Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha maombolezo jana, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Anita Ngowi aliyefariki juzi nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Walter Ngowi mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Anita Ngowi aliyefariki juzi nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam baada ya kuuguwa ugonjwa wa Saratani , mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa jana alasiri katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein akimfariji Clifford Ngowi mtoto wa marehemu Anita Ngowi

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Miriam Ngowi ambaye pia ni mtoto wa marehemu

Mke wa Makamu wa Rais, Mwanamwema Shein akitia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais marehemu Anita Ngowi.
0 comments:
Post a Comment