Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, December 23, 2009

Richard Mwaikenda apongezwa na Jambo Concepts kwa tuzo ya mpiga picha bora 2009

Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambole, Richard Mwaikenda akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto), zawadi na tuzo alizotunukiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), baada ya kuibuka Mpigapicha Bora 2009.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Benny Kisaka (kushoto), akimkabidhi hundi Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009, katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd,inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, wakitakiana heri wakati wa hafla ya kumpongeza Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009 jumamosi iliyopita.Hafla ya kumpongeza ilifanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo, Dar es Salaam jana. (PICHA KASSIM MBAROUK)


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP