Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, October 13, 2009

Maandalizi ya siku ya nyerere yapamba moto Butiama

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Butiama wakiangalia albamu zenye picha za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere walipotembelea banda la Idara ya Habari (Maelezo) wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana Tanzania yanayofanyika katika kijiji hicho. Maonyesho hayo yanakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere na kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru yatakayofanyika jumatano wiki hii.Picha na Anna Nkinda - Maelezo






Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wa kijiji cha Butiama wilayani Musoma katika mkoa wa Mara wakifanya mazoezi ya halaiki kwa ajili ya maandalizi ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kilele cha mbio zamwenge wa Uhuru. Sherehe hizo zitafanyika katika kijiji hicho siku ya jumatano.



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP