Dk. Salim Ahmed Salim akiongea na
wanahabari nyumbani kwake jijini Dar
MKUTANO WA DK. SALIM AHMED SALIM NA VYOMBO VYA HABARI
LEO JUMAPILI, TAREHE 25. 10. 2009585 MSASANI PENINSULA,
DAR ES SALAAM
Mabibi na Mabwana.
Habari za asubuhi
Nawashukuru nyote kwa kuja kwenu.
Mtakumbuka kuwa mapema mwaka huu, Bodi ya Taasisi ya Mo Ibrahim, ambayo mimi ni mjumbe mmoja wapo, ilitoa uamuzi wa kufanya sherehe za kutunuku Tuzo ya Mafanikio ya Uongozi Bora Barani Afrika, hapa Dar es Salaam.
Kutokana na uamuzi wa Kamati ya Tuzo ya Mo Ibrahim mapema mwezi huu wa kutomtunukia yeyote Tuzo hiyo, hapatakuwa na sherehe ya kutoa Tuzo kama ilivyopangwa hapo awali.
Hata hivyo, tumeamua kuitumia nafasi hii kutilia mkazo umuhimu wa Uongozi Bora barani Afrika. Kufuatia uamuzi huo, matukio muhimu mawili yameandaliwa.
Tukio la kwanza litakalofanyika jioni tarehe 14 Novemba, 2004 ni la kiutamaduni ambalo, licha ya shughuli nyinginezo, watakaohudhuria wataweza kushuhudia michango ya wasanii mahiri kama Yossou N’Dour na Angelique Kidjo, tukio ambalo litatangazwa moja kwa moja katika radio na runinga mbalimbali barani Afrika.
Sherehe hizo zitahudhuriwa na watu mashuhuri waliotoa mchango mkubwa kwa bara la Afrika pamoja na mamia ya watanzania na wageni mbali mbali kutoka pande zote za dunia.
Aidha, tukio hilo litatoa kipaumbele kuhusu nafasi, majukumu na wajibu wa vijana barani Afrika hivi sasa na katika siku za usoni.
Tukio la pili ambalo linazinduliwa kwa mara ya kwanza kabisa na Taasisi ya Mo Ibrahim, litakuwa ni Jukwaa (mbonge) ambalo litakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi, Maofisa wakuu wa serikali, Wafanyabiashara, Wanaharakati, Wasomi, Wanafunzi na Vijana kutoka nchi mbali mbali barani Afrika, ili kujadiliana mada mbalimbali zinazohusu fursa na mambo muhimu ya maendeleo.
Jukwaa litafanyika siku ya Jumapili, tarehe 15 Novemba 2009.
Kimsingi, lengo la jukwaa hilo ni kujadili na kuweka bayana fikra na mtazamo wa pamoja wa jinsi ya kushughulikia masuala ya maendeleo kwa siku za usoni.Jukwaa hilo litakuwa na Mada kuu Tatu zitakazojadiliwa katika vipindi vifuatavyo:
Mjadala wa mada ya kwanza, utahusu Haki na Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (Climate Change and Climate Justice).
Mwenyekiti atakuwa Rais Mstaafu Festus Mogae wa Botswana.
Rais Mogae ni Mtunikiwa wa Tuzo ya Taasisi ya Mo Ibrahim kwa mwaka 2008, na ni miongoni mwa wawakilishi wanne maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon, kuhusiana na masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
Mjadala wa mada ya pili, utahusu Kilimo na Usalama wa Chakula (Agriculture and Food Security).
Mwenyekiti wa mjadala huo atakuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Kofi Annan.
Bw. Annan ni Mwenyikiti wa Bodi ya Mshikamano wa Mapinduzi ya Kijani katika Afrika – AGRA.
Mjadala wa mada ya tatu, utahusu Ushirikiano wa Kikanda wa Kiuchumi (Regional Economic Intergration) ambao Mwenyekiti wake ni Bwana Abdoulie Janneh.
Bwana Janneh ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Afrika ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano huu utakuwa ni Muhimu, utakaowaleta watu kutoka sehemu zote za Afrika.
Wadau wote hawa wanakuja pamoja wakati ambapo kwa upande mmoja kuna maendeleo ya jumla katika bara la Afrika lakini kwa upande mwingine kuna vikwazo vya kutia wasiwasi katika baadhi ya nchi na hivyo kujenga umuhimu wa wadau na taasisi mbalimbali kukutana na kutafuta ufumbuzi na changamoto ambazo zinakabiliwa barani la Afrika.
Kwa kufanya hivyo, tutaendeleza mjadala na mazungumzo kuhusu changamoto za msingi ambazo zinakabili bara la Afrika.
Taasisi ya Mo Ibrahim inaamini kuwa ili kutoa mchango madhubuti katika juhudi za kuendeleza uongozi bora katika Afrika, taasisi haina budi kusaidia kufanikisha mijadala na mazungumzo mbalimbali yanoyohusu changamoto za msingi za muda mrefu zinazolikabili bara letu.
Baada ya kueleza hayo, ninapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kazi moja kubwa ya Taasisi ya Mo Ibrahim, kazi ambayo tunaiona kuwa muhimu zaidi kuliko Tuzo yenyewe.
Kazi hiyo ni ile kazi ambayo tathmini yake huwa ni mojawapo ya vigezo muhimu katika uamuzi wa kupatikana kwa TUZO.
Ninakusudia kueleza Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim kuhusu Uongozi Bora barani Afrika (Ibrahim Index on African Governance), chombo maridhawa katika juhudi za kuendeleza uongozi katika Afrika.
Tarehe 5 Oktoba mwaka huu tulitangaza vigezo hivyo huko Cape Town, Afrika ya Kusini.
Vigezo hivyo ni vipimo kamili vya kupimia usawa katika uongozi.
Ni kipimo cha uongozi bora ambacho hutoa taarifa na kuwawezesha wananchi kuendesha serikali na taasisi zao kwa kuwajibika.
Hivyo vigezo vilivyoandaliwa na Taasisi ya Mo Ibrahim ni pamoja na michango ya watafiti maarufu, taasisi, na ule mchango wa Kamati ya Ushauri ambayo inajumlisha Wasomi wa Afrika na Watafiti.
Vinalenga kuchachua mjadala kwa njia makini inayoweka misingi imara katika uongozi bora katika Afrika.
Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim hupima pia kwa kiasi gani huduma zinawafikia wananchi kupitia serikali na asasi zisizo za serikali.
Vigezo vya Mo Ibrahim vimezingatia misingi mikuu minne kama ifuatavyo:
1. Usalama na Utawala wa Sheria
2. Ushirikishaji na Haki za Binadamu
3. Fursai na Uchumi Endelevu
4. Maendeleo ya Watu
Tathmini ya Taasisi ya Mo Ibarahim hupima utawala bora kwa kutumia vigezo 84 ambavyo hukusanywa kwa hali ya kutosheleza inayohusisha taarifa na takwimu (data) ambazo zinatathmini uongozi bora barani Afrika.
Vigezo vinahusisha:
Usalama wa mtu BinafsiUtoaji wa Elimu na Ubora wa Elimu yenyeweHaki za Watu (Civil Liberties)Ubora wa MiundombinuUhuru wa MahakamaVigezo vimegawanywa tena katika sehemu ndogo ndogo (Sub-categories) kumi na tatu zikiwemo:
-Usalama wa mtu BinafsiUtawala wa SheriaHaki za Binadamu(Usawa) wa JinsiaMenejimenti ya UchumiMazingira na Maendeleo ya VijijiniElimuSasa ningependa kugusia suala la TUZO.
Kama mnavyojua, Kamati ya Tuzo haikuweza kuteua mshindi mwaka huu.
Kwa niaba ya Bodi ya Taasisi ya Mo Ibrahim, Rais mstaafu wa Botswana Ndugu Kitumire Masire alisoma tamko la Kamati ya Tuzo kama ifuatavyo:
“Taasisi ya Mo Ibrahim iko mstari wa mbele kusaidia uongozi wa Afrika ili kusukuma mbele hali ya Uchumi na Ustawi wa jamii wa watu wa Afrika.
Lengo la Taasisi ni kuendeleza na kuinua uongozi bora na kutambua umahiri katika uongozi wa Afrika.
Kamati ya Tuzo inatambua maendelea yaliyofikiwa katika baadhi ya nchi za Afrika kuhusiana na uongozi bora na wakati huo huo kuzingatia matatizo yaliyopo katika baadhi ya nchi.
Mwaka huu Kamati ya Tuzo iliwazingatia baadhi ya viongozi wenye sifa na kuheshimika (Credible) lakini baada ya kuzingatia kwa undani na umakini Kamati haikuweza kuchagua mshindi.”
Muundo wa Kamati ya Tuzo unajumlisha viongozi mashuhuri duniani ambao wanaamini kwa dhati kuisadia Afrika katika mapambano yake katika maeneo mbali mbali.
Kamati hiyo ipo chini ya mwenyekiti aliyepokea Tuzo ya Amani ya Nobel, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Tuzo ni pamoja na Marti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland ambaye pia ni Mtunukiwa wa Tuzo ya Nobel, Mohamed El Baradei, ambaye ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na Mtunukiwa wa Tuzo ya Nobel; Mary Robinson, Rais Mstaafu wa Ireland na Kamishna Mkuu wa zamani wa Umoja wa Matifa wa Haki za Binadamu; Aicha Bah Diallo, Waziri wa Elimu Mstaafu wa Guinea na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Mstaafu wa UNESCO pamoja na Mama Graca Machel, Kiongozi mashuhuri wa harakati za Haki na misaada ya kibinadamu na Mtetezi mkubwa wa Haki za Maendeleo ya Watoto.Mimi kama mmoja wapo wa wajumbe wa kamati hiyo ya TUZO, ningependa kusisitiza tu kuhusu maamuzi hayo na kauli iliyotolewa.
Mtakapoanza kuuliza maswali ni vema niwajulisheni waziwazi kwamba sitajibu maswali yeyote yale kuhusu mwenendo wa majadiliano ya Kamati ya Tuzo.
Kifungu cha 11 cha hadidu za rejea kinasema:“Majadiliano na viambatisho vyovyote vya Kamati ya Tuzo ni SIRI KUU. Mjumbe yeyote wa kamati ya TUZO haruhusiwi kutoa siri ya mwelekeo wa mazungumzo au matokeo ya kutofaulu kwa mtu yeyote yule na wakati wowote ule.
”Hata hivyo, kama mjumbe wa Bodi ya Taasisi, ningependa nitoe maono machache:Kwanza kabisa, Wajumbe wa kamati ya Tuzo huzingatia itikadi ya Tuzo na hufanya kazi kwa mujibu wa kanuni na miongozo iliyowekwa.
Wanafanya hivyo kwa misingi ya uhuru, uaminifu na bila upendeleo.
Pili, katika kumchagua mshindi, Bodi hutegemea kwamba Kamati ya Tuzo itatia maanani mambo kadhaa yakiwemo: Utendaji wa nchi kama ulivyopimwa kwa kutumia Vigezo vya Taasisi ya Mo Ibrahim pamoja na chambuzi nyingine zinazoheshimika na kukubalika.
Viongozi wanaostahili ni watendaji wakuu wa nchi au Serikali waliostaafu, ambao wamepata madaraka kwa njia ya uchaguzi huru na halali na kustaafu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita; baada ya kuitumikia nchi kwa mujibu wa Katiba kama ilivyoainishwa wakati alipochukua madaraka.
Kwa mujibu wa maelezo haya, kipindi kinachozungumziwa hapa ni kile cha mwaka 2006, 2007 na 2008
Read more...