Wednesday, October 7, 2009
Tuesday, October 6, 2009
Pinda alipoingia Muhimbili
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mkurugezi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Bakari Shaaban ambaye amelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Oktoba 3, 2009. Kulia ni Mke wa Meja Jenerali Shaaban, Zaina Said.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye amelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam kwa matibabu, October 3, 2009.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Pinda atembelea Banda la Tanzania Geneva
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akipiga simu wakati Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Peter Masika (kulia) akimweleza kuhusu mawasiliano ya elimu ya ugonjwa wa ukimwi kwa njia ya simu yanavyofanywa na taasisi hiyo. Pinda alitembelea banda la taasisi hiyo kwenye maonesho yanayokwenda sambamba na Mkutano Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la kimataifa (ITU) mjini Geneva, Uswisi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Exim Bank ilvyoshiriki katika kuchangia Rotary Dar
Wafanyakazi Wa banki ya Exim wakisaidia kugawa maji kwa baadhi ya washiriki wa matembezi ya hisani ya Dar Rotary Walk ‘09 yaliyoandaliwa na Rotary Club ya Dar es Salaam. ili kupata fedha kwa ajili ya kampeni ya kupanda miti zaidi 100,000 nchini kote. Exim ilikuwa moja ya wadhamini wa matembezi hayo.
Mama Salma Kikwete naye ajiandikisha
Mke wa Rais, Salma Kikwete akijindikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 25 mwakahuu. Alijiandikisha leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge kilivhopo mtaa wa Kivukoni Dar es Salaam.
Mama Salma Kikwete naye ajiandikisha
Mke wa Rais, Salma Kikwete akijindikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 25 mwakahuu. Alijiandikisha leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge kilivhopo mtaa wa Kivukoni Dar es Salaam.
CCM Youth Commander
JK ajiandikisha
Akiondoka baada ya kujiandisha. JK aliwahimiza wananchi kutumia haki yako ya kujiandikisha ili wapige kura kuwachagua viongozi wa serikali zao za Mtaa "Hawa ndio viongozi wenu wa kutatua shida na kero mbalimbali kwa ngazi ya mitaa yenu...maji taka mtaani, ugomvi usiku na mchana..." alisema Kikwete.
Monday, October 5, 2009
Tanzania yanga'ra maonesho ya Mkutano wa Telecom World 2009
Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame akitembelea banda la Tanzania Geneva leo
maandalizi na ufunguzi wa Mkutano wa Telecom World 2009uliofunguliwa na katibu mkuu wa UN leo mjinbi Geneva. Huu ni sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano
Sophia Simba patron for Tanzania Women of Achievement Awards
Frontline Management Team,with Patron Mama Sophia Simba and Sponsors for the Women Of achievement Awards
Hon. Sophia Simba, Minister of State in the President’s office(Good Governance) and chairperson for Umoja Wa Wanawake Tanzania (UWT), is the official patron for Tanzania Women of Achievement Awards.
The awards were launched by a local PR company Frontline Management at the beginning of September with the objectives to empower and inspire women through recognition of the most exceptional and achieving women in the country who have not only achieved success in their own respective fields but have made a significant difference in their communities and society as a whole.
The judging panel is made up of a committee of 6 outstanding Tanzanians including
*Dr. Chijoriga -Dean, University of Dar es Salaam business school,Dr. Ramadhan Dau - Executive Director NSSF, *Mrs. Mary Rusimbi - Founder and former Executive Director for Tanzania Gender Networking Programme,*Sadaka Gandi- Counseling Psychologist,
*Ms.Joaquine De Mello - Commissioner for the Commission for Human rights and Good Governance (CHRAGGR),*Innocent Mungi- TCRA Public Relations and Communication Director*Irene Kiwia - MD Frontline Management.
The categories for the awards include – Arts and Culture, Information & Communication; Public Sector; Young Achiever; Business Entrepreneur; Education; Health; Science & Technology; Social Welfare; Agriculture, and Sports.
This project has received enormous support from organizations ranging from Private, Public, Governmental and NGO’s Like; VODACOMFOUNDATION,BARRICKTANZANIA,SONGASTANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA),TWIGA CEMENT,TANZANIA BREWERIES LIMITED (TBL),UNESCO,MULTICHOICE TANZANIA,NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC),AFRICAN LIFE ASSURANCEFARM EQUIP (QUALITY GROUP).
The category winners and overall winner will be announced during a gala that will take place at the end of November 2009 at the Mlimani City Hall where the winners will receive cash money prize, trophy and certificate.
The nomination forms can be obtained at all sponsor’s offices across the country or online at http://www.frontline.co.tz/ or call 0614 105 186 or email http://uk.mc332.mail.yahoo.com/mc/compose?to=info@frontline.co.tzDeadline for receiving nominee forms is first week of November.
ABOUT FRONTLINE MANAGEMENT:Frontline Management Ltd. (FML) is a full service public relations, event management company based in Dar es Salaam, Tanzania.
We specialize in corporate communication at all levels, from media management, corporate social responsibility, public relations campaigns, corporate events, TV and radio production and brand awareness
WACHEZA FILAMU CHIPUKIZI KUSAKWA TANZANIA
Uibuaji na ukuzaji wa vipaji vya wasanii chipukizi wa filamu ambao hawajawahi kushiriki katika filamu au tamthilia yoyote itawahusisha watanzania wenye vigezo vya kuwa na umri wa miaka 16 na kuendelea, awe na akili timamu, awe ni raia wa Tanzania na ajue kusoma na kuandika.
Mchakato utahusisha kufanya usaili katika mikoa husika hadi watakapopatikana kumi bora ambapo washiriki watachuana kumtafuta msanii chipukizi wa filamu Tanzania.
Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa hapo baadaye Mshindi wa IBUA Film Star Tanzania atajinyakulia zawadi ambayo itatangazwa baadae na pia atapata mkataba wa kushiriki filamu mbali mbali za wasanii wa ndani na nje ya nchi.
Mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kupitia kipindi maalumu kitakachoonyeshwa hapo baadae.
Fomu za kushiriki shindano la IBUA Film Stars Tanzania zinapatikana mikoa husika kama ifuatavyo Arusha (Club Silk), Mwanza (Salma Cone), Mbeya (CPMTL Stationery mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa), Dodoma (Zunny Ice Cream Parlour), Zanzibar (Ofisi za Zenj FM), Dar es Salaam (TCC Chang’ombe, Shear Illusions mlimani City, Royal Salon Sinza, Zizzou Fashions).
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30 Oktoba 2009 kabla ya kuanza usaili mjini Arusha tarehe 31 Oktoba na 01 Novemba.
Zoezi la usaili litafanyika kabla ya wananchi kupata nafasi ya kutoa maoni na kufanikisha kuwapata washindi.
Jacqueline Wolper
Afisa Uhusiano-YEC PRODUCTION
Mashindano ya uvuvi ya Vodacom yafana
Mkuu wa Yacht Club Comodere Spiros (kushoto) akimkabidhi kikombe cha ushinda wa uvuvi wa kutumia boti Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Kisiwa cha Sinda katika Bahari ya Hindi jumla ya nchi Nne zilishiriki Mashindano hayo,mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wenzake waliposhiriki katika mashindano ya kuvua samaki
Watoto wakiwashangaa samaki waliovuliwa jinsi walivyokuwa wakubwa.
Samaki mkubwa aina ya Papa mwenye kilo 157 aliyekuwa mkubwa zaidi baada ya kuvuliwa na Len Botha wa Afrika Kusini katika shindano la Maboti ya kuvua samaki akipimwa kwenye muzani katika kisiwa cha Sinda, shindano hilo lilizishirikisha Nchi Nne yakiwa yamedhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mwishoni mwa wiki.
JK ahudhuria sherehe za miaka 100 ya African Inland Church Mwanza
JK akisalimianan na baadhi ya Maaskofu wa kanisa la African Inland Church Tanzania(AICT) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Kirumba, jijini Mwanza jana, ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini Tanzania.
akihutubia wanachi walishiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza jana asubuhi
vodacom miss TZ 2009 wapokea zawadi zao
Mshindi wa nne wa Vodacom Miss Tanzania 2009, Sylivia Shally akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 3 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Group (Vodacom Group Chief Officer of Corporate Affairs, Bob Collymore ikiwa ni moja ya zawadi kwa kutwaa ushindi huo wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe.
Mshindi wa tatu wa Vodacom Miss Tanzania 2009, Julieth William akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 4 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Group (Vodacom Group Chief Officer of Corporate Affairs, Bob Collymore ikiwa ni moja ya zawadi kwa kutwaa ushindi huo wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,
Mshindi wa pili wa Vodacom Miss Tanzania 2009, Beatrice Lukindo akitabasamu baada ya kupokea mfano wa hundi ya shs milioni 6.2 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Group (Vodacom Group Chief Officer of Corporate Affairs, Bob Collymore ikiwa ni moja ya zawadi kwa kutwaa ushindi huo wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar
Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 9 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Group (Vodacom Group Chief Officer of Corporate Affairs, Bob Collymore ikiwa ni moja ya zawadi kwa kutwaa ushindi huo wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe, jijini Dar usiku kuamkia jana. Zawadi za fedha za washindi wa shindano hilo zitaingizwa katika akaunti zao zilizofunguliwa katika benki ya Kenya Commercial Bank.
Friday, October 2, 2009
TAMASHA LA 28 LA SANAA BAGAMOYO LAENDELEA
kundi la Splendid Theatre likifanya vitu vyake wakati wa tamasha la Bagamoyo la 28 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania akiwa na wasanii wanaoratibiwa na Kampuni Ukala ya Dar usiku wa kuamkia jana. Tamasha hilo la kila mwaka hufanyika Chuo Cha Sanaa Bagamoyo na ni mojawapo ya vivutio vikubwa katika kalenda ya utalii ya mji huo mkongwe. Na safari hii linafanyika katika ukumbi uliokrabatiwa na kujengwa upya wa chuo hicho
SERA YA MAJI YAJADILIWA NA WADAU WA MAJI NA TAASISI ZAKE
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Marck Mwandosya akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kufungua warsha ya Mkakati wa pamoja wa kuangalia upya sera ya maji iliyoanza jana katika jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es alaam, Warsha hiyo inashirikisha wadau mbalimbali wa maji na Taasisi zake na itaendelea mpaka leo.
Thursday, October 1, 2009
Mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Arusha wafana vilivyo

Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Dk William Shija (shoto mbele) akipozi na kamati ya wabunge wanawake wa chama katika hoteli ya Arusha Corridor
Mh. Hubert Kim E. Swan ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani katika bunge la Bermuda ni kivutio cha aina yake kwa jinsi anavyopiga pamba katika mkutano huu
Wah. wakiserebuka katika hafla ya kuwakaribisha iliyoandaliwa hoteli ya Kibo Palace usiku kuamkia jana
Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola na Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Mh. Samwel Sitta (kulia) akipozi na Spika wa Bunge la India Mh. Meira Kumar (kati) na Balozi wa India nchini wakati wa hafla aliyowaandalia wabunge 800 toka mataifa 53 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika hoteli ya Kibo Palace usiku wa kuamkia jana ikiwa ni sherehe ya kuwakaribisha wah. hao wanaohudhuria mkutano wa 55 wa chama hicho. mwakani mkutano huo unatarajiwa kufanyika KenyaMaandamano ya CUF katika Picha
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akimsikiliza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa aliyepokea maandamano yao katika Uwanja wa Kidongo Chekundu.
Baadhi ya mabango ambayo yalikuwa na jumbe tata kutoka kwa wafuasi wa chama cha wananchi CUF





