Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, December 30, 2009

Precision Air yasaidia yatima kituo cha Cornel Ngaleku, Moshi


Wafanyakazi wa Precision Air wakikabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali kwa Mtawa Catherine, anayetunza watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Cornel Ngaleku Children Centre (CNCC) mjini Moshi wikiendi. Precision Air inaasili watoto wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya huduma zake kwa jamii.

Watoto wa kituo cha kulelea yatima wa Cornel Ngaleku Children Centre (CNCC) wakicheza na mfanyakazi wa Precision Air, Nia Mbaga mjini Moshi, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa chakula kwa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya wikiendi. Precision Air inaasili watoto wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya huduma zake kwa jamii


Read more...

Waandishi ndani ya TBL

Meneja wa Upikaji Bia wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL),Dar es Salaam, Kalvin Nkya (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, nchini, jinsi bia inavyochachushwa, walipotembelea kiwanda hicho, jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Maneno Mbegu.



Waandishi wa habari wakiangalia mtambo wa wa kusafisha maji taka na kuwa safi kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Mtambo huo umejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 3


Waandishi wakimsikiliza Meneja wa Upikaji Bia wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL),Dar es Salaam, Kalvin Nkya (katikati), jinsi bia inavyopikwa



Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kulia), akitoa muhtasari kuhusu utendaji wa kampuni hiyo, kwa waandishi wa habari, waliotembelea kujua jinsi bia inavyotengezwa katika kiwanda cha TBL, Dar




Read more...

Dar Cinema 01 - 07 Jan. 2010


CENTURY CINEMAX CINEMA-MLIMANI CITY
NEW WORLD CINEMA-MWENGE

Read more...

TAIFA STARS NA THE ELEPHANTS


Read more...

MAANDALIZI YA KUPOKEA WAGENI WORLD CUP 2010 HAPA NCHINI YANAKWENDA VYEMA- DR.KAWAMBWA

Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Rodger Tenga amesema tayari wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini, na amezitaja nchini hizo kuwa ni Ujerumani, Italia,DenmarkNew Zealand, Brazil,Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Wizara hiyo leo asubuhi wakati alipoelezea maandalizi ya kamati hiyo juu ya kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.
Dr. Kawambwa amesema jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni hiyo ikiwa ni mambo ya matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni wengine baadhi ya mambo wakati watakapokuwa hapa nchini, mpaka sasa televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.
Ameongeza kwamba kwa upande wa Timu ya Ivory Coast itawasili hapa nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo, waliopo kwenye picha kutoka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu

Read more...

Wednesday, December 23, 2009

Vodacom yakabidhi vifaa kwa ajili ya kombe la Mapinduzi Cup

aibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna (kushoto)akikabidhi vifaa vya michezo kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa timu ya Simba Mohamed Kajole mara baada ya kukabidhiwa na Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi (katikati)Maneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Atilio Lupala

Naibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna akionyesha jezi zitakazo vyaliwa kwenye kombe la Mapinduzi baada ya kukabidhiwa na Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania Emillian Rwejuna aliyekaa kushoto.

Naibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna na Katibu Mkuu wa ZFA wilaya ya mjini Nassor Salumu(kushoto)wakionyesha jezi baada ya kukabidhiwa na wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi Vodacom Tanzania

Read more...

Richard Mwaikenda apongezwa na Jambo Concepts kwa tuzo ya mpiga picha bora 2009

Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambole, Richard Mwaikenda akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto), zawadi na tuzo alizotunukiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), baada ya kuibuka Mpigapicha Bora 2009.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Benny Kisaka (kushoto), akimkabidhi hundi Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009, katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Concepts Ltd,inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, wakitakiana heri wakati wa hafla ya kumpongeza Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda baada ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kumtunukia tuzo ya Mpiga Picha Bora 2009 jumamosi iliyopita.Hafla ya kumpongeza ilifanyika kwenye chumba cha habari cha Jambo Leo, Dar es Salaam jana. (PICHA KASSIM MBAROUK)


Read more...

Rais Karume afungua mkutano wa Redet

Baadhi wa washiriki wa Mkutano wa siku mbili kuhusu Hali ya siasa Zanzibar unaoendelea katika ukumbi wa Salama Bwawani,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume alipoufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiufungua Mkutano wa kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar,katika ukumbi wa Salama Bwawani,ulioandaliwa na Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Read more...

Rais Karume Atembelea kituo cha kupokea umeme Fumba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya Umeme Kutoka Afrika Kusini Martin Burls,wa kampuni ya EHT,(aliyenyoosha mkono),wakati alipotembelea Kituo cha kupokea Umeme Funga kuona matatizo yaliyosababish kukosekana kwa Nishati hiyo takriban wiki tatu sasa.

Read more...

Tuesday, December 22, 2009

Waisrael Wavumbua Nyumba Aliyoishi Bwana Yesu

Mabaki ya nyumba inayoaminika aliishi bwana Yesu iliyopo huko Nazareth.

Read more...

Monday, December 21, 2009

Uzio wa hoteli aliyofungua JK juzi A-Taun wapigwa nyundo




Uzio wa hoteli mpya ya kitalii ya Snow Crest jijini Arusha eneo la Ngulelo jijini Arusha ukiwa umepigwa nyundo leo na wakala wa barabara (TANROADS), siku mbili toka JK aifungue rasmi. Picha na Woinde Shizza, Arusha

Read more...

Jiwe la kutengenezea chuma


Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC)Chrisant Mzindakaya(Kushoto) akiangalia moja ya malighafi ya kuzalisha chuma katika Eneo la Liganga mkoani Iringa.. Kulia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo Dk Gharib Bilal na katikati ni Katibu Tarafa wa Ludewa Hivi Karibuni

Read more...

Fundraising Ya ATWID Reading

Mgeni Rasmi Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh Chabaka Faraji Kilumanga

Mwenyekiti wa ATWID Susan Mzee


Fundraising ya ATWID iliyofanyika tarehe 19/12/2009 mjini Reading.Pia ilikuwa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja tangu Association of Tanzanian Women in Diaspora (ATWID) kuzinduliwa.Mgeni rasmi alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza bwana Chabaka Faraji Kilumanga.
Pia alikuwepo Mbunge wa viti maalum Martha Mlata Kulikuwepo na ngoma za asili zilizochezwa na wana ATWID pamoja na shoo ya watoto.Mwenyekiti wa ATWID Susan Mzee alitoa nasaha zake na kuwashukuru wote waliohudhuria kwa muda wao na michango yao.Zaidi ya paundi elfu mbili(£2000)zilipatikana katika hafla hiyo kwa ajili ya kutunisha mfuko wa ATWID.Asante sana
Susan Materu
ATWID Publicity Secretary

Read more...

CRDB wamzawadia Francis Cheka.

Bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa ICB akionyesha ngumi yake mbele ya Mkurugenziwa masoko na utafikti wa Benki ya CRDB Tuli Mwambapa wakati alipokabidhiwa cheki yake ya shilingi milioni 4 katika makao makuu ya benki hiyo leo mchana Cheka alimpiga bondia Isack Tarvez kutoka Brazil kwa KO juzi.


Bondia Francis Cheka akipokea Cheki yake ya shilingi mililoni 4 aliyopewa na benki ya CRDB kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa benki hiyo Tuli Mwambapa, baada ya kumpiga bondia Isack Tarvez kutoka Brazil kwa KO kwenye pambano lao lililofanyika katika ukumbi wa PTA viwanja vya maonyesho vya mwalimu J.K.Nerere barabara ya Kirwa jumamosi iliyopita,. hafla hiyo imefanyika leo mchana katika makao makuu ya benki hiyo mtaa wa Azikiwe jijini Dar es salaam.

Read more...

WAZUNGUMZIA MADHARA YA MATUMIZI YA TUMBAKU


Mwenyekiti wa chama cha Kudhibiti matumizi ya Tumbaku Tanzania Lugard Kagaruki (kulia )akiongea na wadau wa wamiliki wa mahoteli na mabaa jijini leo kuhusu madhara ya matumizi ya tumbaku na moshi wa sigara. Mwingine ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha kudhibiti matumizi ya tumbaku Tanzania Dr. Ali Mzige. (Picha na Mwanakombo Jumaa -Maelezo)

Read more...

Mkutano wa utamaduni wamalizika Morogoro

Wasanii wa Kikundi cha ngoma za asili cha Afya Art cha Manispaa ya Morogoro wakionesha ustadi wa kucheza ngona ya ‘Ngokwa’ ya Kabila ya Wamakonde wa Mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi wakati wa hafla ya kufunga kikao cha saba cha Mkutano Mkuu wa Sekta ya Utamaduni wikiendi hii mjini Morogoro

Mwanamziki mkongwe nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania, ( CHAMUDATA), Kassim Mapili ( mwenye suti) akisiliza hotuba ya mgeni rasmi ( hayupo pichani) wakati wa kufunga kikao cha saba cha Mkutano mkuu wa Sekta ya Utamaduni uliomalizika wikiendi hii.
Picha na John Nditi

Read more...

Khatib atembelea taasisi za muungano Zenji

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano, Muhammed Seif Khatib akimsikiliza makamu mwenyekiti wa tume ya pamoja ya fedha ya jamhuri ya muungano wa tanzania bw abrahaman mwinyi jumbe jambo wakati waziri alipotembelea tume ya pamoja ya fedha ya jamhuri ya muungano wa tanzania huko zanzibar



Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (muungano) Mh. Muhammed Seif Khatib akimsikiliza makamu mwenyekiti wa tume ya pamoja ya fedha ya muungano Bw. Abrahaman Mwinyi Jumbe wakati wa ziara ya waziri kutembelea taasisi za muungano huko zanzibar leo.
picha na Ali Meja

Read more...

Raha ya kushinda


Mpiga Picha Bora 2009, Richard Mwaikenda wa gazeti la Jambo Leo, akipongezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania (PPAT), Juma Dihule, wakati wa hafla ya kuwazawadia waandishi bora 2009, Dar usiku kuamkia jana. Hafla hiyo iliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Jerry Muro wa TBC ndiye aliyeibuka mwandishi bora wa jumla

Read more...

Cheka na ngumi zake.

Fracis cheka akinyanyua juu mikono kama ishara ya ushindi wake dhidi ya mpizania wake Isack Tarvez kutoka Brazil Cheka alimshinda bondia huyo kwa Technical Knock Out katika raundi ya pili ya Mchezo huo uliokuwa wa kugombea mkanda wa Dunia wa ICB uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.

Bondia Mtanzania Francis Cheka kushoto akimsukumia ngumi mpizania wake Bondia kutoka Brazil Isack Tarvez katika mpambano wa Masumbwi ya kimataifa uliofanyika jana katika ukumbi wa PTA kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam Cheka alishinda kwa KO round ya pili.

Read more...

Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Dr.Lawrence Gama.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Dr.Lawrence Gama wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwake Amani Makolo,wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma jana jioni.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Dr.Lawrence Gama wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Amani Makolo,wilyani Mbinga,Mkoani Ruvuma leo jioni.Dr.Gama aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM(photo by Freddy Maro)

Read more...

Mashabiki kwa ubunifu wa kucheza, balaaa!!




Kupagawa kimtindo kulikuwepo kama hivi,mashabiki na wapiga vyombo wa Tshalla Muana wakiwa wamepandwa na mzuka kiaina.
Picha zaidi tembelea Michuzijr Blog

Read more...

JK Same


JK akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya watu kumi na nne wa familia moja ya Shumbi waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo.
Picha na Freddy Maro

Read more...

Rais Karume awatunuku nondo zao wanafunzi wa Ifm Zanzibar

Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya sita ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani abeid Karume alipozungumza nao wakati alipowatunuku shahada juzi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akimtunuku Shahada ya Kawaida Philemon Pius Mechel,katika mahfali ya sita ya Chuo cha Uongozi wa Fedha ,Chwaka Mkoa wa Kusini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akimtunuku Shahada ya Kawaida Bimaka Abdalla Moh’d,katika mahfali ya sita ya Chuo cha Uongozi wa Fedha ,Chwaka Mkoa wa Kusini.
Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

Read more...

Friday, December 18, 2009

JB Mpiana awasili Dar

mwanamuziki wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo JB Mpiana akipungia mashabiki wakati alipotua Dar usiku huu tayari kwa shoo yake na Tshala Muana Ijumaa hii jijini Dar katika ukumbi wa Ubungo Plaza



JB Mpiana na kundi lake zima wakiwasili Dar usiku huu

Read more...

RAIS JAKAYA ATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MAREHEMU GAMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha Maombolezo Nyumbani kwa Marehemu Gama Mbezi beach jijini Dar es Salaam, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na Katibu Mkuu wa CCM.

Read more...

Rais Kikwete atembelea Chuo Cha wanayamapori Mweka

Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanafunzi katika chuo cha wanyamapori Mweka, Bwana Gumbo Mbelwa Mhandeni alipokuwa akitoa maelezo ya tafiti juu ya uhifadhi wa pembe za wanayama mbalimbali wakati Rais Kikwete alipokitembelela chuo hicho jana



Mwanafunzi wa Chuo cha Wanyamapori na uhifadhi, Mweka, Moshi vijijini Bi.Zawadi Mahinda akimwonesha Rais Jakaya Kikwete mbegu ya mti aina ya Msandali wakati Rais Kikwete alipokitembelea chuo hicho jana kujionea shughuli mbalimbali za masomo na tafiti zinazofanywa chuoni hapo. picha na Freddy Maro

Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP