Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, May 3, 2010

Hamis Hamad Mnondwa kumvaa Kigoda


Kijana Hamis Hamad Mnondwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya nia yake ya kumvaa mbuge Abdallah Kigoda wa Handeni ili kuchukua jimbo na kuanza kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Amesema wananchi wa Handeni hawahitaji kutawaliwa ila wanahitaji kuongozwa kwa kushauriana katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo ambao liko nyuma sana kiuchumi, kielimu na kiafya pia, ameongeza kuwa yuko tayari kwa kuwatumikia wananchi wa Handeni kinachotakiwa ni wao kumuidhinisha ili aweze kuwatumikia.

Amesema utaratibu uliotangaza na chama cha mapinduzi unasema fomu zitaanza kutolewa kwa wagombea tarehe 26 mwezi julai na kurudishwa tarehe 28 mwezi huohuo, Hamis Hamad Mnondwa aliongozana na baba yake mzazi katika mkutano huo anayejulikana kwa jina la Njama Issa Mnondwa aliyeko kulia.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP