Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, August 11, 2009

Mazishi ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akimfariji Mjane wa Marehemu wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Mama Mai Maria Msika wakati alipomtembelea nyumabni kwake nje kidogo ya Mji wa Harare kutoa salamu za ploe kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joseph Wilfred Msika. Katikati ni Mama Mwanamwema Shein.

Jeshi la Wananchi wa Zimbabwe likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Joseph Msika(85) aliyekuwa Makamu wa Rais Wa zimbabwe tayari kwa maziko katika makamburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliiwakilisha serikali katika Maziko hayo yakiyofanyika jana.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Joseph Wilfred Msika nyumbani kwake kabla ya maziko ambayo yamefanyika jana katika makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Nyuma ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein. Dk Shein ameiwakilisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maziko hayo.Picha na Clarence Nanyaro/VPO


0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP