Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, August 20, 2009

Voda yapata mdhamini mwenza Miss Tanzania


Mkurugenzi wa kampuni ya Samsung Patricia King'ori akimkabidhi simu aina ya Samsung Star mmoja wa warembo walioshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka jana Frolence Josephat wakati kampuni hiyo ilipotangazwa kuwa mdhamini mwenza wa Miss Tanzania mwaka huu kulia ni Ramesh Shah Jaji mkuu Miss Tanzania na kushoto ni Hashim Lundenga Mkurugenzi Miss Tanzania.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Samsung Patricia King'ori akionyesha moja ya simu zinazotengenezwa na Kampuni hiyo ambazo warembo watakaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania watazawadiwa Kampuni ya Samsung imeingia mkataba wa kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa Dola za Kimarekani 55.000 na itawapatia warembo wote watakaoshiriki shindano hilo simu aina ya (Samsung Star), wengine waliopo katika picha ni Hashim Lundenga mkurugenzi Miss Tanzania katikati na mwisho ni George Rwehumbiza Meneja Udhamini na Mawasiliano Vodacom Tanzania, hafla ya kutangaza udhamini hulo imefanyika jana Savvanah Lounge katika Hoteli ya City Paradise jijini Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP