Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, October 7, 2009

Prof. Mwandosya awatoa hofu wakazi Jijini


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Marck Mwandosya akizungumza na waandishi wa habari leo wakati alipotolea ufafanuzi juu ya uvumi ulioenea kwamba kuna watu wameweka sumu katika mto Ruvu mto ambao ndiyo una chanzo cha maji cha mtqambo wa Ruvu Juu kinachotegemewa na wakazi wote wa jiji la Dar es alaam kwa ajili ya matumizi ya maji, hata hivyo jumla ya watu wanne wamekamatwa na polisi baada ya kukutwa wakiuza samaki wanaodhaniwa kuwa wamevuliwa kwa njia haramu za uvuvi
Waziri Marck Mwandosya amesema wakazi wa jiji la Dar es salaam wasiwe na wasiwasi wowote bali waendelee kutumia maji hayo kwa ni uchunguzi wa kina umefanyika na kugundua kwamba hakuna sumu yoyote ambayo imepatikana katika chanzo cha mtambo wa Ruvu juu ambako ndiyo husukuma maji kuja katika jiji la Dar es salaam kwa matumizi ya wakazi wa jiji.
Amesema eneo ambalo tukio hilo lilitokea ni sehemu iitwayo Kwala katika Wilaya ya Morogoro Kusini lilitiwa sumu kwa lengo la kuvua samaki na wavuvi haramu ni kilomita sabini mpaka kufikia kwenye chanzo cha mtambo wa Ruvu Juu, hivyo hakuna wasiwasi wowote wa kuwepo kwa sumu hiyo na mpaka sasa Sampuli ya maji iko kwa mkemia mkuu ili kubaini kama kuna tatizo lolote pamoja na kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha hakuna aina yoyote ya sumu katika maji hayo, wanaofuatia kwenye picha ni Kaimu katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Damas Shirima na mwisho ni Mkurugezi wa Idara ya Habari Maelezo Clement Mshana.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP