Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, March 29, 2010

Simba na mikakati mbadala

Mwenyekiti wa Mabingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania 2010/2011 Simba Sports Club Mzee Hassan Dalali akifungua tawi la Simba linalojulikana kama "Simba Ng'ata" huko Kurasini Mivinjeni Wilayani Temeke jijini Dar es salaam jana jioni huku wanachama wa tawi hilo wakiangalia, wanachama na mashabiki wa Simba wameliita tawi hilo la simba jina la Simba Ng'ata kutokana na timu ya Simba kufanya mambo makubwa katika msimu huu wa ligi hasa baada ya kutofungwa mchezo hata mmoja mpaka wanatangaza ubingwa.

Wageni mbalimbali wakiwa wamekaa wakati wa uzinduzi wa tawi la SIMBA NG'ATA. Tawi hilo lilifunguliwa rasmi naMwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali aliyefuatana na Mweka hazina msaidizi wa SSC bwana Chano. , aliyekaa katikati ya Chano na Dalali ni Mwenyekiti wa muda wa tawi hilo anayejulikana kwa jina la Moloto, na kushoto kwa Dalali ni Hamisi Jabu baba yake mzazi na mchezaji wa SSC Juma Jabu.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP