Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, April 15, 2010

AICC YASAINI MKATABA WA KUUNDA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (kulia) akibadilishana na Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mkataba huo ulisainiwa katika ofisi za AICC mjini Arusha. Kushoto ni Katibu wa TUICO tawi la AICC, Rashid H. Rashid.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (katikati) akibadilishana na Mwenyekiti wa TUICO tawi la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Ezekiel Kiologwe mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la AICC. Mkataba huo ulisainiwa wiki hii katika ofisi za AICC, mjini Arusha. Kushoto ni Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (katikati) akitia saini mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi tawi la AICC. Mkataba huo ulisainiwa wiki hii katika ofisi za AICC. Kushoto ni Katibu wa TUICO Mkoa wa Arusha, Hussein Ngowo na kulia ni Mwenyekiti wa TUICO tawi la AICC, Ezekiel Kiologwe na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa AICC, Savo Mung’ong’o. (Picha kwa hisani ya AICC) .

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP