Thursday, November 19, 2009
Vodacom Tanzania yamwaga 25m/- Zenji kwa Mapinduzi Cup
UNFPA
Same
Lugha Gongana
Wednesday, November 18, 2009
Busara 2010
Mtanange wa saba wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 11 hadi 16 Februari 2010; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya saa kumi na moja.Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.Hatimaye Kombe la Dunia kutinga Tanzania
Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa juu ya maandalizi ya ujio wa kombe la Dunia linalotarajiwa kuwasili kesho na kuzinduliwa kesho hiyohiyo na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete saa kumi jioni, ambapo pia mashabiki mbalimbali watapata fursa ya kupiga nalo picha kwa kumbukumbu kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika nchi nyingine.Serengeti yamwaga mamilioni kwa Kisura wa Tanzania

Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akikabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi Milioni 35 kwa meneja mradi wa Kisura wa Tanzania Grace Kilembe huku kisura wa Tanzania 2008 Emmy Nelau na Meneja mkuu wa Serengeti Winston Kagusa waliosimama katikati wakishuhudia tukio hilo lililofanyika kiwandani hapo, aliyesimama kushoto ni Brand Manager wa Kampuni hiyo Nandi Mwiyombela, shindano la kisura wa Tanzania linatarajiwa kufanyika Disemba mosi mwaka huu kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar se salaam.
Mchuma wa Fiesta
Meneja Matukio na Promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh naye alipata nafasi ya kuweka saini katika gari hilo.
Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akiweka saini kwenye gari aina ya Mitsubishi pajero linalotarajiwa kutolewa kwa mshindi wa bahati nasibu mashabiki wa Fiesta One Love itakayofanyika sambamba na tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya posta Kijitonyama, mashabiki watapata nafasi ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo kutokana na tiketi zao walizokata ili kuingia kwenye tamasha hilo ambapo wasanii mbalimbali watatoa burudani kutoka hapa nchini na nje ya nchi akiwemo mkali wa Hiphop kutoka nchini Marekani
Busta Rymes, kweli hii ni Fiesta one Love
Mh. Burian na ujumbe wa EU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Batilda Burian akizungumza na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya{EU} kulia kwa Waziri ni Balozi wa Sweden Bw Staffan Herrstrom na Balozi wa Jumui ya Ulaya Bw Tim Clarke uliomtembelea na Kumweleza msimamo wao Kuhusu Mabadiliko wa Tabianchi kuelekea Mkutano wa Denmmark. Picha na Ali Meja
Mh. Sitta amtembelea Dk. Migiro New York
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe.Samuel Sitta akisalimiana na Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha - Rose Migiro alipomtembelea ofisini kwake, makao makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani leo. Spika yupo Jijini New York kuhudhuria Mkutano wa pili wa kamati ya maandali ya mkutano wa Maspika wa Mabunge Duniani utakaofanyika Julai 2010 huko Geneva. Chini wakiwa na Afisa habari wa Bunge Owen Mwandumbya wa Bunge.Rukwa na Matukio.
Picha na Rukwa Peti Siyame
Mama Kikwete katika ziara ya Manyoni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari Itigi msaada wa magodoro 20 kwa ajili ya hosteli ya wanafunzi wasichana wa shule hiyo.
(Picha na Juma Kengele - Ikulu)
Monday, November 16, 2009
TBC SPORTS CLUB WAPEWA JEZI
Youssou Nd'our atembelea Clouds Fm
Washindi wa chemsha bongo wazawadiwa
Mama Kikwete katika ziara ya Bahi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Dodoma mjini kuhusu kujitokeza kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amevaa vazi la asili la kabila la wagogo mara baada ya kuvalishwa na wakazi wa kijiji cha Mdemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.
Mke wa Rais Mwalimu Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisahihisha daftari la Lea Wimbe ambaye ni mlemavu wa kusikia mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya viziwi Kigwe. Mama Kikwete alitembelea shuleni hapo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma
Picha na Juma Kengele - Ikulu
Makamanda wa CCM
Wednesday, November 4, 2009
Jose Mara azaliwa Novemba 2
MBIO MAALUM ZA KUKIMBIZA BENDERA YA TAIFA ZAENDELEA.
Mwanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Pius Sulle akikimbia mbio maalumu za kukimbiza bendera ya taifa kwa kupokezana kutoka Chalinze hadi Segera baada ya kupokea bendera hiyo kutoka kwa wenzao wa Dar es Salaam, juzi. kabla ya kuhitimisha mbio hizo siku ya ijumaa kwa kuipandisha katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro. Mbio hizo za kampeni ya ‘Fikisha Tanzania katika hatua za juu’ zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro





