Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, May 3, 2010

MKUTANO WA INVESTIMENT CLIMATE SUMMIT WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Wiliam Mkapa katikati akisalimiana na ris Mstaafu wa Botswana Festus Mogaye huku Ofisa Mtendaji mkuu wa ICF Issa Omary akisikiliza kabla ya uzinduzi rasmi wa mkutano unaoja uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika Afrika.

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Juma Mwapachu kushoto akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan wakati walipokuwa wakitoka nje mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo.


Balozi wa Rwanda nchini Tanzania mama Fatma Ndagiza akitaniana na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Juma Mwapachu mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Afrika ulioanza leo kwenye hoteli ya Dubble Three Hilton jijini Dar es salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa ICF Issa Omary akimuongoza Rais Mstaafu wa Botswana Festus Mogaye kuingia kwenye chumba cha mkutano wakati wa uzinduzi wa mkutano unaojadili uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Afrika
Ofisa Mtendaji Mkuu wa The Investiment Climate Facility For Africa (ICF) Bw. Issa Omary akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali yatakayozungumzwa katika mkutano wa uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Kiafrika hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo mkutano huo uliozinduliwa leo kwenye hoteli ya Dobble Three Hilton na utachukua siku mbili kabla ya ule wa World Economic Forum unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City hapa jijini Dar es salaam na kubudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi za kiafrika na wataalam wa masuala ya uchumi.
Issa Omary amesema Kutatua matatizo ya uwekezajio katika Tanzania na nchi zingine za kiafrika na kuboresha wa huduma mbalimbali za kibiashara inawezekana tena kwa gharama ndogo sana kitu muhimu ni serikali husika kukaa na wadau mbalimbali na wafanyabiashara ili kupata msukumo wa pamoja katika kurekebisha kasoro mbalimbali zinazokabili huduma sekta mbalimbali za kibiashara
Ametolea mfano kuwa kwa nchi ya Rwanda ambayo kampuni zilikuwa zikisajiriwa kwa muda wa siku 30 lakini kwa sasa kampuni inasajiriwa kwa siku moja na gharama imeshuka kutoka dola 400 za kimarekani mpaka dola 45 jambo ambalo Rais Paul kagame mwenyewe alilisimamia na hatimaye wamefanikiwa.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP