Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, November 4, 2009

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwa amesimama mbele ya gari lake aina ya Suzuki Vitara Grand mara baada ya kukabidhiwa jana mchana kwenye duka la Vodashop mtaa wa Ohio.

Miriam Gerald akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC1 Evance Mhando mara baada ya kukabidhiwa gari lake jana mchana

Meneja mkuu wa Makampuni ya Shivacom Parthiban C. wa pili kutoka kulia na Meneja wa udhamini na mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za Gari aina ya Suzuki Grand Vitara Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald katika duka la kampuni hiyo lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam, Gari hilo jipya lina thamani ya shilingi milioni 53 na litamsaidia mrembo huyo katika kazi zake mbalimbali za kijamii Miriam Gerald alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar es salaam na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP