Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, May 3, 2010

Spika afungua Mkutano wa wadau wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini.

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akifungua rasmi kongamano la mwaka la wadau wa kuzuia na kupambana na Rushwa lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa nchini (PCCB). Kongamano hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Blue pearl, Ubungo Plaza Dar e es salaam ambapo Spika alikuwa mgeni rasmi. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye kongamano hilo wakimsikiliza Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta.



Mgeni rasmi katika kongamano la wadau wa Kuzui na Kupambana na Rushwa nchini , Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Kongamano hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Blue pearl, Ubungo Plaza Dar e es salaam.. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Read more...

Biashara Barabarani.


Kutokana na wajasiriamali wengi hapa nchini kukosa mbinu na maarifa ya kutafuta masoko ya nje ya bidhaa zao, wengi wao wamekuwa wakiuza bidhaa hizo kiholela kama inavyoonekana pichani wajasiriamali hawa katika mji mdogo wa Chalinze wakitafuta wanunuzi kwenye mabasi mwishoni mwa wiki.Picha na Fadhili Akida

Read more...

Maandalizi ya Taifa Cup, Morogoro wapigwa tafu.


Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Mkoa wa Morogoro Haidhuru Ngakoka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Said Mwambungu (kushoto) fedha taslimu shilingi Milioni 1,500,000/= katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, kama mchango wa kampuni hiyo kwa timu ya Moro stars, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Taifa Cup 2010.

Timu hiyo inatarajia kuondoka leo (kesho) kwenda Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuanza mechi yake ya kwanza dhidi ya timu ya Mkoa huo. Ili kuweza kufanikisha maandalizi ya timu hiyo kiasi cha shilingi milioni nane kinahitika, wadau wa soka Mkoani hapa wameombwa kuchangia ili kuweza kufanikisha ushindi wa timu hiyo. Picha na Father Kidevu

Read more...

MKUTANO WA INVESTIMENT CLIMATE SUMMIT WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Wiliam Mkapa katikati akisalimiana na ris Mstaafu wa Botswana Festus Mogaye huku Ofisa Mtendaji mkuu wa ICF Issa Omary akisikiliza kabla ya uzinduzi rasmi wa mkutano unaoja uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika Afrika.

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Juma Mwapachu kushoto akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan wakati walipokuwa wakitoka nje mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo.


Balozi wa Rwanda nchini Tanzania mama Fatma Ndagiza akitaniana na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Juma Mwapachu mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Afrika ulioanza leo kwenye hoteli ya Dubble Three Hilton jijini Dar es salaam.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa ICF Issa Omary akimuongoza Rais Mstaafu wa Botswana Festus Mogaye kuingia kwenye chumba cha mkutano wakati wa uzinduzi wa mkutano unaojadili uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Afrika




Ofisa Mtendaji Mkuu wa The Investiment Climate Facility For Africa (ICF) Bw. Issa Omary akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali yatakayozungumzwa katika mkutano wa uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji katika nchi za Kiafrika hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo mkutano huo uliozinduliwa leo kwenye hoteli ya Dobble Three Hilton na utachukua siku mbili kabla ya ule wa World Economic Forum unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City hapa jijini Dar es salaam na kubudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi za kiafrika na wataalam wa masuala ya uchumi.
Issa Omary amesema Kutatua matatizo ya uwekezajio katika Tanzania na nchi zingine za kiafrika na kuboresha wa huduma mbalimbali za kibiashara inawezekana tena kwa gharama ndogo sana kitu muhimu ni serikali husika kukaa na wadau mbalimbali na wafanyabiashara ili kupata msukumo wa pamoja katika kurekebisha kasoro mbalimbali zinazokabili huduma sekta mbalimbali za kibiashara
Ametolea mfano kuwa kwa nchi ya Rwanda ambayo kampuni zilikuwa zikisajiriwa kwa muda wa siku 30 lakini kwa sasa kampuni inasajiriwa kwa siku moja na gharama imeshuka kutoka dola 400 za kimarekani mpaka dola 45 jambo ambalo Rais Paul kagame mwenyewe alilisimamia na hatimaye wamefanikiwa.





Read more...

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ali Sheni chapisho la (UN-HABITAT)

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ali Sheni akifungua wa mkutano wa siku moja jana jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Karimjee wenye lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya uimarishaji na uendelezaji wa wa Jiji la Dar es salaam jiji hilo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja unaozungumzia uimarishaji na uendelezaji wa wa Jiji la Dar es salaam wakimsikiliza jana jijini humo Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ali Sheni wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.


Read more...

President Kikwete opens 2nd TICAD Ministerial meeting in Arusha.

President Jakaya Mrisho Kikwete and Japanese Minister for Foreign Affairs Katsuya Okada arrives at Arusha International Conference Centre for the opening ceremony of the 2nd TICAD Ministerial meeting yesterday morning(photos by Freddy Maro)

Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe(centre) introduces to President Jakaya Kikwete Japan Minister for Foreign Affairs Katsuya Okada shorly after the President arrived at Arusha International Conference Centre(AICC) to open the second TICAD Ministerial Follow up meeting yesterday morning.















President Jakaya Kikwete delivers his opening speech during the 2nd TICAD Ministerial Follow meeting at AICC in Arusha yesterday morning.




Read more...

Hamis Hamad Mnondwa kumvaa Kigoda


Kijana Hamis Hamad Mnondwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya nia yake ya kumvaa mbuge Abdallah Kigoda wa Handeni ili kuchukua jimbo na kuanza kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Amesema wananchi wa Handeni hawahitaji kutawaliwa ila wanahitaji kuongozwa kwa kushauriana katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo ambao liko nyuma sana kiuchumi, kielimu na kiafya pia, ameongeza kuwa yuko tayari kwa kuwatumikia wananchi wa Handeni kinachotakiwa ni wao kumuidhinisha ili aweze kuwatumikia.

Amesema utaratibu uliotangaza na chama cha mapinduzi unasema fomu zitaanza kutolewa kwa wagombea tarehe 26 mwezi julai na kurudishwa tarehe 28 mwezi huohuo, Hamis Hamad Mnondwa aliongozana na baba yake mzazi katika mkutano huo anayejulikana kwa jina la Njama Issa Mnondwa aliyeko kulia.

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP