Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Saturday, August 29, 2009

NGOMA AFRICA Wanapofunga Mtaa Hamburg Ujerumani



Ras makunja na kikosi chake The Ngoma Africa band,juzi 21-08-2009waliufunga mtaa mrefu katikati ya jiji kubwa la Hamburg,Ujerumani.katika maonyesho ya Alafia -Afrika Festival,na kusababisha ulinzi mkali kuwepo katika onyesho hilo , mbele ya jukwaa kulijaa mashabiki ambao walikuwa wakidai kuwa ngoma africa ni bendi yao ya damu.
Nyuma ya jukwaa kulikuwa kumejaa Polisi ambao nao walisema kuwa baada ya kumalizika onysho hilo lazima Makunja na kikosi chake wasindikizwe na Ulinzi na hakuna mshabiki wa kuwasogelea! hiyo ilikuwa ikimaanisha FFU wa Ngoma Africa chini ya ulinzi wa washabiki na polisi walikuwa salama kabisa.
Poromota wa onyesho hilo aliwatangazia washabiki kabla ya muziki kuanza kuwa "Washabiki wanaombwa kucheza muziki mbele ya jukwaa" tafadhali nyuma ya jukwaa ni sehemu ya ulinzi tuu! jukwaa lipo kati! upande wa mbele washabiki na upande wa nyuma polisi,Ras Makunja na Ngoma Africa yake wamewekwa mtu kati!!



Ras Makunja akiwa na bendi yake Ngoma Africa

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP