Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, October 16, 2009

Sia apewa chake na TTB


Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Peter Mwenguo kushoto akimkabidhi kompyuta yenye thamani ya shilingi 1.1 Balozi wa Utalii nchini (Miss Domestic Tourism) Sia Ndaskoi katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za bodi hiyo jengo la IPS jijini Dar leo, anayeshuhudia katikati ni Maria Mmari Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii, Sia pia amekabidhiwa cheki yenye thamani ya shilingi 2.2.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Peter Mwenguo akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano wa bodi hiyo leo wakati alipomkabidhi zawadi zake balozi wa Utalii nchini Miss Domestic Tourism baada ya kunyakua taji hilo kwenye shindano la Vodacom Miss tanzania mwanzoni mwa mwezi huu ambapo mrembo Miriam Gerald kutoka Mwanza aliibuka mshindi, kulia ni Maria Mmari Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii na kushoto ni Hashim Lundenga Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP