TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA UTALII NCHINI ITALY

Ambapo kwa mara nyingine Tanzania imeshiriki kwenye maonyesho ya Utalii nchini Italy yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Maonyesho yalifanyika katika jiji la Milan Italy kuanzia tarehe 18 Feb mpaka 21 Feb 2010.
Msafara wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Ezekieli Maige. Jumla ya makampuni binafsi 6, Tanapa na Ngorongoro walihudhuria maonyesho haya. Nchi ya Italy ni ya tatu katika kuleta watalii wengi wanaotenbelea nchini Tanzania na wataliano wengi hupenda kutembelea Zanzibar, Mafia, na kwenye Mbuga za Wanyama.
Hivi sasa Tanzania kupitia Bodi yake ya Utalii TTB na Wizara ya Maliasili na Utalii na Balozi mbalimbali za Tanzania iko kwenye mkakati mkubwa wa kuutangaza utalii wake katika mataifa mbalimbali ili kuweza kuongeza kiwango cha watalii kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania na imekuwa ikishiriki katika maonyesho mbalimbali ya Utalii ya kimataifa yanayofanyika Ulaya na MarekaniTanzania inaweza kufanikiwa zaidi iwapo itajiimarisha zaidi katika sekta ya Utalii kwani ni moja ya nchi zenye vivutio vingi na vilivyoorodheshwa katika maajabu saba ya Dunia, hivyo ni jukumu la watanzania pamoja na Taasisi zote zinazohusika na utalii kusimamia vyema na kuutangaza utalii wa Tanzania ili uweze kuingiza pato kubwa la fedha za kigeni na kukuza uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment