Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, December 18, 2009

Stanbic Bank (T) Ltd wasaidia watoto wa Don Bosco Dar

Juu na chini ni Wadau wa Stanbic Bank (T) Ltd wakiwa na marafiki zao wa friends of Don- Bosco.



Wafanyakazi wa idara ya fedha kutoka Stanbic bank (T) Ltd wiki hii waliwakilisha wafanyakazi wenzao wa benki katika majukumu ya kijamii pale walipowatembelea marafiki wenzao wa kituo cha FRIENDS OF DON BOSCO kilichopo Dar es salaam maeneo ya Kimara -Suka. Kituo cha DON BOSCO kina idadi ya watoto 70 wa rika mbalimbali, kuanzia umri wa miaka 4 mpaka 20, wanaosoma katika shule ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya juu.Idara ya fedha ya Stanbic Bank (T) Ltd huwa inajinyima kwa kukatana sehemu fulani ya mishahara kwa kila mwana idara, na makusanyo hayo hutolewa mara mbili kwa mwaka kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.Makusanyo pia hupokewa kutoka kwa wafanyakazi wengine wa Stanbic Bank (T) Ltd ambao hujitolea chochote, ambavyo vyote hukusanywa na kuwakilishwa kwa wahusika kwa niaba yao.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP