Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, August 12, 2009

JK ziarani mbinga

JK akikagua kivuko katika mto Lituhi, wilayani Mbinga kinachotoa huduma kati ya Wilaya ya Mbinga na Ludewa,mkoani Iringa. Wananchi na viongozi wa wilaya hizo walimweleza kuwa kivuko hicho hakijatatua kero ya usafiri kaztika eneo hilo kwa kuwa hufanya kazi miezi michache sana kutokana na kuzidiwa nguvu wakati wa mvua nyingi na kutatizwa na mchanga wakati wa kiangazi. Viongozi wa eneo hilo waliiomba serikali kujenga daraja kama ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.

JK akimjulia hali Bi.Martha Mahundi na motto wake mchanga aliyejifungua kwa upasuaji katika kituo cha Afya Lituhi,wilayani Mbinga,Mkoani Ruvuma, jana.Wa pili kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mbinga Dr.Emmanuel Mapunda na kushoto ni mganga mkuu wa kituo hicho Martin Ndunguru. JK alikitembelea kituo hicho cha Afya ambapo Askofu Mapunda aliomba kituo hicho kupandishwa hadhi na kuwa hospitali kamili.

Mama Salma Kikwete akimtwika maji Bi Magrethi Kayombo wa kijiji cha Litumba Lihamba muda mfupi baada ya JK kuzindua mradi wa maji kijijini hapo, huku JK na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Mh. John Komba wakishuhudia


JK akiwasalimu baadhi ya wanafunzi wakati aliposimama kwa muda katika kijiji cha Ruanda wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma jana. JK alikuwa anaelekea kijiji cha Lituhi ambapo alizindua mradi wa maji, kutembelea kituo cha afya na kuzungumza na wananchi. Picha na Freddy Maro wa Ikulu



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP