Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, August 19, 2009

TIGO YAJA NA ZAWADI


Kulia ni meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando akizindua rasmi na kuelezea jinsi ya kushiriki promosheni mpya na mahali kwa KUKWARUZA na kujishindia zawadi kupitia promosheni mpya ya Tigo itakayojulikana kwa jina la Kila Mmoja Anashinda. Wateja wa Tigo sasa watajishindia pesa Taslim na muda wa maongezi. muda wa maongezi shilingi 100, 250, 500 na 750 na pesa taslim ni 200,000, 300,000, na 1,000,000.Kushoto ni Meneja Matangazo wa Tigo bw, Redemtus Masanja

TIGO yazindua Kila Mmoja Anashinda! Promosheni KWARUZA TIGO USHINDE HADI MILIONI 1,Tarehe 18 Agosti 2009, Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo imezindua rasmi promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya kabla itakayojulikana kwa jina la "KILA MMOJA ANASHINDA
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi wa Tigo Jackson Mmbando alisema Promosheni hii ni kabambe kabisa na tumeianzisha ili kuwafaidisha wateja wetu wa malipo ya kabla, tunaizindua rasmi leo Ambato zawadi za pesa taslim na muda wa maongezi zitashindaniwa na wateja wetu walioko nchi nzimaTayari mzigo wa vocha za KILA MMOJA ANASHINDA zimeshawafikia wachuuzi.
Vocha hizi zinazomuwezesha mteja kujishindia ni vocha za shilingi 2000, 5000, 10,000 tu.Ikiwa mteja atajinunulia muda wa maongezi wa 2,000, 5,000, 10,000 atapata zawadi ya muda wa maongezi 100, 250, 500 au 750 pia kutakuwa na zawadi ya pesa taslim 300,000, 500,000 au 1, 000,000. kila vocha itakuwa na sehemu ilioandikwa neno (ZAWADI) na kufichwa ambapo mteja atatakiwa kukwaruza na akishaijua zawadi yake kuwa ni vocha au pesa taslim atafuata maelekezo yafuatayo ili kujipatia zawadi yake mara moja.
Ikiwa ni muda wa maongezi mteja mara baada ya kukwaruza atapata namba za siri na atafuata utaratibu wa kawaida wa kuingiza vocha yaani *104*xxxxxx# ok hapo hapo atajipatia muda wake wa maongezi.Ikiwa ni pesa taslim mteja atajishindia 300,000, 500,000, au 1,000,000 baada ya kukwaruza sehemu ya ZAWADI atapata namba itakayopiga na kupata maelekezo ya jinsi ya kujichukulia kitita chako haraka.Atakaeshinda muda wa hewani atapatiwa muda wa hewani nasi vinginevyo, Ikijishindia pesa taslim lazima uje na vocha yako ya zawdi ndio utapatiwa zawadi yako.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP