Friday, February 26, 2010
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba ziarani nchini Misri.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba akiwa katika picha ya pamoja na Sheikhul-Azhar (GRAND SHEIKH OF AL-AZHAR) Pr. Dr. Muhammad Sayyed Tantawyi katika Ofisi zake za Masheikhatul-Azhar zilizopo Darassa

Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa S Simba akiwa pamoja na katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Kitaanzania wasomao Nchini Misri (T.S.U) na Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Al-azhar Cairo Nd,Ghalib Nassor Monero katikati Sheikhul-Azahar Baada ya Mazungumzo katika ofisi za Sheikhul-Azhar Daraasa Cairo.

Rais Kikwete aliporejea Dar
JK akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. William Lukuvi mara baada ya kuwasili jioni hii katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nje ya nchi kwenye ziara ya kikazi nchini Uturuki na Jordan. Kabla ya kutua Dar asubuhi alipitia Mwanza kufungua mkutano mkuu wa TAKUKURU
Thursday, February 25, 2010
Dr. Kimei awaaga waliomaliza Kidato cha sita Tambaza
Wahitimu wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Tambaza wakimsikiliza mgeni rasmi Dk Charles Kimei wa CRDB
MWANAFUNZI BORA TANZANIA 2009 APOKEA ZAWADI ZAKE
Baba Mzazi wa Imaculata Prof. Restori Mosha akizungumza na waandishi wa habari kuelezea kipaji cha mtoto wake Imaculata Mosha wakati alipopokea zawadi yake kutokana na kufanya vyema katika mtihani wa kidato cha nne mwak 2009, kulia ni Immaculata Mosha

Mshindi wa jumla kwa masomo yote nchini na kuwa mshindi wa kwanza pia katika masomo ya sayansi kwa kupata "A" katika masomo yote ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2009 Immaculata Mosha, akipokea zawadi yake ya Kompyuta aliyopewa na Chuo cha Clever Tourisim & Hotel Management Hotel kutoka kwa Afisa Elimu Mkuu Wizara ya Elimu Bi. Doroth Mwaluko katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo , Imaculata pia alikabidhiwa shiligi 100.000 kutoka kwa chuo hicho.
KITABU CHA MOSSY MAGERE
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akizindua kitabu cha Mwandishi Mossy Magere (kulia) kinachohusu uchaguzi mkuu 2010 kilichobeba jina "Mshike Mshike wa kisiasa 2010",
Rais Kikwete afungua mkutano wa mwaka wa TAKUKURU
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo unaofanyika mjini Mwanza leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea na kushoto ni Waziriri wan chi Ofisi ya rais Utawala Bora, Sofia Simba.
Miriam Gerald apandishwa tena kizimbani
Miss Vodacom Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’, leo wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 na watuhumiwa hao wanaendelea kuwa nje kwa dhamana.
Anna Makinda apata mpinzani Jimboni kwake.
Mwanasheria wa kujitegemea Bw. Deiniol J. Msemwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Njombe Kusini Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi Oktoba mwaka huu endapo atapitishwa na chama chake.
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo na yeye mwenyewe akapata wasaa wa kuongea na wanahabari na kuwatangazia nia yake hiyo.
Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na Mwanasiasa Mkongwe toka enzi za Uhuru mwanamama shupavu Anna Makinda ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dainiol Msemwa amesema ametuhubutu kutangaza nia yake hiyo kwa kuwa uwezo anao na katiba ya chama cha mapinduzi inamruhusu kufanya hivyo, lakini pia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki hiyo ya kuchagua ama kuchagulia kama raia wa Tanzania.
Katika Picha wengine wanaofuatia ni Enock Ngombale Mwiru Mshauri wa siasa wa mgombea na mwisho ni Jerome Joseph Msemwa wakili
Hii ndiyo adha ya kuota manyoya, usiombe yakukute.
Huyu nae uso wote unamnyoya. Iwapo kama tendo lililovuma siku kadhaa na kuwa gumzo jijini Dar es Salaam juu ya omba omba aliyemuotesha mtu manyoya ni lakweli basi mfano wake ndo huu je inakutokea utafanya nini?
Thursday, February 25, 2010MABALOZI WATEULE WAMUAGA RAIS KARUME
Executive Solutions Wamuombea Alan Turner
Wafanyakazi wa Executive Solutions waliohudhuria misa hiyo maalum ya Turner.
Wastaafu wa iliyokuwa EAC walonga juu ya mafao yao.
WARSHA YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KUELEKEA UCHAGUZI
Washiriki na waandishi wa habari walioshiriki mjadala wa majukumu ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Majadala huo uliandaliwa na Sauti ya Ujerumani.

Mwenyekiti wa MISA –TAN Ayub Rioba akisisitiza jambo jana mjini Dar es salaam kwenye mjadala wa majukumu ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Wengine katikakti ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dunstan Tido Mhando na Mkuu wa Sauti ya Ujerumani kanda Afrika na Mahariki ya Kati Ute Schaeffer (kushoto) .

Picha zaidi za ziara ya JK Jordan
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jordan Samir Rifai.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Seif Ali Iddi na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jordan, Ameir Al Hadidi wakitia saini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Uchumi na Sayansi kati ya Tanzania na Jordan huko Amman, mji mkuu wa Jordan wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo
BALOZI DAUDI MWAKAWAGO AFARIKI DUNIA!
HABARI ZILIZOPATIKANA MUDA SI MREFU ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.
MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.
BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU.
ALIWAHI PIA KUCHAGULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, KOFFI ANNAN KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.
Wednesday, February 24, 2010
Simba 1-1 African Lyon
Matokeo ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika ya Simba na African Lyon umemalizika kwa sare ya 1-1, goli la A. Lyon limefungwa dakika ya 5 na Sentongo, wakati la Simba limefungwa dakika ya 81 na Musa Hasan Mgosi.
Read more...ZATI HONOURS ZANZIBAR HISTORIAN
MEMBERS OF ZATI, COMMISSION FOR TOURISM AND REPRESENTATIVES OF VODACOM AND KCB ON A GROUP PICTURE..CELEBRATING THE SUCCESS OF THE EVENING
.jpg)





