Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, April 8, 2010

Tanzania wakumbuka Hayati Karume


Kutoka kushoto ni Rais wa Zanzibar , Amani Abeid Karume, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha wakisoma Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Abeid Karume, iliyofanyika jana ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume(katikati) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Mrisho Kikwete,pamoja na vingozi wengine wa Kitaifa na wananchi wakiwa katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,Rais wa Kwanza wa Zanzibar,wakimuombea dua katika kumuenzi tokea kufa kwake na kutimia miaka 38,huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana.


Akina mama wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika khitma ya dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar,iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.



Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Ali Mohammed Shein,akimsalimia Mama Fatma Karume,baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Rais Abeid Amani Karume,iliyoambatana na khitma na kutimiza miaka 38 tokea kifo chake huko Afisi Kuu ya CCm Kisiwandui,Mjini Zanzibar jana.










Baadhi ya wananchi wakisoma khitma ya kumuombea dua marehemu Mzee Abeid Karume,muasisi wa ASP na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,kwa kutimiza miaka 38 tokea kifo chake katika ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui jana.


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP