Wednesday, December 30, 2009
Waandishi ndani ya TBL
Meneja wa Upikaji Bia wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL),Dar es Salaam, Kalvin Nkya (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, nchini, jinsi bia inavyochachushwa, walipotembelea kiwanda hicho, jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Maneno Mbegu.
MAANDALIZI YA KUPOKEA WAGENI WORLD CUP 2010 HAPA NCHINI YANAKWENDA VYEMA- DR.KAWAMBWA
Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Rodger Tenga amesema tayari wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini, na amezitaja nchini hizo kuwa ni Ujerumani, Italia,DenmarkNew Zealand, Brazil,Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.
Dr. Kawambwa amesema jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni hiyo ikiwa ni mambo ya matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni wengine baadhi ya mambo wakati watakapokuwa hapa nchini, mpaka sasa televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.
Ameongeza kwamba kwa upande wa Timu ya Ivory Coast itawasili hapa nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo, waliopo kwenye picha kutoka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu
Wednesday, December 23, 2009
Vodacom yakabidhi vifaa kwa ajili ya kombe la Mapinduzi Cup
aibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna (kushoto)akikabidhi vifaa vya michezo kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa timu ya Simba Mohamed Kajole mara baada ya kukabidhiwa na Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi (katikati)Maneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Atilio Lupala
Naibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna na Katibu Mkuu wa ZFA wilaya ya mjini Nassor Salumu(kushoto)wakionyesha jezi baada ya kukabidhiwa na wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi Vodacom Tanzania
Richard Mwaikenda apongezwa na Jambo Concepts kwa tuzo ya mpiga picha bora 2009
Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambole, Richard Mwaikenda akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto), zawadi na tuzo alizotunukiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), baada ya kuibuka Mpigapicha Bora 2009.
Rais Karume afungua mkutano wa Redet
Baadhi wa washiriki wa Mkutano wa siku mbili kuhusu Hali ya siasa Zanzibar unaoendelea katika ukumbi wa Salama Bwawani,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume alipoufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiufungua Mkutano wa kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar,katika ukumbi wa Salama Bwawani,ulioandaliwa na Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Karume Atembelea kituo cha kupokea umeme Fumba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya Umeme Kutoka Afrika Kusini Martin Burls,wa kampuni ya EHT,(aliyenyoosha mkono),wakati alipotembelea Kituo cha kupokea Umeme Funga kuona matatizo yaliyosababish kukosekana kwa Nishati hiyo takriban wiki tatu sasa.
Tuesday, December 22, 2009
Waisrael Wavumbua Nyumba Aliyoishi Bwana Yesu
Mabaki ya nyumba inayoaminika aliishi bwana Yesu iliyopo huko Nazareth.
Read more...Monday, December 21, 2009
Uzio wa hoteli aliyofungua JK juzi A-Taun wapigwa nyundo
Jiwe la kutengenezea chuma
Fundraising Ya ATWID Reading
Mgeni Rasmi Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh Chabaka Faraji Kilumanga
Pia alikuwepo Mbunge wa viti maalum Martha Mlata Kulikuwepo na ngoma za asili zilizochezwa na wana ATWID pamoja na shoo ya watoto.Mwenyekiti wa ATWID Susan Mzee alitoa nasaha zake na kuwashukuru wote waliohudhuria kwa muda wao na michango yao.Zaidi ya paundi elfu mbili(£2000)zilipatikana katika hafla hiyo kwa ajili ya kutunisha mfuko wa ATWID.Asante sana
Susan Materu
ATWID Publicity Secretary
CRDB wamzawadia Francis Cheka.
Bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa ICB akionyesha ngumi yake mbele ya Mkurugenziwa masoko na utafikti wa Benki ya CRDB Tuli Mwambapa wakati alipokabidhiwa cheki yake ya shilingi milioni 4 katika makao makuu ya benki hiyo leo mchana Cheka alimpiga bondia Isack Tarvez kutoka Brazil kwa KO juzi.
Bondia Francis Cheka akipokea Cheki yake ya shilingi mililoni 4 aliyopewa na benki ya CRDB kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa benki hiyo Tuli Mwambapa, baada ya kumpiga bondia Isack Tarvez kutoka Brazil kwa KO kwenye pambano lao lililofanyika katika ukumbi wa PTA viwanja vya maonyesho vya mwalimu J.K.Nerere barabara ya Kirwa jumamosi iliyopita,. hafla hiyo imefanyika leo mchana katika makao makuu ya benki hiyo mtaa wa Azikiwe jijini Dar es salaam.
WAZUNGUMZIA MADHARA YA MATUMIZI YA TUMBAKU
Mkutano wa utamaduni wamalizika Morogoro
Wasanii wa Kikundi cha ngoma za asili cha Afya Art cha Manispaa ya Morogoro wakionesha ustadi wa kucheza ngona ya ‘Ngokwa’ ya Kabila ya Wamakonde wa Mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi wakati wa hafla ya kufunga kikao cha saba cha Mkutano Mkuu wa Sekta ya Utamaduni wikiendi hii mjini Morogoro
Khatib atembelea taasisi za muungano Zenji
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano, Muhammed Seif Khatib akimsikiliza makamu mwenyekiti wa tume ya pamoja ya fedha ya jamhuri ya muungano wa tanzania bw abrahaman mwinyi jumbe jambo wakati waziri alipotembelea tume ya pamoja ya fedha ya jamhuri ya muungano wa tanzania huko zanzibar
picha na Ali Meja
Raha ya kushinda
Cheka na ngumi zake.
Fracis cheka akinyanyua juu mikono kama ishara ya ushindi wake dhidi ya mpizania wake Isack Tarvez kutoka Brazil Cheka alimshinda bondia huyo kwa Technical Knock Out katika raundi ya pili ya Mchezo huo uliokuwa wa kugombea mkanda wa Dunia wa ICB uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Dr.Lawrence Gama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Dr.Lawrence Gama wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwake Amani Makolo,wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Dr.Lawrence Gama wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Amani Makolo,wilyani Mbinga,Mkoani Ruvuma leo jioni.Dr.Gama aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM(photo by Freddy Maro)
Mashabiki kwa ubunifu wa kucheza, balaaa!!
JK Same
Rais Karume awatunuku nondo zao wanafunzi wa Ifm Zanzibar
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya sita ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani abeid Karume alipozungumza nao wakati alipowatunuku shahada juzi.
Friday, December 18, 2009
JB Mpiana awasili Dar
mwanamuziki wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo JB Mpiana akipungia mashabiki wakati alipotua Dar usiku huu tayari kwa shoo yake na Tshala Muana Ijumaa hii jijini Dar katika ukumbi wa Ubungo Plaza
RAIS JAKAYA ATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MAREHEMU GAMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha Maombolezo Nyumbani kwa Marehemu Gama Mbezi beach jijini Dar es Salaam, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na Katibu Mkuu wa CCM.
Rais Kikwete atembelea Chuo Cha wanayamapori Mweka
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanafunzi katika chuo cha wanyamapori Mweka, Bwana Gumbo Mbelwa Mhandeni alipokuwa akitoa maelezo ya tafiti juu ya uhifadhi wa pembe za wanayama mbalimbali wakati Rais Kikwete alipokitembelela chuo hicho jana