Mabalozi wa Zambia na korea ya Kusini wawasilisha hati za utambulisho
JK akipokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wawili wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania. Pichani akipokea hati toka kwa Mhe. Darius Steinbeck Bubala wa Zambia.
JK akipokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wawili wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania. Pichani akipokea hati toka kwa Mhe. Darius Steinbeck Bubala wa Zambia.

wasani wa tasnia ya filamu na muziki walikusanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Msasani, Dar, na kufanya usafi kuadhimisha miaka 10 ya kifo chake. Shughuli hii iliratibiwa na African Stars Entertainment, wamiliki wa bendi ya Twanga Pepeta, chini ya Mkurugenzi wake Da'Asha Baraka akisaidiana na Mamaa Dotnata, pamoja na kikosi kizima cha twanga pepeta na mastaa kibao wa filamu. Shughuli ilifana sana Mjukuu wa Mwalimu, Fortunata Nyerere, aliwashukuru wasanii hao kwa niaba ya familia
baadhi ya wasanii hao wakipozi baada ya kazi
Mama Maria Nyerere akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi mara baada ya mwege huo kuwasili nyumbani kwake kijijini Butiama wilayani Musoma katika mkoa wa Mara kwa ajili ya kuuwasha mwenge wa Mwitongo. Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha. Mwenge huo unatarajiwa kuzimwa kesho kijijini Butiama huku siku hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kufa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Butiama wakiangalia albamu zenye picha za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere walipotembelea banda la Idara ya Habari (Maelezo) wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana Tanzania yanayofanyika katika kijiji hicho. Maonyesho hayo yanakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere na kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru yatakayofanyika jumatano wiki hii.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Mwanamuziki wa kikazi kipya anayekuja juu nchini Tanzania Shaa akisalimiana na wapenzi wa muziki alipokuwa kwenye tuzo za MTV Music Award Nairobi Kenya mwishoni mwa wiki.Sha alikua mmoja ya wanamziki aliechaguliwa kushinda tuzo hiyo amabpo Dibanj kutoka Nigeria aliibuka mshindi.
Mwanamuziki wa kikazi kipya anayekuja juu nchini Tanzania Shaa akisalimiana na wapenzi wa muziki alipokuwa kwenye tuzo za MTV Music Award Nairobi Kenya mwishoni mwa wiki.Sha alikua mmoja ya wanamziki aliechaguliwa kushinda tuzo hiyo amabpo Dibanj kutoka Nigeria aliibuka mshindi JK akiteta jambo na Meneja wa TANESCO kanda ya Ziwa Bwana Makala Kingu muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa umeme katika kijiji cha Kisamwene, kata ya Butuguri wilaya ya Musoma vijijini jana jioni
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa Elimu kwa Watoto wa Kike ulioanzishwa na Gavana wa Benki Kuu (Mwalimu Nyerere Memorial Scholarship Fund) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2009. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndullu.

Baadhi ya Kinamama wenye nyumba eneo la Kipawa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiomba dua kupinga kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya zamani na kutaka itumike sheria ya sasa kwani gharama za vifaa vya ujenzi zimepanda.Wenye nyumba hao walitakiwa kuhama eneo hilo mwaka 1997 Aprili,Jana walikutana kwa nia ya kutafuta taratibu za kisheria kuhusiana na suala hilo.
Baadhi ya Kinababa wenye nyumba eneo la Kipawa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiomba dua kupinga kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya zamani na kutaka itumike sheria ya sasa kwani gharama za vifaa vya ujenzi zimepanda.Wenye nyumba hao walitakiwa kuhama eneo hilo mwaka 1997 Aprili,Jana walikutana kwa nia ya kutafuta taratibu za kisheria kuhusiana na suala hilo.
Wakazi wa jiji la Mwanza wakila shangwe la ukweli la fiesta one love 2009 ndani ya ccm kirumba


The U.S President Barack Obama (pictured) is the 2009 Nobel Peace Prize winner for "his extraordinary efforts to strengthen international diplomacy and cooperation between peoples."
He has got this Prize for giving the world citizens a hope for the better future.
Obama was elected as the first African-American president of the United States of America in November 2008.
The Norwegian Nobel Committee said it attached special importance to Obama's vision of and work for a world without nuclear weapons.
"Obama has as president created a new climate in international politics.
Multilateral diplomacy has regained a central position, with emphasis on the role that the United Nations and other international institutions can play," the committee said on its website.
"Only very rarely has a person, to the same extent as Obama, captured the world's attention and given its people hope for a better future.
His diplomacy is founded in the concept that those who are to lead the world must do so on the basis of values and attitudes that are shared by the majority of the world's population," the committee said.
There were a record 205 nominations for the 2009 peace prize, of which 33 were organizations.
Last year, former Finnish President Martti Ahtisaari won the peace prize for his mediation efforts.
The peace prize was the fifth of this year's Nobel awards, which are also made for medicine, physics, chemistry and literature.
The prizes were endowed by Swedish industrialist Alfred Nobel, the inventor of dynamite.The Nobel Peace Prize - worth 10 million kronor ($1.4 million dollars) - is scheduled to be presented in Oslo Dec 10.
Ilikuwa ni MTV Pre_party ya kujiandaa na the Big Day, wadau mbalimbali kutoka sehemu tofauti za Afrika walitia timu ndani ya Ice Blue Club jijini Nairobi na kujiachia kwa sana, wabongo kama kawa walikuwepo kumsapoti AY na Shaa na hivi ndivyo walivyouza sura
Prof Jay na msanii mwenzie wa Kenya
Meneja Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya 'Win With Zap' iliyozinduliwa jana na kampuni hiyo ya simu kwenye makao makuu yake Sayansi Kijitonyama, Win with zap itawafanya wateja wa Zain kujishindia zawadi mbalimbali za muda wa maongezi katika simu zao mara watakapokuwa wakiongeza salio kwenye simu zao, katika picha wanaofuata ni Meneja Masoko Costantine Magavilla na Deogratius Tarimo meneja wa Zap.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya Tigo Lotto Imaculata Anna Sanga mkazi wa Tegeta Dar es Salaam akionyesha zawadi yake fedha taslimu shs milioni moja muda mfupi baada yha kukabidhiwa katika ofisi za Tigo jijini Dar jana.
Daktari wa Rais Jakaya Kikwete, Dkt. Peter Mfisi, akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam jana, kufafanua masuala muhimu ya afya ya Rais kufuatia tukio la kuishiwa nguvu wakati akishiriki katika sherehe za miaka 100 ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mkoani Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu.
© Dullonet template by Dullonet.com 2009
Back to TOP