Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, April 12, 2010

Rais Kkwete apokea ujumbe maalumu na mchango kutoka UVCCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mchango wa jumla ya Tshs.1,482,200/- kutoka kwa jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga kwaajili ya fomu ya ugombea urais ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makabidhiano hayo yalifanyika juzi jioni ikulu jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi wote wa CCM mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Stephen Julius Masele amnaye pia alisoma ujumbe maalumu wa vijana wa mkoa wa Shinyanga.

Viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam juzi jioni(picha na Freddy Maro).

Read more...

Friday, April 9, 2010

WASHINDI WA NITASOMA SCHOLARSHIP PROMOTION

Bw. Valentino J. Mhoja kutoka Dar es salaam Institute of Technology akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 3 kutoka 4Layers (T) Ltd's Levis Paul akikabidhi zawadi hio Kushoto ni Bi. Venancia Donald.

Bi.Venancia Donald akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 1 kwa niaba ya Witness Lucas wa Tumaini University Iringa. Akikabidhi zawadi hizo kulia ni Levis Paul Campaign & Marketing Manager 4layers (T) Ltd. Shughuli hio fupi ilifanyika leo katika ofisi ya kampuni hio iliyoko Msasani Dar es salaam.

Read more...

Thursday, April 8, 2010

BASI LA VITU LAINI LAPATA AJALI LAUA IRINGA


Basi la kampuni ya vitu laini (pichani )lililokuwa likitoka Lulanzi wilaya ya Kilolo kuja mjini Iringa limepinduka katika eneo la Tagamenda mpakani mwa wilaya ya Kilolo na Manispaa ya Iringa na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 10
Ajali hii imetokea majira ya saa mbili asubuhi.
Picha kwa hisani ya Francis Godwin Blog

Read more...

JK akutana na Wazziri wa Ujerumani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Dr.guido Westerwelle(wapili kushoto) pamoja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Bwana Dirk Niebel(kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.



Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Dr.Guido Westerelle Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi.

Read more...

Mavazi mengine ni utata mtupu!


Read more...

Halmashauri Kuu ya CCM yakutana Dar es Salaam leo


Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC wakiwa katika kikao chao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu mkuu wa CCM Bwana Yusuf Makamba wakiingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam tayari kuanza kwa kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, April 8, 2010. Wengine kutoka kushoto ni Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mwenyriti wa CC na Rais Mstaafu,Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyeti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Amani Abein Karume, Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa.

Read more...

PRINCESS MAXIMA WA UHOLANZI AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI

Princess Maxima mke wa mtoto wa malkia wa uholanzi akijadiliana jambo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo juu ya uimarishaji huduma za kibenki kwa wananchi waliowengi. Princess Maxima huyo na ujumbe wake yuko nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo atakutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali na taasisi za kifedha.


Princess Maxima akipokea zawadi ya vitu mbalimbali ikiwemo Kahawa, Chai na Korosho kutoka kwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Read more...

HARUSI FASHION SHOW ON 10 APRIL



Tanzania’s First and Premier Wedding Fair

TWO DAY EXHIBITION READY TO ROLL

HARUSI FASHION SHOW ON 10 APRIL

With 52 exhibitors showcasing the best in the Tanzanian wedding Industry, the 9th and 10th April 2010 shall be billed as the Dates when Tanzania`s first premiere wedding fair, Harusi Trade Fair, will be held at the Diamond Jubilee. It is geared to be the one stop shopping experience for the discerning bride and groom and their families and friends.

"We are very excited to have received such an enthusiatic response from all the wedding industry stake holders and we hope that this shall be the beginning of bigger and better things to come" Said Mustafa Hassanali organiser of the Harusi trade fair.

On 10 April , the Trade Fair shall close showcasing a wedding fashion show featuring wedding gown designers and Boutique owners showing their collections for KITCHEN PARTY, SEND-OFF, and BRIDAL GOWNS

Entrance for the EXHIBITION is 2,000 ONLY

Harusi trade fair is sponsored by East Africa Radio and TV, Vayle springs, 2M Media, Global Outdoor, Black fox models, Ultimate security, Daily news, Habari Leo and Oryx gas Tanzania ltd.

NOTE TO EDITORS

HARUSI TRADE FAIR EXHIBITORS Lotus Creative Concepts

Nadds House Events hire

Ham Bakerie

Zanzibar Hospitality Services

Fanina investment & Catering services

Dekor Craft

Endepa Event Planners

Luxe Papers

The Wedding Planners and Fantastic Cards Int

Mercy G Beauty Parlour

paper designs

Cathy design& décor

petals & Leaves

Oriflame EA LTD

GABRIEL MOLLEL

Party Cakes

Vayle Springs LTD

AK'S LTD

Upper Zonal Trading

NIRVANA

MHGALLERY

Tanzania Bloggers Network

8020 Fashions

Rebecca Fashion TZ LTD

My shot catering

Kinara Mobile Studio

Baker's Nest Ltd

Swan Fashion

queens jewellers Ltd

Rimza Ali

TEDDZZZ

Slice Of wedding

MSDesign

Markham Suites

Wain Africa LTD

Touch Spa

The Flying Chefs

Mustafa Hassanali Wedding

My shot Production

Big Solutions company

Oryx Gas Tanzania LTD

Patners Wedding Shop

khushya

Al-Musawir

Gracella Bride Wardrobe

Malaika Event Design & Rentals

Entertainment & Music Proffessionals

Décor Place

Modern Catering Equipment Hire

Tally Fashion & Designers

Shear Illusions

It is a trade fair whereby all suppliers and vendors dealing with anything to do with weddings will exhibit their products and services under one roof.

Exhibitors include, wedding gown designers, caterers, cake makers, wedding planners, hotels, Beauty Salons, Decor and much more.

The Fair is geared to be a BI-ANNUAL event reaching over 100,000 about-to-be-married, their families and friends, actively involved in the wedding planning process.

Read more...

Wajumbe wa kamati ya huduma ya jamii ya bunge watembelea ujenzi wa kampasi ya chuo kikuu cha SUZA


Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipotembelea ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) iliyopo Tunguu, nje kidogo ya mji wa Zanzibar hapo tarehe 7 Aprili, 2010. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Omari S. Kwaangw (katikati aliyefunga mikono) na Mheshimiwa Haroun A. Suleiman, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye suti nyeusi na kofia kati) walijumuika pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo na maofisa wengine wa Wizara na SUZA katika picha hii. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo inategemewa kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Read more...

Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika watembelea bunge la Pakistan

Spika wa Bunge la Pakistan, Mhe. Dr. Fahmida Mirza akizungumza na wabunge toka Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika ambao wako Pakistan kwa ziara ya kikazi. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola ambae pia ni mbunge wa Bunge la Pakistan, Mhe. Kashmala Tariq, wa pili toka kulia ni Spika Mirza na watatu kulia ni Mhe. Elijah Okupa toka Uganda, Wa nne ni Mhe. Beatrice Shellukindo na Kushoto ni Katibu wa Msafara huo, Saidi Yakubu wa Bunge la Tanzania

Wabunge toka Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola na Katibu wao wakifuatilia mjadala wa mabadiliko ya Katiba ndani ya Bunge la Pakistan

Read more...

Dalali awafunika akina Wambura, Rage

Ngoma na matarumbeta hayakuwa nyuma kwani yalikuwepo kumsindikiza Mzee Dalali wakati alipojitokeza katika kuwania nafasi ya kutetea yake na kuwa tayari kuwakabili akina Ismail Aden Rage, Michael Wambura katika kuwanania nafasi ya Uenyekiti.


Baadhi ya mashabiki wa klabu walijitokeza kwa mamia ikiwa ni kuonyesha imani yao kwa Mzee Dalali wakati alipojitokeza kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake katika mtaa wa Msimbazi

Mwenyekiti wa sasa wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam ambayo inamaskani yake Mtaa wa Msimbazi Hassan Dalali( mwenye mpira) leo mchana alitinga klabuni hapo kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo tena akisindikizwa na umati mkubwa wa washabiki na wapenzi wa timu hiyo.

Read more...

Jamaa hajajua kama Guta lake ni Jike au Dume, yuko bize akichunguza.

Chini na Juu Dereva wa Guta akiwa chini ya uvungu wa guta lake lililosheheni mzigo, akitengeneza baada ya usafiri huo kumuharibikia akiwa katika barabara ya Nyerere eneo la Darajani jijini Dar es Salaam.



Picha kwa hisani ya Sufian Maphoto Blog

Read more...

Quality Group na Uchumi Group kujenga Dukakuu Dar es Salaam


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uchumi Group ya Kenya, Jonathan Piano (kulia), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi, Kenya juzi, wakati wa hafla ya kusaini mkataba na Kampuni ya Quality Group ya kuanzisha Dukakuu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Grup, Yusuph Manji na mwingine ni ofisa wa kampuni ya Quality Group aliyetambulika kwa jina moja la Vasu



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji (kushoto), akibadilishana hati ya mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uchumi Group ya Kenya Jonathan Piano, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kuanzisha Dukakuu jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika Nairobi juzi.

Read more...

Tanzania wakumbuka Hayati Karume


Kutoka kushoto ni Rais wa Zanzibar , Amani Abeid Karume, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha wakisoma Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Abeid Karume, iliyofanyika jana ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume(katikati) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Mrisho Kikwete,pamoja na vingozi wengine wa Kitaifa na wananchi wakiwa katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,Rais wa Kwanza wa Zanzibar,wakimuombea dua katika kumuenzi tokea kufa kwake na kutimia miaka 38,huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana.


Akina mama wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika khitma ya dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar,iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.



Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Ali Mohammed Shein,akimsalimia Mama Fatma Karume,baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Rais Abeid Amani Karume,iliyoambatana na khitma na kutimiza miaka 38 tokea kifo chake huko Afisi Kuu ya CCm Kisiwandui,Mjini Zanzibar jana.










Baadhi ya wananchi wakisoma khitma ya kumuombea dua marehemu Mzee Abeid Karume,muasisi wa ASP na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,kwa kutimiza miaka 38 tokea kifo chake katika ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui jana.


Read more...

Bangi yateketezwa Tarime

Mkuu wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevya polisi SACP Godfrey Nzowa Akichoma bangi katika shamba lililoharibiwa katikaoparesheni ya kupambana na uhalifu wa ujambazi wizi wa mifugo na kilimo cha dawa za kulevya, poaresheni hiyo imeendeshwa kwa wiki moja sasa katika mkoa wa kipolisi wa Tarime/ Rorya

Mtuhumiwa anayedaiwa kushughulika na kilimo cha Bangi Tyeno Rasto Nyaoke akiwa mbaloni katikati ya askari ambao wanaendesha oparesheni maalum katika mkoa wa kipolisi wa Tarime/Rorya

Read more...

Wednesday, April 7, 2010

Rais Karume akabidhi funguo kwa wananchi waliovunjiwa nyumba


Pichani KuliaWaziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shmsi Vuai Nahodha,Mke wa Rais Mama Shadya Karume,Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa habari na Michezo,Ali Juma Shamuhuna na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abadalla Mwinyi Khamis,wakiwa katika sherehe za kukabidhi funguo kwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao maeneo ya michenzani na kujengwa nyumba za kisasa zenye horofa tano.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,akizungumza na wananchi wakati sherehe za Kukabidhi funguo za nyumba mpya zilizojengwa na Serikali, kwa watu waliovunjiwa nyumba zao Eneo la Michenzani na kujengwa nyumba za kisasa





Wazee waliovunjiwa nyumba zao wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la nyumba za horofa zilizojengwa michenzani Block no 10,bwana Seif Juma (kushoto) na Bwana Said Rajab kwa niaba ya Hashim Abdalla Baharan,wakisubiri kukabidhiwa funguo za nyumba ambazo watalipwa kutokana na kuvunjiwa na kupata nyumba za kisasa.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akimkabidhi funguo za Nyumba mpya za Michenzani Bw Sef Juma,katika miongoni mwa watu waliovunjiwa nyumba zao,katika eneo hilo la Michenzani Mjini Unguja na kujengwa nyumba za kisasa.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akimkabidhi funguo za Nyumba mpya za Michenzani Bw Sef Juma,katika miongoni mwa watu waliovunjiwa nyumba zao,katika eneo hilo la Michenzani Mjini Unguja na kujengwa nyumba za kisasa.





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akimkabidhi funguo za Nyumba mpya za Michenzani Bw Said Rajab kwa niaba ya Hashim Abdalla Bahran,katika miongoni mwa watu waliovunjiwa nyumba zao,katika eneo hilo la Michenzani Mjini Unguja na kujengwa nyumba za kisasa.

Picha na Ramadhan Othman Ikulu.



Read more...

Wanahabari Morogoro wasaidia harambee ya Kilosa


Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akipokea msaada wa nguoazi kutoka kwa wawakilishi wa waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro hivi karibuni wilayani Kilosa. Wanahabari waliotoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za wadau mbalimbali za kuwasaidia waathirika wa mafuriko ya Kilosa ambao bado wanaishi katika Kambi baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Kilosa

Read more...

JK katika sherehe za kumuenzi Mzee Karume


Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo jana mjini Zanzibar.

vijana wananchama wa UVCCM wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa kilele cha maandamano yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mjini Zanzibar kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume.


Rais Jakaya mrisho Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar(kulia) na Mwenyekiti wa jumuiya ya umojawa Vijana wa CCM Bwana Yusuf Masauni wakati wa mapokezi ya maandamano ya umoja wa vijana wa CCM mjini Zanzibar jana jioni.


vijana wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM, UVCCM wakipita mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maandamano ya kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abedi amani Karume yaliyofanyika katika viwanja vya CCm Maisara, Zanzibar jana jioni.



Mwenyekiti wa UVCCM Yusuf Masauni akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya CCM Maisara mjini Zanzibar jana jioni ambapo aliyapokea maandamano ya vijana na kuwahutubia. Leo ni Siku rasmi ya Karume na ni mapumziko nchi nzima



Read more...

NHIF yawapiga somo wachora katuni na wapiga picha

Wachora katuni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya semina iliyowashirikisha Wapiga picha na Wachora Katuni iliyoandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na kufanyika katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu jijini Dar jana.
Mkurugenzi wa Uanachama na Uendeshaji wa mfuko wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wachora katuni na wapiga picha, iliyofanyika Dar es Salaam, jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba.
Washiriki wa semina ya Mfuko wa Bima ya Afya wakimsikiliza mtoa mada, Rehani Athumani (hayupo pichani) wakati wa semina iliyowashirikisha wachoraji katuni na wapiga picha kwenye ukumbi wa baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam
Wapiga picha katika picha ya pamoja baada ya semina elekezi ya NHIF

Read more...

CENTURY CINEMAX CINEMA-MLIMANI CITY and NEW WORLD CINEMA-MWENGE

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP