezi hilo limeanza jana jioni na linaendelea nchini kote.


Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(kulia) akibadilishana mawazo jana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (katikati) pamoja na Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Clifford Tandari( kushoto) mara baada ya uzinduzi wa mchakato wa majadiliano ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania(MKUKUTA) ambazo zoezi hilo limeanza jana jioni na linaendelea nchini kote.

Read more...

Thursday, April 15, 2010

Waziri Mkulo azindua mchakato wa maoni ya MKUKUTA awamu ya 2 mjini Dodoma


Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kuanza kwa mchakato wa kujadili kuhusu Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) awamu ya pili. Mchakato wa kutoa maoni umeanza jana mjini Dodoma ambapo wabunge walipata fursa ya kutoa maoni yao jinsi ya kuboresha awamu ya pili ya MKUKUTA. wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wizara ya fedha na Uchumi John Haule (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Kuondoa Umaskini na Uwezeshaji Anna Mwasha(kulia)

Read more...

Thursday, April 8, 2010

PRINCESS MAXIMA WA UHOLANZI AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI

Princess Maxima mke wa mtoto wa malkia wa uholanzi akijadiliana jambo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo juu ya uimarishaji huduma za kibenki kwa wananchi waliowengi. Princess Maxima huyo na ujumbe wake yuko nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo atakutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali na taasisi za kifedha.


Princess Maxima akipokea zawadi ya vitu mbalimbali ikiwemo Kahawa, Chai na Korosho kutoka kwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Read more...

Wednesday, March 31, 2010

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VITABU

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiangalia vitabu mbalimbali vya sayansi vilivyotolewa kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia elimu ya Sayansi nchini.Kulia ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.

Wakuu wa vyuo na shule mbalimbali za Sayansi nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya sayansi za maabara kutoka kwa watu wa marekani jana jijini Dar es salaam.Vitabu 1920 vyenye thamani ya shilingi milioni 91 vimetolewa na kukabishiwa kwa wakuu wa vyuo hivyo.
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa chuo cha maabara Litembo kilichoko wilayani Mbinga mkoani Ruvuma sista Angelina Marry Kihwili vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi na Afya nchini.Katikati ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.


Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa shule za maabara za Sayansi, Muhimbili Mr. Colman Msuya vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi nchini.

Read more...

Tuesday, March 30, 2010

Maige aanza upandaji miti Shinyanga


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige mwenye suti nyeusi, akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Town iliyoko mjini Shinyanga,wakati wa sherehe za kuelekea Siku ya Taifa ya kupanda Miti nchini ambayo kitaifa inafanyika Aprili Mosi mkoani Shinyanga, aliyeshika. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Felician Kilahama na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Fabian Stanslaus.

Read more...

Friday, March 26, 2010

Waziri Membe afungua Diaspora II London


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mwanaidi Majaar wakipata maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba za kuuza kutoka Miranda Lutege,Meneja uhusiano wa Benki ya Biahara ya Afrika( CBA)muda mfupi kabla Waziri Membe hajafungua mkutano wa pili wa Diaspora hapa London leo.

Read more...

Thursday, March 18, 2010

Chiza azindua mradi wa maji Msoga

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Chistopher Chiza (suti nyeusi)akikagua mradi wa maji wa umwagiliaji huko kijijini Msoga Pwani wakati wa uzinduzi huo leo. (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magesa Murongo.


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akiweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Msoga mkaoni Pwani leo

Naibu wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza aliavaa suti akipokea maelezo kutoka kwa wafugaji wa Kimasai leo katika uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi kijini Msoga mkoani Pwani leo.




Naibu Waziriwa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akiangalia vijidudu vya mbu kwanjia ya darubini leo katika kijiji cha Mwendapole Kibaha mkoani Pwani katika mabanda ya maonyesho ya kuadhimisha miaka ya 22 ya wiki ya maji kilele cha maadhimisho hayo ni machi 22, 2010. Picha na Mwanakombo Jumaa -Maelezo

Read more...

Wednesday, March 17, 2010

Familia ya karimjee yatoa msaada kwa wananchi Kilosa

Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akipokea msaada jana mjini Dar es salaam wa magodoro 2000 na blanketi 2000 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Kilosa waliokubwa na mafuriko ambayo yaliwasababishai kupoteza mali zao zote. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 75 umetolewa na Mwenyekiti wa Karimjee Jivanjee Family Bw. Hatim Karimjee (kushoto) kwa niaba ya wenzake.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Read more...

MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF AMALIZA MUDA WAKE WA KAZI NCHINI


Bw. Heimo Laakknonen akifurahia zawadi ya Kinyago alichopewa kama zawadi na Mh. Waziri mara baada ya kuifungua
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF Bw. Heimo Laakkonen akifurahia zawadi aliyopewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Margaret Sitta. Bw. Heimo amefika ofisini kwa Mhe. Waziri jana kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini

Bw. Heimo akimvisha Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Margareth Sitta Skafu kama zawadi kwa Mhe. Waziri

Read more...

Tuesday, March 16, 2010

NAIBU WAZIRI CHIZA AZINDUA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MWANGOMOLE.

Naibu Wazri wa maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akizindua mradi wa kilimo cha Umwagiliaji wa Mwangomole, katika Kijiji cha Kwala, Kibaha mkoa wa Pwani leo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho, maadhimisho hayo ya 22 ya wiki ya Maji pia yanafanyika sambamba na maonyesho kwenye viwanja vya Mwendapole.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christophe3r Chiza (kaundasuti) akiangalia ramani ya mradi huo (anayeamuonesha (katikati ) ni Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi, Rogers Ishengoma. (Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo)

Read more...

Thursday, March 11, 2010

SEMINA YA KUHAKIKI RIPOTI YA (APRM TANZANIA) YAFANYIKA JIJINI DAR

Wajumbe wakiwa Mkutunoni. APRM (African Peer Review Mechanism) ni Mpango wa Hiari wa Nchi Wanachma wa Umoja wa Afroka Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Borauliobuniwa na Viongozi wa umoja huo 2003.


Balozi na Mkurugenzi Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Francis Malambugi akifungua semina ya siku moja jijini Dar esalaam leo. Semina hiyo ni ya Kitaifa ya kuhakiki Ripoti ya nchi iliyoandaliwa na APRM Tanzania.(Africa Peer Review Mechanism)- Mpango wa Hiari wa nchi za Umoja wa Afrika Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Borakwa madhumuni ya kubadilishna mawazo juu ya Ripoti ya nchi Tathmini ya Utawala Bora.


Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatillia hotuba ya mgeni rasmi ambae pichani hayumo


Baadhi ya maofisa mbalimbali wakisikiliza mambo mabalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa na mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina hiyo inayofanyika jijini Dar es salaam.
Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo


Read more...

Mkama 'Mwenyekiti Mpya wa bodi ya TSN'


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana. Wilson Mkama kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya Magazeti ya serikali TSN.
Uteuzi ambao unaanza Februari 26 mwaka huu.
TSN ni wachapaji wa magazeti ya daily News, Sunday News, HabariLEO na HabariLEO Jumapili.
Mkama kabla ya kustaafu kwake alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Kabla ya kwenda Maji Mkama alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwapo ya kuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam.
Kufuatia uteuzi huo Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
1.Bi Hajjat Hawa Manga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa watumishi wa Umma (PSPF).
2.Bwana.Kalua Simba, Mchumi wa kujitegemea kutoka sekta binafsi.
3.Clement Mshana , Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
4.Bwana.Charles Rajabu, Afisa Habari Mkuu Daraja la kwanza,Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.

Read more...

Dr. Asha-Rose Migiro hosts Zanzibar Minister in New york


The UN Deputy Secretary General Dr. Asha-Rose Migiro shakes hands with the Zanzibar Minister For Women, Children and Gender Ms. Aaha Abdullah Juma who paid a courtesy call on her today in New York. Minister Asha Abdullah Juma is attendind

Read more...

Maafisa mipango

Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akifungua mkutano wa siku tatu wa maafisa Mipango , wachumi kutoka Serikalini unaoendelea mjini Morogoro.



Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na wachumi na maafisa mbalimbali (hawapo pichani) jana mjini Morogoro wakati alipofungua mkutano wa siku moja wa Maafisa Mipango na Wachumi kutoka katika Wizara , Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini. uliojadili mambo mabalimbali ya kiuchumia na mpiango kwa ujumla.

Read more...

Makatibu Wakuu waongelea reli ya Afrika Mashariki

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki Balozi Juma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Reli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar kuanzia kesho, dhima kuu ikiwa ni Uendelezaji wa mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kudumisha ushirikiano, kurahisisha usambazaji wa bidhaa na kukuza uchumi za Jumuiya ya Afrika Masharikai na zile za SADC na COMESA.


Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu Injinia Omar Chambo (kulia)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uimarishaji wa miundombinu ya reli katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ujenzi wa reli mpya kutoka Dar es salaam - Tanzania mpaka Kigali - Rwanda ambayo pia itaiunganisha nchi ya Burundi. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax.

Read more...

Tuesday, March 9, 2010

TANZANIA KWENYE MKUTANO WA WADAU WA KAHAWA NCHINI GUATEMALA

Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Stephen Wassira (wa pili kutoka kushoto), akiwa na Wajumbe wengine kwenye Mkutano huo ni Bw. Pius Ngeze, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa (TCB) Adolf Kumburu, Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Professa James Terri, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa (TACRI) na Bwana Yusuf Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.


ukumbi wa mkutano huo wa kahawa




Read more...

BENARD MEMBE AONGEA NA WANAFUNZI WA ALGERIA

Mh.Membe akiwa katika picha ya pamoja na ana ATSA walio hudhuria kikao kicho na wazir(hakuna wanawake kwa kuw kikao kilikuwa ucku napia cha kishtukiza kutokana na ratiba ya waziri, katika ATSA kuna kina dada pia)


MH. MEMBE akiwa katika picha ya pamoja na viongozi w juu wa ATSA, Kutoka shoto ni Rais wa ATSA mh.SEIF PEPO akifuatiwa na Mh.MEMBE ,akifuatiwa na makamu wa Rais wa ATSA.mh.Habibu H.RUHOMBO na mwisho i mwweka hazina na wa atsa mh.OMARY PINDO

Mh. Membe akiwa katika picha ya pamoja yeye na ujumbe wake na viongoz a juu wa ATSA kutoka kuli ni DR.mshokolwa akifutiwa na mbe wa mbea mjini Mh.BENSON MPESYA akifuatiwa na mkurugenzi wizara mambo ya nje anayeshughulikia mauala ya Afrika balozi.


Mlezi wa ATSA DR.Mshokolwa akitoa nasaha zake kwa wanATSA huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyezuru Algeria Kikazi Mh. Bernanrd Membe akimsililiza ka makini mwisho wa meza


Read more...

Friday, March 5, 2010

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII Prof. DAVID MWAKYUSA ATEMBELEA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizindua ramani inayoonyesha mtandao wa vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali na sehemu vilipo hapa nchini mara baada ya kutembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mganga Mkuu wa serikali Dkt Deo Mtasiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba (aliyesimama nma ya waziri)


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba(katikati) akimwonyesha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa maeneo mbalimbali na namna Mfuko huo unavyoendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi ili kuinua utoaji wa huduma kwa wateja.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akipata maelezo ya namna mtambo mkuu wa kuhifadhi kumbukumbu (main server)unavyofanya kazi ndani ya ofisi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

Read more...

Thursday, March 4, 2010

WAZIRI WA UCHUMI MUSTAFA MKULO ATEMBELEA KILIMO CHA UMWAGILIAJI BABATI

Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akisikiliza maelezo juzi kutoka kwa Mkulima wa Mpunga Mohamed Shaban(kulia) juu ya scheme ya umwagiliaji ya kilimo cha mpunga ya heka 900 katika Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati. Wengine wanaosikiliza ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mercy Sila(kushoto). Waziri Mkullo alikuwa na ziara ya kutembelea mashamba hayo na kujionea shughuli za uzalishaji wa mpunga na pia kupata maoni kutoka kwa wakulima hao kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa zao hilo kupitia uwezeshaji wa Serikali.



Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo(katikati) akiwahutubia wakulima wa zao la mpunga wa Kijiji cha Mawemailo wilayani Babati juzi mara baada ya kutembelea scheme yao ya umwagiliaji yenye heka 900 mashamba ya mpunga. Waziri huyo aliwasisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wao waliouonyesha ili kuzalisha zao hilo kwa manufaa yao na Taifa. Wengine kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Dkt Ian Langibori na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Emmanuel Kamba. Picha na Tiganya Maelezo-Babati

Read more...

Wednesday, March 3, 2010

UN na Wanawake


WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTAWALA BORA MHE. SOPHIA SIMBA AKISHIRIKI NA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 54 WA KAMISHENI YA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HALI YA WANAWAKE. WAZIRI SIMBA ALIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO AMBAPO ALISISITIZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MCHAKATO WA KUTAFUTA AMANI NA AKAINISHA JIHUDI MBALIMBALI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KATIKA KUBORESHA HALI YA WANAWAKE( PICHA NA HABARI KWA HISANI YA UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP