Ndugu jamaa na marafiki wa waliokuwa watuhumiwa wa mauaji ya wafanyabiashara watatu kutoka mkoani Morogoro wakishangilia mara baada ya ndugu zao kuachiwa huru katika mahakama kuum ya Tanzania jijini Dar.

Abdalla Zombe akiingia kwenye Gari tayari kurudi nyumbani mara baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na wenzake 9 ambao walikuwa waktuhumiwa kwa kesi ya kuwauwa wafanyabiashara watatu kutoka mkoani morogoro, Jaji Salum Masati aliyekuwa akisoma hukumu hiyo iliyochukua takriban masaa saba na zaidi katika kuhitimisha hukumu hiyo, amesema watuhumiwa hawana hatia kwakuwa serikali imeshindwa kuthibitishia mahakama juu ya tuhuma zilizokuwa zikiwakabili washitakiwa hivyo mahakama inawaachia huru watuhumiwa wote wako huru kuanzia sasa

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es salaam Abdallah Zombe akisindikizwa na makachero mara baada ya kuachiwa huru na mahakama kuu ya Tanzania baada ya kutopatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na wenzake 9

Umati ulizidi kuongezeka hadi lango kuu kujaa

Watu wakishangilia baada ya huku kutolewa na Zombe na wenzake kuachiwa huru
0 comments:
Post a Comment