Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, December 18, 2009

DIANA IBRAHIM ndiye Kisura wa Tanzania 2009.



Huyu ndiyo Diana Ibrahim Kisura wa Tanzania 2009 aliyeshinda katika shindano la Kisura lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwene Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam


Mama Tunu Pinda katikati aliyeshika maua akiwa katika picha ya pamoja na Kisura wa Tanzania 2009 Diana Ibrahim wa tatu kutoka kulia mara baada ya kushinda kwenye shindano hilo lililofanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam, wengine ni Jaji mark Bomani mwenyekiti wa kampuni ya bia Serengeti wa kwanza kushoto na anayefuata ni mama Masaburi, kulia ni Juddy na Teddy Mapunda mwenye kilemba Meneja uhusiano wa kampuni ya bia Serengeti



Kisura wa Tanzania 2009 Diana Ibrahim katikati akiwa na washindi wenzanke Jaquiline Benson aliyeshika nafasi ya pili na Mwajabu Juma kushoto aliyeshika nafasi ya tatu mara baada ya kwatangaza washindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo.









Mavazi haya alibuni mbunifu Zamda George hayupo pichani, kila mrembo alivaa nguo iliyobuniwa kwa staili tofauti.

Visura wakipita jukwaani katika mavazi ya ubunifu kama unavyowaona katika picha.






Hawa ndiyo walioingia tano bora ya kisura wa Tanzania hapa wakipozi kwa picha.


Picha zote kwa hisani ya Fullshangwe Blog

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP