Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, September 30, 2009

Dr. Shein Mvomero


Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein,akifunua pazia kuweka jiwe la msingi majengo ya Shule ya Sekondari Wami katika kijiji cha Dakawa Wilayani Mvomero Morogoro jana,Dk.Shein amechangia shilingi milioni tatu katika ujenzi huo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Issa Machibya.Picha na Amour Nassor

Read more...

Discussing...

Prime Minister Mizengo Pinda chatting with the Minister for Livestock Development and Fishery,Mr John Magufuli at a meeting discussing livestock development in the country,held in Dodoma held yesterday.Photo by Prime Minister Office

Read more...

MWANAMITINDO FATMA AMOUR KUZINDUA "MAGIC OF TANZANIA" NCHINI MAREKANI

Mkuu wa kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Marekani aliyekaa kulia Karen Grisette akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ubalozi huo leo wakati alipowatangaza Wanawake watanzania 13 wanaotarajia kwenda nchini humo kwa mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa kwa mwezi mmoja, hili ni kundi la tatu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo hayo makundi mengine mawili yameshakwenda na kupata mafunzo na wamerejea nchini.
Karen amesema wasanii hao kutoka mikoa ya Tanga, Zanzibar Bagamoyo Dar es salaam Arusha na Dodoma watashiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
Ameongeza kuwa mafunzo yataanza tarehe 6 oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, ameongeza kuwa wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs ambaye ataongoza wenzake 12 katika safari hiyo anatarajiwa kuzindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi utakaofanyika jimbo la Ohio tarehe 12 oktoba, pia atatambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine nchini Marekani.Fatma Amour akitoa shukurani zake kwa Ubalozi wa Marekani kwa kumchagua kwenda katika mafunzo hayo yatakayochukua mwezi mmoja nchini Marekani.

kutoka kushoto ni Fatma amour,Zena Abdallah,Amoke Kyando aliyerejea kutoka katika mafunzo hayoSalma Masenga, Harieth Kagangule, Mwandale mwanyekwa (Big Mama) na Scolastca Malecela wakiwa katika picha ya pamoja

Read more...

Wanafunzi wa Kibasila

Read more...

Mama Kikwete Twiga sekondari.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua Maabara ya Komputa katika shule ya Sekondari ya Twiga wakati wa mahafali ya kwanza shuleni hapo juzi.

Mama Salma Kikwete akihutubia wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya kwanza ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Twiga
iliyopo Tegeta Dar es Salaam

Read more...

Tuesday, September 29, 2009

Ajinyakulia Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu


Mratibu wa Gofu wa kampuni ya Illovo Ltd, Pieter Van Eeeden (kulia) akimkabidhi mcheza gofu, thian Myburgh (kulia) Simu mpya aina ya Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu yaliyofanyika wiki iliopita katika uwanja wa gofu wa Illovo, Kilombero Mkoani Morogoro. Mashindanon hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Zain na kukutanisha wacheza golf mbalimbali wa mkoa wa Morogoro.

Read more...

Mambo ya uzinduzi wa michuano ya Netiboli

Katibu mkuu msaidizi wa CHANETA Rose Mkisi kushoto na Mweka hazina wa chama hicho Flora Kasambara wakiingia katika viwanja vya mashindano kabla ya kufunguliwa rasmi na mke wa rais Mama Salma Kikwete jana


Mke wa Rais Mama Salama Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya netball kwenye uwanja mkuu wa Taifa jana akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho ambapo Tanzania ilishinda magoli 33-19 mashindano hayo ya kimataifa ya Netball yanasimamiwa shirikisho la vyama vya Netball vya kimatifa International Federation of Netball Association (IFNA)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati alipofungua mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yanayofanyika nchini yakiandaliwa na chama cha Netball CHANETA yaliyoanza jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa. kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na anayefuata ni Anna Bayi Mwenyekiti wa Chama cha hicho.


Kuazia kushoto ni Timu za Tanzania, Namibia na Afrika kusini zikiwa zimekaa tayari kwa kupigiwa nyimbo za mataifa yao wakati wa ufunguzi wa mashindano ya NetBall kwa nchi za Afrika jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa.

Mchezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Queen akijaribu kufunga goli katikati ya walinzi wawili wa timu ya Lesotho wakati wa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Mchezo wa Netball kati ya timu hizo iliyofanyika jana kwenye uwanja mkuu wa taifa Tanznia ilishinda magoli 33-19.

Read more...

JK afungua jengo la ubalozi wetu Washington DC


Jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani ambalo JK alilifungua jana asubuhi. Jengo hili limenunuliwa na serikali ya Tanzania kwa jumla ya dola za kimarekani $10,415,000.


JK akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani jana asubuhiJK akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijinji Washington Marekani jana asubuhi.
JK akisalimiana na wageni mbalimbali na mabalozi waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani zilizofanyika jana asubuhi
JK akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Balozi iliyopo katika jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani jana asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na wapili kushoto ni Balozi wa Tanzania Washington Ombeni Sefue


Picha na Freddy Maro wa Ikulu

Read more...

Barack Obama and First Lady Michelle Obama With World Leaders at the Metropolitan Museum in New York

President Barack Obama and First Lady Michelle Obama pose for a photo during a reception at the Metropolitan Museum in New York with H.E. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Deputy Secretary-General of the United Nations, Wednesday, Sept. 23, 2009. (Official White House Photo by Lawrence Jackson)


President Barack Obama and First Lady Michelle Obama pose for a photo during a reception at the Metropolitan Museum in New York with H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, Wednesday, Sept. 23, 2009. (Official White House Photo by Lawrence Jackson)

Read more...

Mavazi ya Netball yanatofauti gani na yale ya Mamiss?
Read more...

Vyoo vya kikohozi.

Ukitaka kujua kama kuna mtu anatumika humu ndani basi we kohoa tu na utapata majibu, lakini hii ni maalum kwa wliopitia mazingira kama haya.

Read more...

Viongozi wetu wametokea huku lakini leo hii ni mafisadi wakubwa na wanasahau walikotoka na waliowaacha nyuma yao.


Hili ni taifa la kesho, je na hawa watakuja kuwa mafisadi wakubwa katika nchi hii hapo baadae?

Read more...

Maria Nyerere azungumza na waandishi


Mjane wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere (Mama wa Taifa) akizungumza na waandishi nyumbani kwake Msasani Dar es Salaam jana, kuhusiana na tuzo aliyoipokea Mapema mwezi huu kutoka kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa inayotambua Mchango wa baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika.

Read more...

Haya ndiyo ya mjini kila mtu kivyake!!


Read more...

Kwanza Jamii mtaani

Read more...

Monday, September 28, 2009

Wanafunzi Kibasila Sekondari wafunga BarabaraWANAFUNZI wa shule ya sekondari kibasila na shule ya msingi kibasila leo walikua na mgomo kutokana na eneo hilo kuwa na ajali za mara kwa mara kusababisha vifo kwa wanafunzi wa shule hizo.
Tukio hilo lililotokea leo asubuhi ambapo wanafunzi wawili wa shule ya msingi kibasila waligongwa na mwananchi mmoja ambaye alikua akiwavusha barabara kugongwa na hali yake sio nzuri na yuko hospitali ya temeke kwa matibabu zaidi.Kwamujibu wa mashuuda wa tukio hilo walisema kuwa wanafunzi waliogongwa ni Consolatha Kilasa ,Wiliston Sango wote wa darasa la 5 waliokuwa wakitoka nyumbani kuelekea shuleni ata hivyo jina la msamaria mwema halikupatikana.
Akiongea na gazeti hili mmoja wa walimu alisema kuwa mwanafunzi mmoja aliyejulikana kwa jina Wiliston Sango yupo hospitali ya mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi kutokana na kujeruhiwa vibaya.
Pia katika tukio hilo wanafunzi waliweza kuzuia baadhi ya magari yasipite katika eneo hilo likiwamo gari la jeshi lenye namba za usajili 2813 JW97 Defender na gari la polisi PT-0176.
Makamu mkuu wa shule ya kibasila mwalimu Catherine Urio alito wito na kuomba wakala wa barabara kuweka matuta,taa,alama za pundamilia na askari wa kuongozea magari kwani kutokuwepo kwa vitu hivyo kunasababisha ajali nyingi na watu upoteza maisha kwa wingi.
Hatahivyo wanafunzi walisema kuwa hawataki kusikia siasa zinatendeka wanachotaka wao matuta yawekwe na taa pia trafiki awepo katika barabara hiyo ya changombe.
Wakati huo huo mwenyekiti wa serikali za mitaa Sophia Kinega alisema ni halali kwa wanafunzi kufanya mgomo huo kwani ajali nyingi zinatokea na kuua wanafunzi mara kwa mara kwani wanafunzi hao wanaona uchungu kuona wenzao wakipoteza maisha.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jordan Lugimbano aliwataka wanafunzi aongee nao ila wanafunzi hao walionekana wakimzomea,baada ya muda wanafunzi walikubali na kwenda kuongea nae iliwaweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Read more...

Rais Kikwete akutana na Ban-ki-Moon New York

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika mkutano na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-ki Moon na ujumbe wake katika ofisi yake iliyopo ndani makao makuu ya Umoja wa Mataifa(UN) jijini New York mapema jana asubuhi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban-ki Moon katika makao ya Umoja wa Mataifa jijijni New York Marekani mapema jana (photo by Freddy Maro)

Read more...

Afunga Ndoa na Wanawake Wanne Kwa Mpigo


Mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini ambaye ana mke na watoto 11 amejipatia umaarufu wa ghafla duniani baada ya kufunga ndoa na wanawake wanne kwa mpigo.Bwana harusi Milton Mbhele aliwasili kwenye harusi yake jumamosi akiwa kwenye gari jeupe aina ya limousine akiwa pamoja na mabibi harusi wake wanne.Mabibi harusi wote wanne walivalishwa pete za ndoa na kupigwa busu la nguvu na bwana harusi Mbhele katika harusi kubwa ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na mamia ya watu.Sheria za Afrika Kusini zinaruhusu ndoa za wake wengi hata rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ana wake watatu. Utamaduni wa wake wengi ni wa kawaida katika makabila ya Zulu na Swazi.Hata hivyo ni mara chache sana hutokea mwanaume akafunga ndoa na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Read more...

Miss Utalii Temeke 2009- Erica Allan (kati), wa pili Mariam Khamis(kushoto) na 3-Zainabu Matagi-


Mbunge wa Temeke ,Abbas Mtemvu & Mariam Mtemvu, wakishuhudia fainali za shindano la Miss Utalii Temeke 2009, City Garden usiku wa kuamkia jumamosi

Mh Mtevu akimvisha taji Miss Utalii Temeke 2009- erica Allan mara baada ya kuibuka kinara wa mashindano hayo.

Read more...

Saturday, September 26, 2009

JK Na Kamaresh New York


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bwana Kamaresh Sharma jijini New York .Rais Kikwete yupo jijini New York Marekani ambapo anahudhuria Mkutano Mkuu Baraza la Umoja wa Mataifa(Picha: Freddy Maro)

Read more...

JK na Ray chambers wa mumbe maalum wa malaria


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Malaria Bwana Ray Chambers mara baada ya kufanya mazungumzo jijini New York Marekani .

Read more...

Ajali zaingine jamani!!!


Dereva wa lori akitafakari jinsi ya kumuingia mdosi wake mara baada ya kupata ajari ya kuifumua vilivyo daladala.

Read more...

TBL yaipiga jeki kamati ya usalama barabarani

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar leo, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu akibandika stika kwenye gari Dar yenye maneno yanayotahadharisha madereva kutoendesha magari huku wakiwa wamelewa. Stika hiyo ni moja kati ya 4000 zilzotolewa msaada na TBL kwa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama . Pia TBL ilitoa msaada wa fulana 800 kwa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe,

Read more...

Friday, September 25, 2009

Sura ya Biashara hiyoooooooooo!


Read more...

BASKETBALL CHARITY DAY

Jaji Mkuu wa Tanzania na Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini TBF Jaji Augustino Ramadhan akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo asubuhi wakati alipotangaza maandalizi ya bonaza la mpira wa kikapu lililopewa jina la "BASKETBALL CHARITY DAY" litakalofanyika kuanzia oktoba 17 mpaka 22 na kuhitimishwa tarehe 24 kwa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa viwanja zaidi ya vitano nchini kote huku mgeni rasmi akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete, jumla ya shiligi milioni 10 zinatarajiwa kukusanywa katika Harambee hiyo , wanaofuata katika pisha ni Lawrence Cheyo Katibu mkuu wa TBF na Saimon Msofe Mwenyekiti wa caha cha Basketball jijini Dar es salaam (DABA). Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF Lawrence Cheyo akimkaribisha Mlezi wa shirikisho hilo Jaji mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhan wa pili kutoka kulia wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar, anayefuatia ni Eke Mwaipopo mchezaji wa zamani mpira wa kikapu na mwenyekiti wa kamati ya tamasha la kikapu linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Read more...

JAPAN YATOA BILIONI 2.4 KUSAIDIA MPANGO WA KUDHIBITI UKIMWI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akibadilishana hati na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa jijini leo kuhusu msaada wa fedha wenye thamani ya bilioni 2.4 za kitanzania kwaajili kununulia madawa na vitendea kazi muhimu katika mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi.( 2.4 billion for procerement of equipment, medicines and services necessary for implementing the HIV/AIDS Control programme mara baada ya kusaini hati hizo hafla ya kusaini hati hizo imefanyika katika Wizara ya Fedha na Uchumi.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo).

Read more...

Miss Tanzania ndani ya Vodashop


Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania leo mchana huu wametembelea duka la Vodashop lililopo mtaa wa Samora karibu na Idara ya Habari Maelezo na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika duka hilo, kama unavyoona mmoja wa wafanyakazi wa vodacom katika duka hilo Jannet Massanja aliyesimama katikati akitoa maelezo kwa warembo hao na kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na warmbo hao shindano la Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika wiki ijayo oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es salaam.

Read more...

USAID YAMWAGA VIFAA VYA KUPIMIA KIFUA KIKUU

Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni akiangalia kifaa cha kupimia ugonjwa ya kifua kikuu (Microscope) iliyokabidhiwa kwake na Elise Jensen (wa kwanza kulia) mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani (USAID) huku maofisa wa Wizara na shirika la USAID wakishuhudia, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Wizara ya Afya. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Microscope 40, Jokofu moja na microscopy slide boxes 1600 vyote vikiwa na thamani ya dola za Kimarekani 109,715 na vitagawanywa katika mikoa yote nchini.

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP