Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, August 11, 2009

TUZO ZA VINARA WA FILAMU 2009 KUWASHIRIKISHA WANANCHI

TUZO ZA VINARA WA FILAMU
2009 KUWASHIRIKISHA WANANCHI

Mchakato wa kutafuta vinara wa filamu Tanzania kwa mwaka huu utawahusisha wananchi kupitia upigaji kura.

Wapenzi wa tasnia ya filamu nchini watapendekeza filamu ambazo wanaona zinastahili kuingia tuzo za vinara wa filamu. Mbali an wananchi pia kuna taasisi mbali mbali kama vile kampuni ya uhasibu inayotambulika kimataifa litasimamia zoezi la mapendekezo ya filamu.

Filamu zenye kura nyingi ndizo zitakazoingia katika tuzo hizi. Pia filamu zitakubaliwa kutokana na mapendekezo ya waandaaji na majaji.

Kuteua filamu ni kwa njia ya ujumbe mfupi ambapo mpenzi atatakiwa kuandika neon vinara kasha jina la filamu anayoipenda na kutuma kwenda 15551 kwa gharama ya Tshs 300.

Vipengele vitakavyowaniwa mwaka huu katika tuzo za vinara ni Mwigizaji bora wa kiume na wa kike wa mwaka, Mwigizaji chipukizi wa kiume na wa kike, Filamu bora ya mwaka, Muongozaji bora wa Mwaka, Mwandishi bora wa filamu, Adui bora, Msanii bora msaidizi wa kiume na wa kike, Mhariri bora wa mwaka, Mtunza Sauti bora, Mtunza Mwanga bora, Mpiga picha bora wa mwaka, Mtayarishaji bora wa filamu, Mtunzi bora wa filamu, Mapambo na maleba bora, msanii maarufu wa kiume na kike na Tuzo ya heshima.

Vipengele vilivyoongezwa ni mtunza taa bora, mtayarishaji bora wa filamu (producer) na wasanii maarufu wa kike na wakiume (People’s choice Award).

Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa baada ya upigaji kura.

Filamu zinazostahili kupendekezwa ni zile zilizotengenezwa kuanzia januari 2009. Filamu zitakazo ingia moja kwa moja ni zile ambazo bado hazijaingia sokoni lakini yatawasilishwa na watengeza filamu wenyewe.

Zoezi la kupendekeza filamu litafanyika hadi septemba 30 kabla ya kupatikana wahusika kwenye kila kipengele kabla ya wananchi kupiga kura kuwapata washindi.

Khadija Khalili
Mratibu

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP