Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, November 16, 2009

Mama Kikwete katika ziara ya Bahi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpima uzito mtoto Jonathani Deogratus mwenye umri wa miezi kumi ambaye alipatikana na uzito wa kilo 11.5 huku mama wa mtoto huo Rosemary Deogratus akimsaidia kuweka kwenye mzani wakati alipotembelea kituo cha afya Kigwe kilichopo wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Dodoma mjini kuhusu kujitokeza kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa kijiji cha Kigwe juu ya kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa maralia wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo katika wilaya ya Bhi mkoani Dodoma kwa ajili ya kuwapatia msaada wa vifaa mbalimbali vya afya.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amevaa vazi la asili la kabila la wagogo mara baada ya kuvalishwa na wakazi wa kijiji cha Mdemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.



Mke wa Rais Mwalimu Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisahihisha daftari la Lea Wimbe ambaye ni mlemavu wa kusikia mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya viziwi Kigwe. Mama Kikwete alitembelea shuleni hapo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma

Picha na Juma Kengele - Ikulu

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP