
Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Dk William Shija (shoto mbele) akipozi na kamati ya wabunge wanawake wa chama katika hoteli ya Arusha Corridor

Mh. Hubert Kim E. Swan ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani katika bunge la Bermuda ni kivutio cha aina yake kwa jinsi anavyopiga pamba katika mkutano huu

Wah. wakiserebuka katika hafla ya kuwakaribisha iliyoandaliwa hoteli ya Kibo Palace usiku kuamkia jana

Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola na Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Mh. Samwel Sitta (kulia) akipozi na Spika wa Bunge la India Mh. Meira Kumar (kati) na Balozi wa India nchini wakati wa hafla aliyowaandalia wabunge 800 toka mataifa 53 wanachama wa Jumuiya ya Madola katika hoteli ya Kibo Palace usiku wa kuamkia jana ikiwa ni sherehe ya kuwakaribisha wah. hao wanaohudhuria mkutano wa 55 wa chama hicho. mwakani mkutano huo unatarajiwa kufanyika Kenya
0 comments:
Post a Comment