Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, July 29, 2009

mkutano mkuu wa CCM Reading UK

Takribani wanachama 500 wa CCM Nchini Uingereza wahudhuria Mkutano Mkuu wa Tawi jijini Reading UK uliofunguliwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mhazini Mkuu wa CCM Taifa Mhe.Amos G. Makalla.
Pamoja naye toka Tanzania ni Mshauri Mkuu wa Siasa wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Rajabu Luhwavi. Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee aliwakilisha Taarifa ya maendeleo ya CCM UK na Mwenyekiti wa CCM UK Nd. Maina Owino alimkaribisha Mhe. Amos Makalla kufungua rasmi Mkutano huo Mkuu.
Mhe. Makalla alisema kazi ya ujenzi wa Chama na Taifa la Tanzania ni letu wote na lazima wote kwa usawa bila ubaguzi tuvune matunda ya Uhuru wetu Viongozi hao wa kitaifa waliwataka Watanzania kuongeza juhudi za makusudi kuitangaza Tanzania kwa mema na pia Kutosita kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali ili kuboresha utawala bora na maadili mema ya uwajibikaji.
Aidha wote wamewataka Watanzania wanaoishi Ughaibuni wasikae kimya na watoe taarifa katika vyombo husika pale wanapo ona hawajatendewa haki kwa mujibu wa sheria za Tanzania mara warudipo nyumbani. Watanzania wengi walihamasika na kuendelea kujiunga na CCM siku hiyo ya Jumapili 26/07/2009.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP