Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, February 18, 2010

Waziri Kawambwa ndani JNIA

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Prosper Tesha(kulia) akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kwenye chumba cha kuongozea Ndege kwa Waziri wa Miundombinu Dkt Shukuru Kawambwa (kushoto) jinsi ya uongozaji wa Ndege za ndani na njea ya Nchi zinatua katika Uwanja wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Waziri Kawambwa alitembea uwanja huo jana kuangalia shughuli mbali za maboresho ya uwanja huo zinazoendelea.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Prosper Tesha(wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kwa Waziri wa Miundombinu Dkt Shukuru Kawambwa (kushoto) kazi ya uboreshaji wa Uwanja wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zinazoendelea. Waziri Kawambwa alitembea uwanja huo kuangalia shughuli mbali za maboresho ya uwanja huo zinazoendelea
(Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO)

Read more...

Ukarabati waanza ofisi ya SA, Sofia House

Ofisi za Uwakala wa Tiketi wa shirika la ndege la Afrika Kusuni ambazo zilishika moto hivi karibuni katika jengo la Sophia mtaa wa Maktaba na Bibi Titi limeanza kufanyiwa ukarabati na siku si nyingi watarejea katika huduma kama kawaida.

Read more...

Ali Kiba in Coventry live on February 19, 2010


Read more...

Wanaopenda kucharge simu huku ikiwa Kitandani, habari ndiyo hii!!

Jamaa kaungua vibaya kutokana na mambo ya kuchaji simu huku akiendelea na mambo yake kitandani





Haya ndiyo mambo ya simu kuchagi ukiwa umeiweka kitandani




Read more...

Wednesday, February 17, 2010

Mkullo atembelea Moscow


Waziri wa Fedha Mh. Mustafa Mkullo (katikati waliokaa) akiwa na baadhi ya Watanzania waishio na wanaosoma vyuo vikuu mbalimbali Russia waliofurika kumlaki katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Moscow Capt. mstaafu Balozi Jaka Mwambi.. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi na kushoto ni Mke wa Balozi wa Tanzania Urusi


Waziri wa Fedha Mh. Mustafa Mkullo akijibu swali kutoka kwa Watanzia waliofurika kumlaki katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Moscow Capt. mstaafu Balozi Jaka Mwambi. Kuumeni ni mke wa Mh. Mwambi

Read more...

Wadau walamba milioni za tigo bwerere leo


Meneja wa promosheni wa Tigo Redemptus Masanja (shoto) akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja Bw. Imani Kayange wa Kiwalani Rumo kama zawadi yake ya Tigo Bwerere leo jijini Dar, huku meneja uhusiano Jackson Mmbando akipiga chabo katikati.

Read more...

KCB yasaidia vifaa Buguruni leo

Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KBC na mbunge wa kuteuliwa Janet Mbene(kushoto)akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha Afya Buguruni Mwajuma Mbaga(kulia) vifaa vya kupimia magonjwa mbalimbali Utra sound printer,dottla machine na oxygen concentrator vifaa hivyo vina thamani ya Sh Milioni 4.3.wa pili kushoto Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Joram Kiarie,Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnyamani Jabir Abbas,Diwani wa kata ya Buguruni Magina Lufunondo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Afya cha Buguruni mara baada ya benki hiyo kufika hapo kutoa msaada vya kupimia magonjwa mbalimbali Utra sound printer,dottla machine na oxygen concentrator vifaa hivyo vina thamani ya Sh Milioni 4.3

Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KBC na mbunge wa kuteuliwa Janet Mbene akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kupimia magonjwa mbalimbali Utra sound printer,dottla machine na oxygen concentrator vifaa hivyo vina thamani ya Sh Milioni 4.3,katika kituo cha Afya cha Buguruni jijini Dare s Salaam.Kutoka kushoto Mkuu wa Masoko wa benki hiyo Christina Manyenye,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Joram Kiarie na kulia Diwani wa kata ya Buguruni Magina Lufunondo.

Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KBC na mbunge wa kuteuliwa Janet Mbene(kushoto)akimkabidhi Diwani wa kata ya Buguruni Magina Lufunondo (kulia) vifaa vya kupimia magonjwa mbalimbali Utra sound printer,dottla machine na oxygen concentrator vifaa hivyo vina thamani ya Sh Milioni 4.3.Wakati benki hiyo ilipoenda kutoa msaada huo katika kituo cha Afya cha Buguruni jijini Dare s Salaam.

Read more...

MZUNGU KICHAA ALIZIMA TAMASHA LA BUSARA KWA MBWEMBWE



Mzungu Kichaa pia ni fundi wa kuling'uta gitaa la sollo na mwanamuziki wa kigeni anayekiwakilisha vyema kiswahili kutokana na jinsi anavyoimba , hapa anaonekana kufanya mambo makubwa wakati wa maonyesho ya mwishoni mwa tamasha hili la busara lililomalizika jana Mjini Zanzibar na ametokea kupendwa na watu wengi katika tamasha hilo kutokana na kuimba kiswahili kwa ufasaha na kuwakuna zaidi mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo wakati mwingine unapomuona akiimba huwezi amini kama jamaa ni mzungu, Mzungu Kichaa ni mmoja wa wasanii wakubwa hapa asili yake ni kutoka Nchini Denmark lakini maisha yake yote amekulia hapa Tanzania

Read more...

UBALOZI WA UFARANSA WAWAPIGA JEKI WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA


Baadhi ya wafanyakazi wa chama cha msalaba mwekundu wakiwasubiri wageni katika ofisi zao zilizoko Masaki jijini Dar es salaam.



Balozi wa Ufaransa Nchini Bw. Jacques Champagne de Labriolle (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali katibu mkuu wa chama cha msalaba mwekundu na Meya wa jiji la Dar es salaam Adam Kimbisa, vifaa hivyo vimenunuliwa na ubalozi huo kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, na ni mahema, Vyandarua, vyombo vya kupikia kwa ajili ya familia ambazo hazina nyumba madawa ya kusafishia maji ya kunywa na usambazaji wa maji safi vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 94 za kitanzania, hafla hiyo imefanyika katika ofisi za msalaba mwekundu zilizopo Msaki jijini Dar es salaam.

Read more...

NAPOLI:MISS & MISTER VALETINE 2010

pichani Mr Bonny Milinga akimkabidhi tuzo Mister Valentine 2010 Napoli Italy Mr Salim Mapoz,pembeni ni mmoja wa wasimamizi wa tukio zima ndugu Allan Bendera.


pichani Miss Valentine Bi Aziza Tesa akiwa na Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania Italy Mh Abdulrahaman A.Alli pamoja na mjumbe wa jumuiya ndugu A.Bendera.

Miss Aziza Tesa ndie miss valentine 2010 Napoli

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za valentine mjiniNapoli.katika sherehe hizo mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wale wote waliohudhuria na wote walioshiriki katika kufanikisha sherehe za siku ya wapendanao, mwenyekiti aliwapongeza miss & mister valentine 2010 na kuwataka wawe mabalozi wa jumuiya na kuhimiza umoja baina ya watanzania.Picha zaidi tembelea WABONGO UGHAIBUNI.

Read more...

ALI KIBA IS IN THE BUILDING ' LIVE IN MANCHESTER '




After huge success of Kenya / Tanzania Independence in manchester last year & Swagger like us Bongo UK in Birmingham and many more,we thought is that time of the new year,to spice it up and wat a way to experience a ONE NIGHT STAND with the man himself ...ALI KIBA on Saturday 20th Feb will be performing live his best tracks & Classics like Cindrella,naksh mrembo, mac muga,usiniseme,karimu & many more..as well on the night there will be an after party were drinks and vibes will be flowing,sexy pipo with our finest Dj'sDj D MAK - Dj SKIP - HANNIE G ... on rotation playing best inR n B ! Afro beatz ! Genge ! Bongo Flava ! Hip Hop ! Kwaito ! Funky Houze and many more.——————————————Mahali Food Catering Services will provide fantastic African Food for reasonable prices all night.► Nyama Choma ( Mbuzi )► Fried Chicken► Chapati► Vitumbua► Kachumbari ( African Salad )► PilipiliThis mouth watering food will satisfy those tastebuds and leave you wanting more.......hence the option of takeaways will also be there !!!!———————————► Dresscode:- sexy,suave or sophisticated & stylish
( absolutely no hoodies or caps )► ENTRANCE:- £10 B4 MID,£15 AFTER.►info: HOTLINE NUMBER ★☆ 07988356791 ★☆VENUE : THE METHODIST CHURCH, CENTRALL HALLMANCHESTER,OLDHAM STREET M1 1JQ

Read more...

Tuesday, February 16, 2010

Mzee Mkapa afunika Iringa

"Japo nilikataza wanafunzi kuja kunipokea ila basi ngoja nicheze nao wananipenda sana"Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa akicheza na wanafunzi wa shule ya msingi Ilula ambao walishindwa kuvumilia madarasani na kutoka kumpokea kiongozi huyo kipenzi cha watanzania



Maofisa wa taasisi ya Mkapa wakimsikiliza kwa makini Mkapa wakati akieleza sababu ya kutojitokeza mara kwa mara katika vyombo vya habari kwa madai ya kutingwa na majukumu ya kimataifa na kitaifa juu ya UKIMWI.


Rais (mstaafu) wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa akisalimiana na wagonjwa katika hospitali teule ya wilaya ya Kilolo (Ilula ) leo asubuhi ,Mkapa yupo mkoani Iringa na wilaya ya Kilolo yatoa taarifa tata kuhusu hali ya migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo



Watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkapa leo. Picha zote na Francis Godwin wa Iringa




Read more...

Ally Rhemtulla na Zain wazindua mfuko wa kuchangia elimu wilaya Kisarawe

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Khanifa Karamagi (wa kwanza kutoka kushoto) akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe.

Bango linalomuonyesha Ally Rhemtullah ambaye ameamua kujiunga katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe kwa njia ya kufanya Fashion Show aliyoipatia jina la 'Fashion For Education Benefit'.

Mbunifu wa Mitindo, Ally Rehmtullah (pili kutoka kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe. Wa kwanza kulia ni Prof. Emmanuel Bavu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Harambee Kisarawe, Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Khanifa Karamagi pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza. Ufunguzi wa Kampeni hiyo umefanyikia katika hoteli ya Double Tree iliyoko Masaki jijini Dar mapema leo asubuhi.
Mwaka 2008 Wialaya ya Kisarawe ilikuwa na Shule za kata 11, ikilinganishwa na shule 6 zilizokuwapo mwaka 2006. Hata hivyo pamoja na ongezeko hilo shule 11 zilidhihirika kuwa na mapungufu kama ifuatavyo:-
1. Uhaba wa madarasa.
2. Uhaba wa nyumba za walimu na chache zilizopo kutokufikia viwango stahiki.
3. Kutokuwepo mifumo ya maji na umeme.
4. Shule zote kutokuwa na maabara.
5. Wanafunzi kutembea umabli mrefu kutoka majumbani kwao au kulazimika kupanga katika nyumba za jamii inayozunguka shule kwa kuwa hakuna hosteli mashuleni.
Mapungufu yote yaliyoorodheshwa pamoja na mengine yalithibitika kurudisha nyuma juhudi za kuimarisha elimu na maendeleo ya wilaya kwa ujumla.
Ili kuepuka hali hiyo, mapema mwaka 2008 uongozi wa wilaya uliona umuhimu wa kuhakikisha wilaya inazindua na kubuni mpango mkakati wa kushirikisha wilaya inazinduka na kubuni mpango mkakati wa kushirikisha wananchi wa Kisarawe walio ndani na nje ya wilaya, marafiki na wadau mbali mbali kuchanga kwa hali na mali ili kuboresha miundo mbinu katika shule zote za kata na kujenga chuo kimoja cha ufundi.
Mpaka sasa jumla ya michango yote ni Tsh. 29, 285,200/= ahadi ni
Tsh. 25, 174,500/= na USD 50,000/= pamoja na eneo la ekari 98 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi lililotolewa na mwananchi mmoja wa Wiraya ya Kisarawe.
Kwa wale wateja wa mtandao wa Zain jinsi ya kuchangia 'Unatuma ujumbe mfupi wenye neno ELIMU kwenda namba 15620 ambapo kampeni hii itaanza rasmi 1st March 2010 na kila SMS utakayotuma utakatwa shilingi 250/=. Pia kwa wale wanaotumia huduma ya ZAP wanaweza kuchangia kwa kutumia hiyo namba ila kima cha chini ni shilingi 1000/=






Read more...

JUMLA YA MILIONI 22 ZATENGWA KWA ZAWADI KILIMANJARO MARATHON

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (shati la mistari) akifafanua masuala mbalimbali kwa wandishi wa habari jijini leo kuhusu mbio za nyika za 2010 ambazo zitafanyika mwisho wa mwezi wa Februari 2010 mkoani Kilimanjaro. mwigine ni Meneja ya Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania(RT) Suleiman Nyambui (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini leo kuhusu wakimbiaji wa mbio za nyika za Kilimanjaro 2010 ambazo zitafanyika mwisho wa mwezi huu Mkoani Kilimanjaro(kulia) ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.Mbio hizo za nyika zimedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Vodacom Tanazania pamoja na makampuni mengine nchini ikiwemo kampuni ya KK Security,Tanga Cement. Good Year, Kilimanjaro Water,Tanzanite One, DT Dobie Tanzania, TPC, New Africa Hotel na Keys Hotel, jumla ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa na wanariadha mabimbali wanaotarajiwa kushiriki katika mbio hizo . Picha na Mwanakombo Jumaa.-Maelezo

Read more...

Unajua hukumu ya "Sharia" inavyotekelezwa?















Hizo ndizo hatu kwa hatua katika utekelezaji wa hukumu ya sharia.

Read more...

Kalunde Band yasherehekea miaka minne ya kuzaliwa kwake siku ya wapendanao

Bosi wa Kalunde Band akiongea usiku wa kuamkia jana katike sherehe za kutimiza miaka minne ya kundi hilo linalokuja juu kwa kasi kwenye ukumbi wa Rainbow Mbezi beach jijini Dar. Kalunde band ilizaliwa siku ya wapendanao miaka minne ilopita kwa kufanya shoo yake ya kwanza Giraffe hotel jijini

Fabak Fashion walikuwepo kuonesha mavazi


Deo Mwanambilimbi (kati) akiongoza kikosi kizima cha Kalunde Band kusherehekea kwa mpigo siku ya wapendanao pamoja na hepi besdei ya nne ya kuzaliwa bendi hio ukumbi wa Rainbow Club Mbezi Beach jijini Dar

Read more...

MACHOZI BAND YAWAPAGAWISHA WAPENDANAO ARABELA

Lady Jay Dee na Gadner wa pili kutoka kulia wakijichanganya na mashabiki wao yote hii ni katika kuonyesha upendo kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wao.


Hapa ilikuwa ni kushangweka kwa kwenda mbele kama unavyowaona wapenzi wa bendi ya machozi wakiserebuka vya kutosha stejini kwenye klabu ya Arabela usiku wa Valentine
Mwanamuziki wa bendi ya Machozi Mwinyi Machozi kulia akiongoza wenzake wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho la kukata na shoka kwenye ukumbi wa Arabela



Lady Jay Dee aka Binti Komadoo akifanya vitu vyake jukwaani wakati bendi yake ya machozi ilipofanya onyesho la wapendanao kwenye klabu ya Arabela usiku wa Valentine, kushoto ni mwimbaji mahiri wa bendi hiyo Jonico Flower, usiku huo ulikuwa bomba na watu walionekana kuwa na furaha huku wakinywa, wakicheza muziki na kufurahia maisha na wenza wao ama ndugu zao wawapendao


Read more...

Ufunguzi wa kikao cha halmshauri kuu ya Taifa kinachoendelea mjini Dodoma

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wapili kushoto) na viongozi waandamizi wa CCM kutoka kushoto Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba na Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha halmshauri kuu ya Taifa kinachoendelea mjinji Dodoma


Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta akijadiliana jambo na mjumbe mwezake Abdulrahman Kinana mjini Dodoma JANA asubuhi wakati wa kikao cha halshauri hiyo kinachoendelea
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta akijadiliana jambo na mjumbe mwezake Abdulrahman Kinana mjini Dodoma jana asubuhi wakati wa kikao cha halshauri hiyo kinachoendelea.Picha kwa hisani ya Freddy Maro


Read more...

ALI KIBA LIVE IN BRISTOL FROM 10.30 TO DAWN


For tickets Call: 07786047228 (Cardiff) and Rest of UK 07969122807, 07818246540, 07969899287Be there or be square!!!

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP