Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, April 7, 2010

JK katika sherehe za kumuenzi Mzee Karume


Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo jana mjini Zanzibar.

vijana wananchama wa UVCCM wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa kilele cha maandamano yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mjini Zanzibar kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume.


Rais Jakaya mrisho Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar(kulia) na Mwenyekiti wa jumuiya ya umojawa Vijana wa CCM Bwana Yusuf Masauni wakati wa mapokezi ya maandamano ya umoja wa vijana wa CCM mjini Zanzibar jana jioni.


vijana wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM, UVCCM wakipita mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maandamano ya kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abedi amani Karume yaliyofanyika katika viwanja vya CCm Maisara, Zanzibar jana jioni.



Mwenyekiti wa UVCCM Yusuf Masauni akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya CCM Maisara mjini Zanzibar jana jioni ambapo aliyapokea maandamano ya vijana na kuwahutubia. Leo ni Siku rasmi ya Karume na ni mapumziko nchi nzima



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP