JK ndani ya Musoma
JK akiteta jambo na Meneja wa TANESCO kanda ya Ziwa Bwana Makala Kingu muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa umeme katika kijiji cha Kisamwene, kata ya Butuguri wilaya ya Musoma vijijini jana jioni
JK akibonyeza kitufe wakati akizindua mradi wa umeme katika kijiji cha Kisamwene kata ya Butuguri,wilaya ya Musoma vijijijni jana jioni
JK akiongea na mwanafunzi Ezekiel James wakati alipokagua darasa la mfano muda mfupi baada ya kufungua shule ya Sekondari ya Chifu Oswald Mang’ombe jana jioni wilaya ya Musoma vijijini.
Mwanafunzi Godbless Buluhya wa shule mpya ya sekondari ya Chifu Oswald Man’gombe iliyopo musoma vijijini akifanya jaribio la kisayansi wakati JK alipokagua maabara ya shule hiyo jana jioni.Wengine katika kutoka kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mstaafu Enos Mfuru(wapili kushoto) na wanne kulia ni Mbunge wa Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono.
Mama Maria Nyerere akimkaribisha JK muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Musoma jana jioni. JK yupo mkoani Mara kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo pamoja na shughuli nyingine atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge siku ya Jumatano ambayo pia itakuwa ni kuadhimisha siku ya Nyerere.
0 comments:
Post a Comment