Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, April 8, 2010

Wajumbe wa kamati ya huduma ya jamii ya bunge watembelea ujenzi wa kampasi ya chuo kikuu cha SUZA


Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipotembelea ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) iliyopo Tunguu, nje kidogo ya mji wa Zanzibar hapo tarehe 7 Aprili, 2010. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Omari S. Kwaangw (katikati aliyefunga mikono) na Mheshimiwa Haroun A. Suleiman, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye suti nyeusi na kofia kati) walijumuika pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo na maofisa wengine wa Wizara na SUZA katika picha hii. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo inategemewa kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP