Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Showing posts with label Waziri Mkuu. Show all posts
Showing posts with label Waziri Mkuu. Show all posts

Friday, April 16, 2010

Bungeni Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Aprili 19, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Spika wa Bunge Samuel Sitta (kulia) wakati alipoongoza kikao cha wabunge hao kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 18, 2010. Kushoto ni Kaimu Katibu wa wabunge wa CCM na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama. .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA KUSINI NA MALAWI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere , Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 16, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya (katikati)na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere , Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Peter Msolwa wakitoka kwene ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, leo Aprili 16, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Thursday, April 15, 2010

Bungeni Dodoma

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 15, 2010


Baadhi ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikili Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma leo.


Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo akifungua mkutano wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wanawake kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma

Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo (waliokaa watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa baada ya kufungua mkutano wao wa mwaka kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha ST. Gaspar Conference Cetre Mjini Dodoma,





Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya wabunge, bungeni mjini Dodoma, Aprili 15,2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Ta, Dr. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akifurahia jambo katika Mazungumzo na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama kwenye viwanja vya Bunge Aprili 15, 2010.




Read more...

Wednesday, April 14, 2010

Bungeni Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Usalama Barabarani upande wa watu wenye ulemavu , Jutoram Kabatelle kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Aprili 14, 2010.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa , Kingunge Ngombale -Mwiru kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma,


Waziri mkuu, Imzengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa Viti Maalum, Gaudentia Kabaka (katikati) na Mbunge wa Busanda , Lolesia Bukwimba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Aprili 14, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Monday, April 12, 2010

Bungeni Dodoma

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma, Aprili 13, 2010. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Askari wakihamisha siwa kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya Aprili 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo katika mazungumzo kati yake na Mbunge wa Kwimba, Bujiku Sakila kwenye viwanja vyaBunge Mjini Dodoma, Aprili 13, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Tuesday, March 30, 2010

Mtoto wa Mkulima ndani ya Vietnam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride la heshima

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea maua kutoka kwa mtoto wa Vietnam wakati alipopokelewa rasmi kwenye viwanja vya Ikulu ya Hanoi , Machi 29, 2010 kuanza ziara yake ya kikazi nchini Vietnam. Kulia ni mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung.

Read more...

Friday, March 26, 2010

Pinda ndani ya Japan

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Japan, Mhe. Lumumba Lumbumba baada ya mkutano wake na mabalozi wan chi za Afrika mchini Japan uliofanyika kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo, Machi 26, 2010. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga picha na Gavana na Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu ya Japan, Bw. Shosaku Yasui kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Japan Machi 26, 2010.

Read more...

Wednesday, March 17, 2010

Waziri mkuu wa Finland na Tanzania wazindua Taasisi ya Maendeleo Endelevu Dar es salaam

Waziri mkuu wa Finland Matti Vanhanen's na waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo Endelevu Dar es salaam (Dar es salaam Institute for Sustainable Development) jana jijini Dar es salaam. Taasisi hiyo inafadhiriwa na serikali ya Finland.


Waziri mkuu wa Finland Matti Vanhanen's akiwahutubia viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo Endelevu Dar es salaam (Dar es salaam Institute for Sustainable Development) kwa lengo la kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya umma kuelewa sera ,mipango na utekelezaji wa majukumu mbalimbali, uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda,Mwenyekiti wa Bodi Ms Ritva Koukku- Ronde na Balozi wa Finland nchini Tanzania Juhan Toivonen.

Read more...

Waziri Mkuu wa Finland ziarani Tanzania

Pinda na Waziri Mkuu wa Finland, Matti Vanhanen wakitazama ngoma baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kuendelea na ziara yake nchini iliyoanzia Arusha, Jumapili iliyopita.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu wa Finland, Matti Vanhanen ambaye aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jana kuendelea na ziara yake nchini iliyoanzia Arusha Jumapili iliyopita (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Thursday, March 11, 2010

Pinda na Kaimu Rais wa Nigeria


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Rais na Kaimu Rais wa Nigeria, Dr. Goodluck Jonathan kwenye hoteli ya Transcorp Hilton jijini Abuja anakohudhuria Mkutano wa Viongozi wa wakuu kuhusu maendeleo ya biashara na viwanda vya kilimo barani Afrika. Alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo.

Read more...

Wednesday, March 10, 2010

Waziri Mkuu akiwa Nchini Nigeria

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipoata maelezo kutoka kwa balozi wa Tanzania nchini Nigeri, Balozi Msuya Mangachi (kulia) kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo katika jiji la Abuja March 9, 2010.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kushoto akikagua eneo lililotengwa akwa jili ya jenzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria katika jiji la Abuja wakati alipolitembelea March 102010.

Read more...

Monday, March 8, 2010

Pinda alipotembelewa na Waziri Mkuu wa Msumbiji

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Aires Bonifacio Baptista Ali


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Msukbiji, Aires Bonifacio Baptista Ali (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mazungumzo ya kiserikali (Official Talks) kati yao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Msumbiji, Aires Bonifacio Baptista Ali (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mazungumzo ya kiserikali (Official Talks) kati yao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Aires Bonifacio Baptista Ali baada ya mazungumzo ya kiserikali kati kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri MKuu jijini Dar es salaam.



Read more...

Wednesday, March 3, 2010

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda Akutana Na Wakuu Wa Mikoa Dodoma

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda (hayupo pichani) wakati alipowahutubia mkutano wa kazi kati yake na Wakuu wote wa mikoa nchini mjini Dodoma


Waziri Mkuu, Mkuu Mh.Mizengo Pinda akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Kiongozi wa Wakuu wa Mikoa nchini, Mh. Anatoli Tarimo (kushoto) kuingia kwenye ukumbi wa mikutano mjini Dodoma kuongoza kikao cha wakuu wa mikoa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mh. Celina Kombani na Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mh.Aggrey Mwanri.

Read more...

Tuesday, March 2, 2010

Pinda katika mazungumzo na wageni wake


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Uturuki Nchini, Kadri Sander Gurbuz katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam leo.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi nchini, UNHCR,, Mhe. Olyseyi Bajulaiye, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini leo.

Read more...

Tuesday, February 23, 2010

Dk Shein atembelea U-Dom

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM, wakati alipotembelea Chuo hapo leo



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Idris Kikula baada ya kukamilisha ziara yake ya kukitembelea Chuo kikuu cha Dodoma UDOM leo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo hicho

Read more...

Pinda ndani ya Ziara yake Tabora


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (Kulia) wakizungumza na watoto baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Sokoine, Igunga wakiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora , Februari 21, 2010.



Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Buzoli wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofungua josho la ng’ombe katika kijiji cha Bulayang’ombe wialyani Igunga akiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora

Read more...

Monday, February 22, 2010

Pinda uso kwa uso na Rostam


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akipata maelezo kuhusu bwawa la maji la Mwamapuli wilayani Igunga, Tabora kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz (wa tatu kulia) wakati alipokagua bwawa hilo linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimussa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Monday, December 14, 2009

Pinda na Apiyo


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Timothy Apiyo wakati alipomtembelea nyumbani kwake Sitakishari, Ukonga jijini Dar, kumjulia hali wikiendi hii. Mzee Apiyo alikuwa amelazwa Sauzi kwa matibabu na anaendelea vyema

Read more...

Thursday, October 22, 2009

WAFANYA BIASHARA KUTOKA UJERUMANI WAJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara na wawekezaji toka Ujerumani waliokuja kujionea fursa za uwekezaji na biashara nchini, wafanyabiashara hao walimtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 20, 2009.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read more...

Tuesday, October 13, 2009

Pinda na Nyerer Memorial Scholarship Fund

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa Elimu kwa Watoto wa Kike ulioanzishwa na Gavana wa Benki Kuu (Mwalimu Nyerere Memorial Scholarship Fund) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2009. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndullu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mawaziri Wakuu wastaafu. Edward Lowassa (kulia) na Dr. Salim Ahmed Salim katika hafla ya kuchangia mfuko wa maendeleo ya Elimu kwa watoto wa kike (Mwalimu Nyerere Memorial Scholarship Fund) kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2009.

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP