Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, October 15, 2009

Maria Nyerere akimbiza mwenge

Mama Maria Nyerere akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi mara baada ya mwege huo kuwasili nyumbani kwake kijijini Butiama wilayani Musoma katika mkoa wa Mara kwa ajili ya kuuwasha mwenge wa Mwitongo. Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha. Mwenge huo unatarajiwa kuzimwa kesho kijijini Butiama huku siku hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kufa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi akiuwasha mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwenge wa Mwitongo ukiwaka baada ya kuwasha na utaendelea kuwa hivyo hadi utakapozima wenyewe.


Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2009 wakiomba dua katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo kijiji cha Butiama wilayani Musoma mkoa wa Mara.


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP